Sasa Jiwe kaingiaje hapa!? Mwacheni Marehemu apumzike zake,Kesha maliza yake hapa Duniani,kazi imebaki kwetu na sisi kusubiri zamu zetu za Umauti kutufikia!!Huyo Mungu wako jiwe unayemwabudu pia alikuwa Mwizi. wewe mwenyewe mtu akikosea mwamala akatuma kwenye simu yako unakimbia haraka kwenda kuutoa na kwenda kwenye mataputapu.
ushamba wa hela sio mzuri kabisaTamaa, Apes nature hata yale Machipanzee huwa yanawazuia wenzao kula matunda pori mti mzima linahodhi limoja na kutoa kibano cha haja kwa yeyote atakae gusa mti.
hata Ya Barrick mlisema hivyo hivyo wataenda MIGA je yaliishia wapi?Ni vizuri kuheshimu sheria wakati wote. Ubabe huwa hausaidii siku zote,utasifiwa kwa muda na baadaye utaumia au utawaumiza watu wako.
Kumbuka ubabe wa Nyerere kwa yule mkulima mzungu, gharama zake zilimkuta Magufuli. Mara mbili ndege zetu zilikamatwa.
Hakujifunza tu!! Mambo ya kisheria hayamalizwi kwa ubabe hata kidogo.
Waseme tu pesa zinaenda kwa mstaafu fulani
Mungu atunusuru
Mbona hawakudai enzi za Magufuli? Pesa wanarudishiana kina msoga.
Watanzania ebu tuache ujinga! Tutajiwe kesi na mahakama iliyoamua Symbion walipwe kiasi hicho cha pesa!
Isije ikawa watu wanatengeneza tu mazingira ya kupewa pesa hizo bila kesi yoyote na kumsingizia Hayati Magufuli kwamba alivunja mkataba kinyemela.
Kwanza nyie mnaoshabikia mmejuaje mkataba ulivunjwa kinyemela bila kesi na hukumu ya Mahakama?!
Au ndo mnataka tuunganishe dots kwamba huu ulikuwa ni mkakati uliopangwa ndo maana akina Zitto Kabwe wamemshambulia Marehemu Hayati Magufuli mfululizo?!
Angekuwa shujaa saizi si angekuwa Ikulu? Tatizo hakuwa na akili ππππAma kweli ulegelege siutaki kwenye maisha yangu!!
JPM umenipa somo kubwa sana,
Ujasiri wako na uthubutu wako uliwogofya waizi wote wa ndani na nje ya nchi, hata wazungu waliufyata, ila sasa upepo unasomeka kirahisi, eti wezi waliokuwa wakituibia kwa mikataba ya kipumbavu na mezani kwa watia sain kumewekwa dollar za rushwa, na sasa tunawalipa tena waizi wetu!
Kwa nini hawakudai fidia enzi yako!!? Nimegundua, hata biblia imesema, waoga wote hawaustahili ufalume wa mbinguni, Bali wenye nguvu ndio watakaouteka
Na nchi yetu bila watu majasiri, maendeleo tutayasikia tuu!
Sasa tuchague nani? Chadomo? Acha utani ππHii nchi itachelewa sana kupata maendeleo ya kweli chini ya utawala wa ccm.
Bora ziende tuu kuliko zilivyokuwa kwa sukuma gang wala hazikutusaidia.Ipo siku tunaotukanana humu tutaimba wimbo mmoja! Wajukuu zetu watatu address kama akina Chief Mangungo.
Kama chama chao wenyewe walijimilikisha mali itakuwa rasilimali za umma? Hizi fedha zinazunguka alafu zinarudi kwa walewale waliohodhi na wanaoona hii nchi ni yao wenyewe!
Tuendelee kutafuta ugali, mambo mengine huwezi kupata jibu leo wala kesho. Endeleeni kutukanana hadi siku utapojua ulikuwa unajitukana mwenyewe.
Dawa ya deni ni kulipa,afu unakuta mama kakwama kwenye mambo yake Kisa upuuzi wa sukuma gang walipokuwa madarakani so kaamua ku clear messKwa hiyo awamu ya sita ndio ilivunja mkataba mnavolalamika hapa kuwa awamu ya sita haifai?
Kuna watu sijui mnwazia kupitia naniliu!
Mna chama chenu kinaitwa Umoja Party hamieni huko huko.Kwaheri Magufuli kwaheri uzalendo karibu ufisadi karibuni watumbuaji wa pesa
Sahauni kuhusu maendeleo katika nchi hi
Mwananch wa kawaida anaposikia habar kama hii n maumivu kias gani anayapitia
....MUDA WA MABADILIKO N SASA...
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Hili ndio swali huwa nawauliza watu watuambie hayo Maendeleo yaliyokuwepo ni yapi maana naona kufa kwake kumefungua maendeleo kuliko ilivyokuwa sasa watusaidie maana hata miradi hakuna hata mmja alikamilisha.Kipindi Cha jpm kulikuwa na maendeleo gani zaidi ya kuwafanya vijana machinga waliosoma na wasiosoma hakuna tofauti.
Moja ya swali zuri, yaani ukiangalia wapiga kelele huko nje si tuu wako disorganized na Wana migogoro isiyoisha zaidi ni wezi wanaopiga makelele kwa sababu wako Nje ndio maana walifoka bei na hawawezi kurudi..Suppose ni kweli CCM inabidi itolewe, ibadilishwe, tueleze ibadilishwe na nani?. Yaani kwa sasa hapa tulipo, tuitoe CCM, tumpe nani?.
Kukosekana kwa anye serious and credible opposition in Tanzania, ni afadhali CCM iendelee!. Kiukweli Watanzania tumshukuru sana Mungu for CCM, kuna watu wangechukua nchi hii...
Naomba nisimalizie!.
P
Na wewe jipange uchote au zamu yako ilikwisha?Ni wakati wa kuchota sasa
Huwezi kataza kampuni kutoa mgao,hiyo ni wenyewe ..Swali la msingi ni je kwani hawakutoa huduma ya umeme? Pili kwa nini ulikiuka mkataba uliosaini mwenyewe?hata kama tunasaidiwa kingi lakin sio bure ni mikopo lakini basi hata hichi kidogo tunachokusanya wenyewe angalau basi kitufae kutuletea maendeleo japo kiduchu kuliko kulipa hizo kampuni za kitapeli kisha hizo kampuni nazo wanatoa mgao wa 10% kwa hawa walafi wetu usidhani mikataba mibovu kama hiyo wakubwa wamesaini bure tu wana mgao wao wanapata kwenye malipo yoyote yatakayofanywa ndomana hawaoni tabu kuidhinisha pesa zitoke
Mbona iptl walidai na mlikataa kuwalipa huku riba ikizidi kukua?Mbona hawakudai enzi za Magufuli? Pesa wanarudishiana kina msoga.
Kwani hawakutoa huduma waliyokubaliana kwenye mkataba?Dah !!! haya mambo haya kufanya wafanye wengine lawama apewe mwingine !!!!
Walioleta Symbion kwa Mikataba ya Ajabu (Hakuna Lawama)!!!!
Waliokuwepo wakati inaonekana sio Kheri kuwalipa Symbion ? (Hakuna Lawama)
Yule ambaye ameshaondoka / amekufa hawezi kujitetea (Apewe lawama zote chini ya Jua ila mazuri yote tuchukue Sisi)
Kweli combination ya Unafiki na Kukosa Aibu ni Combination moja Hatari Sana....
Mbona sukuma gang walileta kampuni feki za kujenga Bwawa hamsemi,VP alilisema hili na akaongesea wanacvm ndio wanahujumu Bwawa..Ndio maana huyo januari makamba wahuni wenziwe wamemuweka hapo nishati ili waweze fanikisha ufisadi kuiba fedha ya umma. Utaona awamu ya jpm walikaa kimya hao symbion. Sasa hata mikakati ya bwawa la nyerere watahujumu ili kuleta wanyonyaji wa kimarekani ili walipwe ujira.