Nilipita kipenyo kimoja Sudan Temeke niliona mabinti wameweka mapaja nje wanatangaza biashara saa nne asubuhi.
Nilijua ni hostel za wanafunzi kwa harakaharaka. Ila nilipounganisha nukta nikakumbuka na kufahamu kuwa wako pale kibiashara.
Serikali yenye vyombo vya ulinzi na usalama zaidi ya vinne imeshindwa kukomesha ushetani huu wa mabinti kujiuza na wanaume kununua?
Nilipita Sokota usiku saa nne niliona barabara wameenea wadada poa, dereva alipunguza mwendo wadada wakaanza kutukaribisha huduma.
Je, wahusika wakuu wa kuzuia huu uhuni nao ni wanufaika wa hii biashara Tanzania?
Wananufaika kwa kununua bidhaa zao au wameamua kupuuzia siku zipite?
Ningekuwa na mamlaka kubwa ningeikomesha hii biashara nchini ndani ya siku 3 tu.
Kama hamtaki au hamuwezi kudhibiti basi muwarasimishe ili serikali ipate kipato kidogo.
NI wazo zuri ila serikali kuhalalisha umalaya si wazo sahihi kwani kodi watakayolipa pengine haitalingana na kipato chao.
Mnatakiwa watanzania wachache kama wewe wenye muono kama wako kuanzisha taasisi ya kushughulika na mambo kama haya.
Na si lazima uombe fedha serikalini pekee waweza hata kuomba fedha kutoka vyanzo vya nje ya nchi na ukafanikiwa cha msingi ni uamini fu na lengo lako.
Kwanza, umalaya unahusisha usafirishaji wa binadamu yaani wasichana wadogo, udhalilishaji wa kijinsia,matumizi ya madawa ya kulevya, mimba za bila kupangwa na madudu mengine,
Pili kwenye mfumo wa kijamii umalaya huleta ushawishi mbaya kwamba ndo dili mjini hivyo hapo ndipo serikali inapotakiwa kushughulikia hii kwa kuweka sheria inayomlinda malaya na hata huyo mnunuzi wa huduma.
Mambo yafuatayo yanapaswa kutekelezwa ili kuhakikisha malengo yako yanatimia:
1.Malaya wote wanatakiwa kuandikishwa na kupewa vitambulisho.
2, Majumba na sehemu zote zinazohusiana na umalaya zijulikane na zitozwe kodi kubwa kulingana na mapato yao.
3, Iwe ni kinyume cha sheria kujitangaza hadharani
4. Vituo vya afya viwe na taarifa zote muhimu za wagonjwa wanaotokana na shughuli za uzinzi na umalaya.
5. Mayala wote waweke taaarifa za kumbukumbu za walotembea nao.
Ukiweka sheria ndogondogo kama hizi zinaweza kupunguza kidogo kasi ya ukuaji wa haya mambo.