Serikali kuajiri Maafisa 800 wa TAKUKURU ili wakapambane na mafisadi

Serikali kuajiri Maafisa 800 wa TAKUKURU ili wakapambane na mafisadi

Jibu swali wewe huwezi kula Rushwa ukiona pesa?
Kwa hiyo wwe mradi tu ukiona pesa uko tayari kula Rushwa ili upindishe haki za watu!!?? Jaribu kuvumilia njaa yako usije ukaishia pabaya na kupenda kwako kula Rushwa!!
 
Huyu fisadi papa anaehamasisha ufisadi hapa nchini ataguswa kweli?!
 
SERIKALI imesema kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), itaajiri maofisa 800 wenye taaluma mbalimbali kwa lengo la kwenda kudhibiti upotevu wa fedha za umma hasa miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alisema maofisa hao watasambazwa maeneo mbalimbali nchini ili kukabiliana na vitendo vya rushwa katika miradi ya serikali inayotekeleza.

“Ninakiri kuwa kuna upungufu na ubadhirifu katika miradi mingi inayotekelezwa ikiwamo ile ya kimkakati, hivyo serikali imeamua kuongeza nguvu ili kudhibiti ubadhirifu huo kwa kuongeza maofisa hawa watakaotawanywa wilaya zote,”alisema.

Chanzo: Nipashe

My Take
Vijana msipotoka awamu hii ya Samia mjue ndio basi watakuja watu dizaini ya Rais wa Wanyonge harafu mtaona mtakavyoishia kuwa machinga .
Waliopo rushwa imewashinda hawa 800 ndiyo wataweza?
 
Hiyo ni taasisi ya kupanda na kupalilia rushwa haina maana kabisa kuwepo ni kupoteza hela za walipa kodi
Ni kweli bora wange waajiri Madaktari na walimu kuliko kuajiri watumishi hewa.
 
humu ndani ukisema waliowahi kutoa rushwa kwa takukuru aisee, ni wengi kuliko utakavyotarajia. anayepinga hili haijui takukuru.
 
SERIKALI imesema kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), itaajiri maofisa 800 wenye taaluma mbalimbali kwa lengo la kwenda kudhibiti upotevu wa fedha za umma hasa miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa...
Tanzania hakuna rushwa hao maafisa wanini?
 
Anaongeza wapigaji tu, rushwa haijanza jana wala juzi ipo na utaendelea kuwepo
 
Back
Top Bottom