Serikali kuajiri Maafisa 800 wa TAKUKURU ili wakapambane na mafisadi

Serikali kuajiri Maafisa 800 wa TAKUKURU ili wakapambane na mafisadi

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
SERIKALI imesema kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), itaajiri maofisa 800 wenye taaluma mbalimbali kwa lengo la kwenda kudhibiti upotevu wa fedha za umma hasa miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alisema maofisa hao watasambazwa maeneo mbalimbali nchini ili kukabiliana na vitendo vya rushwa katika miradi ya serikali inayotekeleza.

“Ninakiri kuwa kuna upungufu na ubadhirifu katika miradi mingi inayotekelezwa ikiwamo ile ya kimkakati, hivyo serikali imeamua kuongeza nguvu ili kudhibiti ubadhirifu huo kwa kuongeza maofisa hawa watakaotawanywa wilaya zote,”alisema.

Chanzo: Nipashe

My Take
Vijana msipotoka awamu hii ya Samia mjue ndio basi watakuja watu dizaini ya Rais wa Wanyonge harafu mtaona mtakavyoishia kuwa machinga .
 
Vijana fursa hizo hapo.


My Take
Vijana msipotoka awamu hii ya Samia mjue ndio basi watakuja watu dizaini ya Rais wa Wanyonge harafu mtaona mtakavyoishia kuwa machinga .

Eti mkapambane na mafisadi, Thubutu 🤣🤣🤣🤣🤣!! Ufisadi kupambana nao Nchi hii labda uje utawala wa chama kingine na katiba iwe mpya!!
 
Back
Top Bottom