Serikali kutumia kigezo cha kupitia JKT ili kupata nafasi za kazi wakati si vijana wote huchaguliwa kujiunga na JKT ni ubaguzi wa wazi

Naunga mkono hoja
 
Afrika bado kuna ujinga mwingi Sana baada ya kupata uhuru miaka ya 1960s bado watu wanatumia sifa primitive kabisa za kupata ajira mfano sifa moja wapo ya askari wa kikoloni ilikuwa kutojua kusoma na kuandika Leo hii sifa ya kuwa police lazima uwe umefeli 4m 4 [emoji23]

60% ya viongozi waliopo serikalini Wana uwezo mdogo"Prof Assad
 
Uzalendo unafundishwa
Acha kukariri mkuu kwamba uzalendo unafundishwa.Mataifa ya ulaya hakuna habari za jkt kama huku kwetu lakini watu wanazipenda nchi zao kutoka mioyoni mwao na ufisadi aidha hakuna kabisa ama kwa asilimia chache.

Huku Africa ufisadi ni mkubwa sana na ndo tunaolazimisha watu wakajifunze uzalendo.Uzalendo upo moyoni mwa mtu sio
ufundishwa.
 
Wanafundishwa shule kuipenda nchi yao,historia yao,akina milambo wao,utamaduni wao,hawawi wazalendo from no where,hapo isike humjui,abushiri humjui,gen mayunga humjui,twalipo humjui
 
Wanafundishwa shule kuipenda nchi yao,historia yao,akina milambo wao,utamaduni wao,hawawi wazalendo from no where,hapo isike humjui,abushiri humjui,gen mayunga humjui,twalipo humjui
Mbona blaah blah nyingi mkuu.Jibu swali kama uzalendo unafundishwa mbona ufisadi hauishi tena watu wanaiba mchana kweupe.

Mbona hata sisi tunafundishwa kuhusu ukasiri wa kina Mkwawa,Isike,Mirambo nakadhalika lakini wizi na ufisadi haviishi.
 
Ndomana mkatakiwa muende,sababu mmepitia malezi ya kibwege Sana,mmelegea,Hamna nidhamu,Hamna uzalendo
Hivi watu wengine huwa mnaelewa mkilewa au? Mleta mada kasema Wazi si vijana wote wanaohtimu form 6 wanachaguliwa kwenda JKT. Kwa hiyo kutumia dhana hiyo kama kigezo muhimu ni ubaguzi, halafu wewe unakuja unasema nendeni JKT utafikiri kwenda huko Mtu anajipeleka.
 
Ila kiukweli, kama Nchi tunatatizo kubwa sana la watoa maamuzi. Kuna watu wamewekwa ktk nafasi mbalimbali za maamuzi, lakini ni zero kabisa. Sijui hili tatizo litakwisha lini...mie sijui.....
 
Mimi sikuchaguliwa jkt lakini nilijipeleka pale kanembwe wakanipokea Kwa mikono miwili Na posho nkawa Napokea kama kawaida....Ni uzembe wako kutoenda jkt wazi?
 
Una uhakika so vijana wote huenda jkt
 
Unaonea mkuu, kuna miaka hitaji la kwenda JKT liliondolewa tangu 1994,na hata waliporejesha, walioitwa walikuwa wachache sana, tusiwahukumu kwa njia hizo

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Kizazi chenye shida ni hiki ambacho miaka ya 2000 kilikua shule ya misingi,hawajitambui aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…