Kama hujawahi kufanya kazi serikalini,kaa kimya. We ulitaka watoke hadharani wakiri kuwa alikua amechanjwa?
Husikii kuwa hiyo ni kampeni ya nchi nzima so hiyo habari isitoke hewani?
Ulitaka wamchukue nani akanushe kuwa siyo madhara ya chanjo zaidi ya aliyehusika na tukio?
Pia ulitegemea muhusika akanushe ilihali keshakubali kuwa upande wa wanao chanjwa?
Na kampeni yoyote lazima iwe na wanaokubali na wanaokataa. Sioni sababu ya kumuadhibu au kumtukana asiyetaka chanjo.
Madhali ishakua ni hiari,waache watu waamua. Ila kama kuna ajenda ya siri nyuma ya chanjo,wakubali pia na matokeo yake.
Sent using
Jamii Forums mobile app