Serikali kutumia kigezo cha kujitolea kuajiri Walimu siyo haki

Mi
Mimi naona ni haki sema tu yaweza kua bahati maana Kuna mwalimu uenda alijitolea miaka 3 wakati fursa inatokea alikua kapumzika Basi inakula kwake.
 
Sasa mtu kafeli mtihani ataendeleaje na masomo?
Wananchi waliopo huko wanaishi vipi? Yaani wewe na kashahada kako ka ualimu ushajiona ni mtu maalumu Sana? Ili uende ualimu kwa vyovyote vile ulifeli. Sasa failure unaanzaje kuleta tambo na nyodo?
 
First appointment kwa kumbukumbu yangu unapangiwa popote.si lazima ulipojitolea.mfano wapo waliojitolea tanesko lindi na wakapangiwa tanesko mwanza baada ya kuajiriwa...wapo walionitolea halmashauri na manispaa mbali mbali na walipoajiriwa walipangiwa mikoa tofauti na ile waliojitolea.
Mwajiri anahitaji mtumishi ila si lazima yule aliekuwa anajitolea hapo.
Wapo waliojitolea taaisisi na kada mbali mbali km utendaji wa vijiji ,walimu,maendeleo ya jamii ,manesi kilimo mifugo nk na wakipopangiwa walipangiwa tofauti na pale.
 
Yaani kujitolea tu iwe kigezo cha kuajiri, tena kada muhumu ya ualimu? Devision zero zitazidi kuwa nyingi aisii. Yaani academic perfomance iwe second hand? Kisa mtu alijitolea?, je wajitolee graduate wote? Wataishije ili waweze kutimiza majukumu yao vizuri?
 
nawewe pia imagine kijana kajitolea shule x miaka(2) 2018-19 alafu akaacha kutokana na kushindwa kumudu gharama za maisha.

alafu kuna kijana kajitolea kuanzia mwezi uliopita tu lakini jina lake linaenda ila huyu wa miaka miwili anabaki .
busara haikutumika hapa
 
Bila shaka wanao unawafundisha mwenyewe na mkeo ambao hamkufeli (Kama unao lakini, maana maoni haya hayawezi kutoka kwa rijali)
Mm wanangu wapo nje. Hawawezi kufundishwa na failures. Nchi za watu ualimu wanaenda majiniaz tu na wanalipwa vizuri. Hapa failures wanaenda ualimu na mishahara yenu sawa na ya mabaa medi
 
Sehemu yoyote nafasi za kazi zikitoka huchukua kwanza volunteer wao waliojitolea then nafasi nyingine ndo hutoa kwa wengine baada ya volunteer wao kupata nafasi. Usikate tamaa tafta shule hata kijijini omba sehemu ya kulala huko ni rahisi kupata and no competition.
Never give up
 
Kujitolea au ku volunteer ni aina fulani ya cheap labour ambayo tusingeitegemea itokee miaka 60 baada ya kupata uhuru. Nalazimika kunukuu maneno ya marehemu Mzee Sita na Mzee Mwambulambo walipomwambia Mwalimu kuwa "ni heri wakati wa ukoloni"!
U volunteer uko duniani kote hata kwenye mashirika makubwa duniani watu walianza na u volunteer
 
Mimi nimekuelewa mtoa mada, hoja yake Ni rushwa kwenye huu mchakato, mchongo uko hivi, ili jina lako litumwe tamisemi, andaa laki 4 mpaka 6 kutegemeana na eneo ulipo, watu Nasikia wanatoa Sana, yaani unaanza na mkuu wa shule, afisa elimu kata, na wakaguzi na mkurugenzi, wote hawa mpaka wale kuepuka kutokukutambua, RUSHWA. Mimi naona nikawaida, ukitaka Cha uvunguni sharti uiname,. Tuliipenda wenyewe, chaguo letu wenyewe, acha tuisome namba maana hata Mimi kura yangu nilimchagua mheshimiwa
 
Wananchi waliopo huko wanaishi vipi? Yaani wewe na kashahada kako ka ualimu ushajiona ni mtu maalumu Sana? Ili uende ualimu kwa vyovyote vile ulifeli. Sasa failure unaanzaje kuleta tambo na nyodo?

nimelipenda jibu lako ingawa kiasi flani siyo zuri. Lakini nadhani umemjibu kulingana na yeye kujiona wa maana sana hawezi kuishi maneeo kama hayo wakati kuna watu wanaishi na kuendesha maisha yao.
 
Umelalama, lakini kwa muongozo nilionao ni kwamba kuna ajira watatangaza, kisha wajitoleao wana kipaumbele.
 
Wananchi waliopo huko wanaishi vipi? Yaani wewe na kashahada kako ka ualimu ushajiona ni mtu maalumu Sana? Ili uende ualimu kwa vyovyote vile ulifeli. Sasa failure unaanzaje kuleta tambo na nyodo?

Kosa walilofanya serikali yangu kwenye taaluma ya ualimu, [emoji29][emoji29] linatudharirisha mno.. haya bhana [emoji1487][emoji1487]
 
Walimu wa nchi hii kama wamelogwa hivi,pamoja na misoto wanayopitia bado hawaelewagi somo.

Huwa nashangaa sana mnavyopigia chapuo huu uongo, walimu ndo huamua nani awe kiongozi? Hii sio nchi ya kidemokrasia? Mnapotafuta mchawi, muanze kujitathmini ninyi wenyewe.
 
Acha mbwembwe bwana wewe.
Unajua mazingira ya kujitolea yakoje? Mtu anajitolea atakua anakula nini, atavaa nini na je mahitaji mengine atapata wapi?
Acheni usanii kama serikali haiwez kuajili iseme sio inakua na ujanja ujanja mwingi.
 
Pole sana maagizo kutoka juu yatakuwa yanabeba upuuzi humo chunguza uone
Imewahi kutokea huku niliko yaani mwanamke ana mme walikuwa wilaya moja baadae mwanamke kahamishwa kwenda wilaya nyingine na kadri siku zinavyosonga mwanamke anazidi kupewa ukuu na kuhamishwa kwenda mbali zaidi na mme wake yaani ilifika mahali mke akawekwa umbali wa kutumia masaa 7 kufika kwake kwa gari kutoka aliko mmewe .Kuja kuchunguza kumbe mke anachezewa na maafisa wa juu yaani jamaa anajua ni uhamisho wa kawaida kumbe kuna uchafu nyuma ya pazia.

So kuwa makini na pia kuwa na moyo wa subira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…