JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 8,556
- 18,428
Tutaheshimiana Tu,
Kama US na China, ni Tit for tat
Kama US na China, ni Tit for tat
Mkuu. Unawaona kenya wanavyo tu treat? Hawapo tayari kwa mazungumzo wapo ktk harakati za kuharibu na kuhujumu uchumi wa Tz. Hawa jamaa wanajua wanachofanya siyo kwamba hawajui. Tutazungumza vizuri baada ya kuwa tumebanana mbavu kisawa sawa. Hapo tutakuja jadiliana kwa heshima. Nchi hizi si lazima ziwe na urafiki.
tulizana, hatujafikia huko, na ni bora kuanzwa kuliko kulianzisha, kwenye magombano hata kama umekamia kuumiza make sure upande unaopingana nao ndio wawe wabeba lawama ya ugomvi, create a situation to justify your actions in a fight.Tufunge biashara zao zote TZ. Hakuna kuuza wala kununua. Inawezekana ktk biashara hizo wakatufanyia hata hujuma. Ili kuonesha kuwa TZ kuna maambukizi makubwa ya Corona.
Tanzania haitegemeni uwepo wa Kenya nayo iwepo. Kwa miaka mingj hawa jamaa wamekuwa wakituona Tz kama wanyonge wao sana.hatuwezi acha hali hii iendelee.
Kwa sasa hakuna tunalotegemea Kenya kusema kuwa tutaathirika sana ikiwa sote tutaamua kuuonesha uanaume.
Heshima haiji isipokuwa kwa kujiheshimu kwanza. Jamaa wameongea sana,wametuponda sana kwa dharau.sasa ufike wakati. Waelewe kuwa hata bubu kuna hatua akifika anaweza tamka maneno machache.
Tufunge mpaka, tuwaambie waTZ walioko Kenya warudi Tz na Wakenya waliopo Tz warudi kwao. Tuagane kwa amani tu maana tunakolekea tunafahamu jinsi Wakenya walivyo Violent. Wanaweza anza wadhuru watu wetu kule kwao.
Pia tuzuie bidhaa kutoka na kuingia Kenya. Tubaki kwetu na vyetu na wao wabaki kwao na vyao. Kwa hali iliyopo sasa ni vyema kila mtu ashike hamsini zake.
Na kwa wale Watanzania wanaodhani wao wana Ukenya mwingi ndani yao wahamie Kenya tu, maana kuna wapuuzi ambao wanapenda sana kujipendekeza mataifa mengine.
Katika hili tunasimama kama Watanzania vyama ni vya baadaye sana.
Mkuu sipingi mtazamo au ushauri wako kwa serikali. Je ushauri wako huu una faida yoyote kwa wananchi wa kawaida, wafanyabishara, wakulima nk? Inawezekana haya maamuzi yako yanaendeshwa na emotions za kisiasa zaidi, huku ww kama mwanasiasa ukijua hutapata tatizo lolote, maana mshahara wako uko palepale. Kinachoendelea kwa sasa naona ni mvutano wenye kubeba ubabe wa wanasiasa zaidi, kuliko makundi yenye shughuli za kiuchumi kwa nchi hizi mbili. Ngoja tuone maamuzi ya wanasiasa wa nchi hizi 2, dhidi ya maslahi ya nchi zao.
Atakatwa katikati upande utaenda dar mwingine nairobiAsa mtoto wa legendary Diamond kwa Natasha itakuaje?
Tuache kujiona wanyonge kila siku. We can stand alone. Mambo ya anga ni sehemu ya Muungano. Hii ni collective decision na naunga mkono. Wao wanatakiwa kujitathmini piaHii naona italeta mgogoro mwengine ndani ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Katika haya maamuzi ya kuzuwia ndege za KQ kutotuwa Airports za Tanzania nina wasiwasi mkubwa kama Wazanzibari wameshirikishwa katika kutoa haya maamuzi. Zanzibar wanategemea kwa kiasi kikubwa bidhaa kutoka Kenya kupitia soko la Mombasa na kuingiza mizigo kwa njia ya ndege kwa kutumia KQ. Itawaathiri kwa kiasi kikubwa kibiashara. Ukitiilia maanani kuna mizigo mengi tu sasa hivi iko transit pale NBO inasubiri kwenda ZNZ na DAR kwa kutumia hiyo KQ. Hilo Serikali yetu hawajalifikiria. Wangetowa muda wa kama wiki 2 ili kutatuwa hilo tatizo kwa kuwafikiria wafanya biashara wao.
My point is bila kenya hatuwezi. But ndio wateja wetu wakubwa.We wont lose anything.tuna nchi ambazo tutafanya nazo biashara vizuri tu.tumejivika ulemavu kuwa bila kenya hatuwezi uza mazao yetu.no way. Hatuwezi bembeleza ujirani jirani yako si mlie karibu naye.jirani yako ni mtu mnayesaidiana na kuelewana.
Usa wenyewe huo ukuta hawajajenga mpaka leo. Senate ilisitisha mpango wa trump.Sasa serikali ingeweka na pazia kabisa ili na mlima Kilimanjaro usionekane upande wa Kenya...[emoji41][emoji41]
Alafu tusubiri nyumbu wa Serengeti wanapo rudi upande wa Tanzania, kisha tujenge ukuta mkubwa kama wa USA na Mexico....[emoji2955][emoji2955]
Alafu baada ya hapo tuzuwie bidhaa zote za biashara zisiingie Tanzania kutoka Kenya....[emoji850][emoji850]
US na china wako another level.Tutaheshimiana Tu,
Kama US na China, ni Tit for tat
Hapa tu nikacheka na kuona unapiga siasa zilezile za propaganda. Eti...
"...kupigwa bao tokana na kasi na viwango vya Rais Magufuli...."
Hizi fikra za kutukuza mtu badala ya mikakati ya kuinua viwango vya maisha ya watu masikini waliopigika, ndiyo inatufanya tuendelee kuwa masikini wa kutupwa chini ya utawala wa CCM wa mika zaidi ya 60...!!
Kwa hiyo wanapotupush kwenye kona tuwafanyeje? Hata vita na Idd Amini ilikuwa na madhara lakini "some times you got to fight when you are a man"Haya mambo yanahitaji kutatuliwa kwa utaratibu, tunawahitaji kwa ustawi wa wakulima wetu na wanatuhitaji kwa bidhaa za viwandani. Watakaoumia si viongozi bali ni sisi wananchi wa kusifu na kushangilia.
Uzalendo wa namna hii ni uharibifu na wa hatari, USA anaharibu soko la China kwa wakulima wake lakini kwenye bajeti anatenga mabilioni kwa wakulima kama fidia.
Sisi bado maskini sana kuvimbiana namna hii hatukuhitaji kabisa. Maamuzi ya kutumia hisia namna hii bila kufikiria ni hatari kwa ustawi wa nchi yetu.
Mgogoro wowote ule utatuzi wake unafanyika kwa hatua. Hatua za mwanzo ambazo huwa zinajaribu kulinda uhusiano na masilahi ya pande zote mbili ndizo ambazo hutangulia kupewa kipaumbele.Kwa hiyo wanapotupush kwenye kona tuwafanyeje? Hata vita na Idd Amini ilikuwa na madhara lakini "some times you got to fight when you are a man"