Serikali kutumia Bil. 169/- kujenga VETA 60 nchi nzima

Serikali kutumia Bil. 169/- kujenga VETA 60 nchi nzima

Katika mwaka wa fedha 2022/23 Serikali ya Rais Samia Suluhu imewekeza Tsh 169bn/- kwenye ujenzi wa vyuo vya ufundi (VETA) 60 nchi nzima.
Ni wazonzuri sana, lakini hao vijana watajifunza technologies gani? Na wakimaliza watakuwa wame gain nini?
 
..kwa hiyo wasiboreshe viwango vya taaluma waongeze mavyuo tu sio?
Kwani huwa unajitawaza ndo ujisaidie?

Huwezi boresha kiwango bila vyuo, unaviborshea wapi? Unajenga vyuo ndo mengine yanafuata in process. Ajira, vifaa n.k
 
Kwani huwa unajitawaza ndo ujisaidie?

Huwezi boresha kiwango bila vyuo, unaviborshea wapi? Unajenga vyuo ndo mengine yanafuata in process. Ajira, vifaa n.k

..kabla hujajisaidia unatakiwa ujihakikishie kwamba kuna mazingira ya kutoka ukiwa msafi.

..lazima choo kiwe na karatasi za kujisafisha, maji safi, pamoja na sabuni.

..hivi unavyotaka twende ni sawa na mtu anayejisaidia kwanza, bila kujali hatua na mazingira niliyoyaeleza hapo.

..Mtu huyo anaweza hata kujisaidia kwenye suruali, na mambo ya kujiswafi ata-deal nayo baada ya hapo.

..Naendelea kusisitiza kwamba Veta zizingatie VIWANGO vya taaluma na mafunzo badala ya idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
..kabla hujajisaidia unatakiwa ujihakikishie kwamba kuna mazingira ya kutoka ukiwa msafi.

..lazima choo kiwe na karatasi za kujisafisha, maji safi, pamoja na sabuni.

..hivi unavyotaka twende ni sawa na mtu anayejisaidia kwanza, bila kujali hatua na mazingira niliyoyaeleza hapo.

..Mtu huyo anaweza hata kujisaidia kwenye suruali, na mambo ya kujiswafi ata-deal nayo baada ya hapo.

..Naendelea kusisitiza kwamba Veta zizingatie VIWANGO vya taaluma na mafunzo badala ya idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa.
Sawa. Ila na majengo yawepo pia.
 
Kati ya vitu vya maana serikali ya awamu ya sita imefanya ni hili la veta bola tupate ufundi tujiajiri maana kukaa kusubiri michongo sio kabisa nasikia vitakuepo vyuo vya veta kila wilaya hii ni neema kwa sisi wa mikoani
Tumechelewa Sana'a!!
 
Ni kweli tumechelewa sana. Lakini hata hivyo naomba kuuliza kama program ya mambo vijana watajifunza unaijua?
Nimesikia kwa watu, mimi mwenyewe sijafika huko, kuwa kwenye chuo cha VETA Chang'ombe wamekuwa equipt na CNC Lathe machines na CNC milling machines with CATCAM program, lakini hazitumiki, kwasababu hawana wataalaam wa kuzi operate hizo machines.

Sasa kama kuna mtu ana taarifa kamili kuhusu huu uzushi, ningeomba atujuze. Maana sisi wengine kidogo tulibahatika ku deal na hivyo vitu. Tungeweza kwa njia moja au nyingine tumia hiyo opportunity kuwajengea uwezo vijana wetu kujifunza skills za kutengeneza products mabali mbali na hizo machines na ambazo zingewafanya wajiamini kwenye manufacturings Industries duniani.

Tungeweza wafundisha vijana wetu sio tu jinsi ya ku operate hizo machines, bali hata technic na technologies nyingi za kutengeneza tools na jinsi ya kutafuta technical solutions katika challenges mbali mabali za kiufundi na vile vile kutambua surpleiers mbali mbali duniani ambao wanaweza agiza hizo tools kama lathe jaws, lathe cutting blades na kadhalika.

Nasikitika serikali yetu kwa kukosa washauri wazuri wenye utaalam wa material science kumshauri Rais kutambua umuhimu wa kuwa na mtambo wetu wa kuoka na kutengeneza aina mbali mbali ya chuma (steel).

Ingekuwa vizuri sana kusaidia amsha bongo ya vijana wetu watundu na wenye kuthubutu.

Kwenye hizi videos chini nnaweza jionea kazi zinazofanywa na CNC Lathe and Milling Machines.



 
Katika mwaka wa fedha 2022/23 Serikali ya Rais Samia Suluhu imewekeza Tsh 169bn/- kwenye ujenzi wa vyuo vya ufundi (VETA) 60 nchi nzima.
Habari hii ni nzuri sana kwa sisi watanzania. Hongera Rais Samia wa JMT
 
Saf sana wazo zuri tumuunge mkono mama Samia
 
WanaJamiiforum na watanzania wenzangu kwa ujumla kwenye #32 nimetoa coment yangu kuhusiana na hii mada inayoendelea ya Serikali kutumia Bil.169/- kujenga VETA 60 nchi nzima, lakini mpaka hivi sasa sijapata feed back yoyote kutoka kwenu. Inamaana hamjanielewa au ndiyo niseme bado tuko gizani kuhusiana na mambo haya ya kiufundi?

Nilitegemea kuwa vijana wa keo wanao penda maendeleo na waliaji wakuu wa ajira wangeweza toa maoni yao juu ya hiyo hoja.
Lakini kwa masikitiko makubwa naweza sema kuwa hii ni ishara ya kwamba vijana wengi wanashabikia tu mambo ambayo wanayasikia kuhusu serikali ikiyatekeleza, lakini kiukweli wake hawajui nini kinaendelea.

Na nimwonekano kwangu kuwa hata shughuli zinazo fanyika kwenye hivyo vyuo vya ufundi VETA wengi wetu tutakuwa hatujui au tuseme mafunzo yanayo tolewa huko ni ya low level, kiasi kwamba hata matokeo yake hatuyaoni kwenye jamii kiasi kwamba yakawasaidia vijana kwenye kutimiza malengo yao ya kujitegemea wenyewe kwa ajira na hata ujasiliamali.

Kwenye nchi za wenzetu zilizo endelea na kwenye nchi ambazo viwanda vya ufundi vimetamalaki mada kama hii na mchango kama huo nilio utoa wa mambo yanayo husu technic na technology, vijana wengi wangeonyesha interest na kuhoji, vile vile wataalam wengi kutoka viwandani, vyuo vya ufundi na hata vyuo vikuu wange participate kwa namna moja au nyingine kwenye kuuliza maswali au kutoa michango yao ya kuelezea chochote wanacho kielewa kuhusiana na mambo ya ufundi.

Kwa hali hiyo nawaomba watanzania mjijue au kujitathmini wenyewe jinsi gani upeo wenu wa kuelewa mambo muhimu yanayo husu maisha yenu unavyo zidi kuelekea shimoni. Yaani kwa maana nyingine ni kwamba mko mbali sana na uelewa wa mambo ya kiufundi katika manufacturing industries.

Hiyo kwangu ni picha halisi ya discussion zenu kwenye hii platform. Mmejikita sana kwenye mambo ya kisiasa na ushabiki wa kivyama na udaku zaidi kuliko uhalisia wa mambo muhimu yatakayo weza badili maisha yetu kwa ujumla.

Labda ni waulize swali, wakati mnapo zumgumzia maswala ya ajira mnamaanisha ajira zipi?
 
Nani kama Mama??
Ujuzi uwe wa kutatua matatizo yaliyo mengi kwenye jamii

Wafundishe na mahousegirl jmn😅
Hii ni major issue aisee
 
Back
Top Bottom