Serikali, katika hili tuwawahi Wakenya kwa KO kabla hawajatuwahi wao

Tutaheshimiana Tu,
Kama US na China, ni Tit for tat
 

Mkuu sipingi mtazamo au ushauri wako kwa serikali. Je ushauri wako huu una faida yoyote kwa wananchi wa kawaida, wafanyabishara, wakulima nk? Inawezekana haya maamuzi yako yanaendeshwa na emotions za kisiasa zaidi, huku ww kama mwanasiasa ukijua hutapata tatizo lolote, maana mshahara wako uko palepale. Kinachoendelea kwa sasa naona ni mvutano wenye kubeba ubabe wa wanasiasa zaidi, kuliko makundi yenye shughuli za kiuchumi kwa nchi hizi mbili. Ngoja tuone maamuzi ya wanasiasa wa nchi hizi 2, dhidi ya maslahi ya nchi zao.
 
tulizana, hatujafikia huko, na ni bora kuanzwa kuliko kulianzisha, kwenye magombano hata kama umekamia kuumiza make sure upande unaopingana nao ndio wawe wabeba lawama ya ugomvi, create a situation to justify your actions in a fight.
 
Kwa mtizamo wako. Je unadhani sasa ni sawa watanzania wasiingie kenya ila wakenya waingie tanzania? Huu ndo utakuwa mtizamo ambao si wa kisiasa kwa mujibu wako?

Fitna na hujuma hizi zilianza mapema sana kwenye suala la covid 19 kumbuka madereva wetu walivyonyanyaswa na kubagizwa. Hilo tulipaswa tuliache?

Sasa wametangaza kuwa sisi si moja ya nchi ambazo ndege zetu zitaingia kenya.sawa. je sisi tufanyeje?tuseme zao ziendelee kuingia?

Mi nadhani kuna kipindi tusimamie kile tunachoamini.ndo heshima itakuwepo.kuna siku wakenya watasema wanaume wa tanzania wasioe wanawake wa kenya ila wanaume wa kenya waje kuoa watanzania.utakuwa tayali?

 
Tuache kujiona wanyonge kila siku. We can stand alone. Mambo ya anga ni sehemu ya Muungano. Hii ni collective decision na naunga mkono. Wao wanatakiwa kujitathmini pia
 
We wont lose anything.tuna nchi ambazo tutafanya nazo biashara vizuri tu.tumejivika ulemavu kuwa bila kenya hatuwezi uza mazao yetu.no way. Hatuwezi bembeleza ujirani jirani yako si mlie karibu naye.jirani yako ni mtu mnayesaidiana na kuelewana.
My point is bila kenya hatuwezi. But ndio wateja wetu wakubwa.
Huwezi kufungua duka halaf yule mteja anae nunua vitu vingi ukamnunia. Thats childish.
Hayo mataifa mengine ambayo tunafanya nayo biashara tuna mahusiano mazuri nayo? Je wakulima wetu wananufaika direct bei bora za mazao?
Sisemi tukubali kupelekwesha. Tuwe firm yes..
But hapa tuna loose wote.
Tuweke pride pembeni
 
Usa wenyewe huo ukuta hawajajenga mpaka leo. Senate ilisitisha mpango wa trump.
 

Kwa hiyo kiongozi, kusema Magufuli tu kumekuspa mzio!. Chuki za nini kwa raisi anayefanya mambo makubwa kutoka hasi aliyoikuta? Wapi umeona nimeongea CCM wala Chama Cha Siasa? Mbona mimi sina chama? Ebu angalia vizuri tena kiongozi.

Umaskini hautaisha kwa kukataa kweli ama kwa maamuzi ya mihemuko au kupalilia chuki na matengano. Tuungane na tukubali kutumia taaluma na vipaji vy akila mtu kama vinatuletea maendeleo. Huwezi kuondoa umaskini kwa kukopa fedha za kula. Raisi Magufuli amejikita katika kuimarisha secta ya umma na kujeng amiundo mbinu ambayo ni msingi wa sustainable development.

Hate is fatal.

Naomba ndugu zangu tuwe na focus na nia nzuri. Hakuna mtu asiyejua, hata wenye CCM wanajua kwamba wanatembelea exceptionalism ya Rais Magufuli. Bila Magufuli hakuna ccm wala nini. Hatuwezi kukanyaga neema ambayo Mungu ametupa kupitia rais Magufuli eti tu kwa sababu tutaonekana tunaifia ccm. Vyama vya siasa vipo na vinabaki kama vilivyo lakini tusivifungamanishe sana na vipaji vya watu ambao wakihama wana hama navyo.

Kama asingekuwa raist Magufuli, mtu mwingine yeyote kutoka hiyo ccm tungeshafungwa minyororo shingoni tukikatiza bahari, na mengine mengi yaliyokuwa yanapaliliwa. Tena wapiga debe wasithubutu kumpigia kampeni Membe waije kutukumbusha machungu.


MAGUFULI OYEE!
 
hivi mnadhani mipaka ya nchi ni kama milango ya sebule na chumbani mkogombana mmoja analala sebuleni??
 
Umeandika kiuwepesi mno
Hivi unajua kuwa Kuna watanzania Wana nufaika kwa kufanya biashara na watu kutoka Kenya...
Na Kuna wakenya wananufaika na kufanya biashara na wakenya?
We unafikiri migogoro kama hii ikitokea viongozi wa nchi mbili hizo wao Wana dhurika!
Hapo kinachotakiwa ni diplomasia itumike kutatua tatizo na kama Kuna nchi moja kati yetu ndiyo inaonekana Ina matatizo Labda Kenya apewe makavu live, ili raia wajue

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Na wale waliooa na kuolewa Kenya wavunje ndoa zao?
 
Hatuendi hivyo bwana mdogo
 
Viongozi wengi wa kenya wana stress za korona musamehe bure watanzania ni watu waungwana toka zamani . nyie waacheni wafanye chochote mwisho wa siku watakuja na magoti kutaka maindi ya gizeri . hawana shamba kubwa ni huku gairo watakuja na tutawakamua .wecheni tu kelele zao sie tunyamaze tu.
 
Kwa hiyo wanapotupush kwenye kona tuwafanyeje? Hata vita na Idd Amini ilikuwa na madhara lakini "some times you got to fight when you are a man"
 
Kwa hiyo wanapotupush kwenye kona tuwafanyeje? Hata vita na Idd Amini ilikuwa na madhara lakini "some times you got to fight when you are a man"
Mgogoro wowote ule utatuzi wake unafanyika kwa hatua. Hatua za mwanzo ambazo huwa zinajaribu kulinda uhusiano na masilahi ya pande zote mbili ndizo ambazo hutangulia kupewa kipaumbele.

Ubabe hufuata baadae ikiwa mazungumzo ya mwanzo yameshindikana. Na hatua hii hufuatia baada ya kuangalia ni jinsi gani changamoto zitazotokana na ubabe huo zitatatuliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…