Serikali kurudisha tena Mswada wa Bima ya Afya kwa Wote tena bungeni kesho 01/11/2023

Serikali kurudisha tena Mswada wa Bima ya Afya kwa Wote tena bungeni kesho 01/11/2023

Yan we jamaa bana, umeusoma huo mswada ? Huo ni mswada wa mwaka jana August 2022
 
Wadau tupitie hapa muswada wa bima ya afya kwa wote unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni Jumatano tarahe 01 Novemba 2023
English version please maana kiswahili wengine ni shida kidogo kuoanisha na legal interpretation
 
Ni ndogo kwa wenye nacho, lkn % kubwa ya watanzania ni hohehahe.

Ndiyo maana serikali hiyo hiyo inayoona kuwa wananchi wanaweza kuchangia 120k kwa mwaka iliwaondolea ada ya shule za msingi na sekondari (sh 40,000 kwa mwaka). Na Sasa wamefuta mpk ada za vyuo vikuu.

Sasa kama wananchi walishindwa kulipa sh 40,000/ watawezaje 120,000??? Huoni hii ni contradiction????
Yan elewa, issue sio watu wanaweza kulipa au lah, issue ni practibility ya bima baada ya watu kulipa hio fedha, watu wakilipa hio pesa je mfuko wa bima ya Afya utaweza kusustain kwa muda gani? Au ndio utakuwa unategemea ruzuku za serikali kila mwaka ?
 
Serikali kupitia Wizara ya Afya inatarajia kurejea Bungeni tena hapo kesho Novemba 1 2023 na Muswada wa Bima ya Afya kwa wote ambao ulikwama mnamo Mwezi Februari 2023 kwa hoja iliyotolewa na Bunge ya kutokuwepo kwa chanzo endelevu cha fedha kutekeleza Mpango huo.
Bila kuturejeshea toto afya kadi huo muswada hauna maana.
Na hivyo vifurushi vilivyopangwa awali nadhani ilikuwa maalumu kwa familia za wanasiasa kama ilivyo kwenye fao la kujitoa walivyo litoa na wao kuacha kikokotoo kwa watu wengine ila wao haliwahusu.

Huu ubinafsi ilipaswa wananchi wote tuungane kupinga haya matabaka wanayoyaleta.
 
Kama wanalipia wenyewe ni sawa, ila isituingilie kwenye bajeti ya nchi saaana

Afya ya mtu ibaki kuwa jukumu la mtu binafsi zaidi. Serikali iweke mazingira wezeshi ya watu kujali afya zao wenyewe.

Mbona cost sharing ilikuwa inatosha. Maana isitokee mmoja akatozwa kodi kubwa kumlipia anayeendesha boda kasi. Au anayelewa pombe kali. Au, tena huyu ndo wa kuchapa kabisa..... anayepewa ugali nyama na mbogamboga kwa mamantilie halafu anakula anaziacha mboga za majani 🥴
 
Wangeweka laki moja kwa familia ya watu 5 zaidi ya hapo laki na nusu. Alafu wakaliweka ni jambo la lazima kwa mkuu wa familia kulipia hata ikiwezekana kidogo kidogo kwa mwezi elfu kumi.
Hapana kulazimishana, ibakie hiyari.

Ni kama kusema watu wote walipie luku tanesco hata walioamua kutumia sola zao tu.

Kuna watu afya sio kutibia magonjwa tu. Je nikitaka bima ininunulie matunda, inilipie gym itaweza? Sasa ya nini kulazimishana kuweka mipango ya magonjwa wakati ninataka afya.
 
Kama Wananchi hawaugui ugui Hovyo salio huwa kubwa na hivyo hutumiwa na Serikali kwa Shughuli nyingine za Maendeleo

Nasema ni kwa nchi ambazo raia wake Wana Afya njema

Mlale Unono 😀😀
 
Yan elewa, issue sio watu wanaweza kulipa au lah, issue ni practibility ya bima baada ya watu kulipa hio fedha, watu wakilipa hio pesa je mfuko wa bima ya Afya utaweza kusustain kwa muda gani? Au ndio utakuwa unategemea ruzuku za serikali kila mwaka ?
Hapa unaelezea udhaifu mwingine wa mpango huu wa huduma ya bima ya afya kwa wote.

Mchango wa sh 120k kwa mwaka kwa kila mnufaika ni mkubwa Sana na pesa itakayokusanywa ni nyingi mno. Lkn tatizo itakuwa ni ubadhirifu na ufujaji ndiyo utaufanya mfuko huu kushindwa kuhimili kutoa huduma kwa wote.

Kwasabb hata hii NHIF ambayo imekuwa ikichangiwa na wafanyakazi pekee imeyumbishwa na serikali ambayo ilichota bilioni 126 na ikazifuja.
 
Kama wanalipia wenyewe ni sawa, ila isituingilie kwenye bajeti ya nchi saaana

Afya ya mtu ibaki kuwa jukumu la mtu binafsi zaidi. Serikali iweke mazingira wezeshi ya watu kujali afya zao wenyewe.

Mbona cost sharing ilikuwa inatosha. Maana isitokee mmoja akatozwa kodi kubwa kumlipia anayeendesha boda kasi. Au anayelewa pombe kali. Au, tena huyu ndo wa kuchapa kabisa..... anayepewa ugali nyama na mbogamboga kwa mamantilie halafu anakula anaziacha mboga za majani [emoji3061]
Nakubaliana na ww swala la afya ni la mtu mmoja mmoja wasijejutongezea kodi ili kulipia mnywa pombe mmoja
 
Serikali kupitia Wizara ya Afya inatarajia kurejea Bungeni tena hapo kesho Novemba 1 2023 na Muswada wa Bima ya Afya kwa wote ambao ulikwama mnamo Mwezi Februari 2023 kwa hoja iliyotolewa na Bunge ya kutokuwepo kwa chanzo endelevu cha fedha kutekeleza Mpango huo.

View attachment 2798960
NIDA TU IMEWASHINDA BIMA KWA WOTE MNAWEZAJE NA SHARTI NINKILA WANACHAMA LAZIMA AWE NA JAPO NAMBA YA NIDA
 
Hapa unaelezea udhaifu mwingine wa mpango huu wa huduma ya bima ya afya kwa wote.

Mchango wa sh 120k kwa mwaka kwa kila mnufaika ni mkubwa Sana na pesa itakayokusanywa ni nyingi mno. Lkn tatizo itakuwa ni unadhirifu na ufujaji ndiyo utaufanya mfuko huu kushindwa kuhimili kutoa huduma kwa wote.

Kwasabb hata hii NHIF ambayo imekuwa ikichangiwa na wafanyakazi pekee imeyumbishwa na serikali ambayo ilichota bilioni 126 ikazifuja.
Soft government kuelekea 2024 na 2025
 
NIDA TU IMEWASHINDA BIMA KWA WOTE MNAWEZAJE NA SHARTI NINKILA WANACHAMA LAZIMA AWE NA JAPO NAMBA YA NIDA
Mkuu kwemye implementation ule mswada wa kwanza ulikuwa na lazma sana kwa sababu mtu asingeweza kusajili laini au kumiliki laini bila kuwa na Bima iliwakaba sana nahisi ndo maaan haukupita ngoja tuone wa kesho
 
Sawa mkuu karibu uchangie
Mtatuambia mlichoamua maana hamna uwezo wa kusukiliza wananchi. Na sisi wengine hatuna muda wa kusikiliza hilo bunge kibogoyo la majizi ya kura, kwani tunajua ni rubber stamp ya matakwa ya serekali.
 
Back
Top Bottom