Serikali kujenga madarasa mapya manne katika kila shule ya Sekondari ya Serikali. Watoto wote 1M kuanza shule Januari 2022

Kwahio Hayo madarasa Manne una uhakika yatabeba wanafunzi wote kila kata Mkuu??...

Halaf Mkuu tukitoa hayo madarasa Mindombinu mingine Vip??Au unataka tu watoto waende shule halaf wamalize hawajui chochote??
Miondombinu gani hakuna mkuu wangu,

Hebu tuweni na shukrani wazee,

Mbona Mama anamaliza kila kitu kwa wakati yani,

#KAZI IENDELEE
 
Shule ya Sekondari ya kata ninayoishi hapa Jijini Mwanza inahitaji madarasa 54 kwa mujibu wa Taarifa ya Shule kwenye Kikao wa Wazazi. Sasa hivi shule ina madarasa 22. Yakiongezeka manne (04), yatakuwa 26. Bado 27! Si haba!
 
Mimi nimenukuu maneno ya Kaimu katibu mkuu,

Ila ni lini watoto wote wa form One walianza shule kwa wakati mmoja nchi nzima?

Kuna watu walianza shule mpaka mwezi wa nne,
Kuanza shule mapema kunatokana na mtoto kukamilishiwa mahitaji yote mapema na sio wingi wa madarasa.

Uchumi bado mbovu hadi leo na mambo hayo ya shule ni Mzigo mkubwa kwa wazazi na walezi walio wengi.

Mambo ni Magumu sana na familia nyingi Maskini wanafikia hata kufa Moyo na kutoamini kama Elimu itawakomboa siku moja
 
HHayo madarasa yatajengwa kwa miezi miwili? Maana bado miezi miwili kujngia mwaka mpya 2022.
Huku kwetu hakuna hataa dalili ya ujenzi wa darasa
Hata mwezi mmoja unatosha kukamilisha hayo majengo.
 
Mimi nimenukuu maneno ya Kaimu katibu mkuu,

Ila ni lini watoto wote wa form One walianza shule kwa wakati mmoja nchi nzima?

Kuna watu walianza shule mpaka mwezi wa nne,
Kwa hiyo mzee unaamini kuwa wanafunzi wote wataaanza kwa tarehe moja mwakani?

Naona matofari mengine yatatumika kama meza na viti kwa wanafunzi wapya.
 
Hawa ndio shida kabisa
 
Miondombinu gani hakuna mkuu wangu,

Hebu tuweni na shukrani wazee,

Mbona Mama anamaliza kila kitu kwa wakati yani,

#KAZI IENDELEE
Mkuu! Shule Tanzania hiii zenye miundombinu mizuri ni zile shule Maalumu tu utakuta kuna walimu wakutosha Vifaa vya kujifunzia kwa vitendo vya kutosha ila fuata hizo shule zingne walimu hawatoshi huko vijijini pia hakuna Vifaaa kwenye maabara yani ni majengo tu ya majengwa ya Kaandikwa LABORATORY.
 
Mbona kasema Vijifedha kapata mahali,

Sasa wewe unasemaje tena ni kodi yako,

Nadhani tuendelee Kumuunga mkono Rais anafanya makubwa sana,

Haya ni machache tu kati ya mengi
Sipingi kujengwa madarasa, napinga matumizi ya maneno, Rais Samia (au Magufuli enzi zile), napenda matumizi ya maneno yafuatayo.

Serikali ya Tanzania kujenga madarasa manne kila shule.

Zingatia tofauti ya Rais Samia na serikali ya Tanzania.
 
Majengo sawa ila kiti na meza ndo mtihani .kasha la i phone simu ndani Tecno Pop 2
 
Safi Sana hili la wanafunzi kuanza shule kwa pamoja lina manufaa sana kwa walimu na wanafunzi kitaaluma.

Kwa walimu linapunguza mzigo wa kazi ya kuanza kufundisha mada upya kwa wale wa chaguo la pili. Hivyo inampasa aidha atumie muda wa ziada (remedial time) ikiwemo zile siku zinazompasa kupumzika kisheria siku za wikiendi au aongeze masaa/muda wa kukaa kazini tena mara nyingi maofisa elimu hulazimisha bila malipo ya overtime.

Kwa wanafunzi wanaochelewa kuanza (second selection) mara nyingi huanza mwishoni mwa mwezi wa tatu au wa nne kabisa. Wao mara nyingi wanaathirika kitaaluma na kisaikolojia. Kitaaluma walimu wengi huwaharakisha au huwarukisha baadhi ya mada ndogo au mada kuu. Mara nyingi pia hukosa kozi ya Kiingereza (English Orientation Course) Kama wenzao wanaoanza kuripoti shuleni. Na hata kama wakipewa huwa si vile inavyotakiwa. Kisaikolojia wengi wanakuwa mitaani kwa muda mrefu kuanzia pale walipomaliza mitihani yao ya darsa la Saba mpaka kujiunga, hivyo morali ya kusoma hupungua. Wengi ndio wanaongoza kuacha shule (School drop out),kuwa na kesi za utoro,kupata mimba,mapenzi,nidhamu n.k

Kiuhalisia chaguo la pili huwa hawafanyi vizuri kitaaluma na ndio waachaji shule wazuri. Naipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuliona Hilo. Lisimamiwe vizuri kwa manufaa ya vijana wetu.
 
Mleta mada, mama ana kazi ya kujenga madarasa manne kila shule kwa miaka minne mfululizo. Acha niamini atafanya hivo. Kama hakuna massive dropouts maana yake madarasa hatatosha wakiingia form two.

Kwa kifupi, ukiongeza uwezo kwa form one - ni lazima uongeze angalau madarasa manne kila mwaka kwa miaka ya 2023, 2024 na 2025. Bila kufanya hivo wazazi wajiandae au kutakuwa na upungufu mwaka 2023!
 
vitu vidogo sana hivyo
Miak 70 ya uhuru kusifu ujenzi wa madarasa manne ni vitu vvidogovidogo
Ni vitu vidogo lakini kupunguza mzigo kwa wazazi ni jambo muhimu. Vijijini wananchi mara nyingi hulazimika kilipa kati ya tsh. 10,000-. 30,000 kwa kaya ili kuchangia ujenzi wa madarasa. Tena wengine kukamatiwa hadi mifugo ua kulazimisha kuleta kifusi Cha mchanga au kokoto wakishindwa kupata fedha.
 
Huyu raisi samia anafanya mambo makubwa sana!

Haijawahi kutokea katika historia ya nchi hii madarasa 4 katika kila shule ya sekondari kujengwa bila michango ya wananchi! Haijawahi kutokea.

Bahati mbaya,kuna wanaCCM masilahi wanajifanya hawaoni kazi hizi nzuri za mama. Wao kuponda tu.
 
Tatizo la mama wala siyo wapinzani. Wapinzani wanamuelewa sana mama Samia. Tatizo ni maccm masilahi ambao walikuwa wamezoea dhuluma kwa wananchi. Hawa wamekatiwa mirija ya dhuluma wamegeuka wapinzani wa serikali ya awamu ya sita.
 
Mimi nimenukuu maneno ya Kaimu katibu mkuu,

Ila ni lini watoto wote wa form One walianza shule kwa wakati mmoja nchi nzima?

Kuna watu walianza shule mpaka mwezi wa nne,
Nahisi wewe ndiye Samia mwenyewe maana kila siku ni kusifia kulikopitiliza kama wale waliokuwa wakumsifia dikteta Magufuli
 
BIG RUBBISH PRAISE AND WORSHIP
 
Hivi anajenga Nani hasa maana wabunge nao wanadai wanajenga wao ,katani nako madiwani hivyohivyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…