Serikali kuwapatia viwanja Polisi ili wasifedheheke wakistaafu

Serikali kuwapatia viwanja Polisi ili wasifedheheke wakistaafu

Kama mimi ni mzaliwa wa Babati na kituo changu cha kazi ni Mtwara. Kiwanja nikipatiwa Mtwara itakuaje niki staafu?
Kwani ukistaafu hutakiwi kuishi sehemu tofauti na uliyozaliwa
 
Hii nchi inashangaza sana yani limtu kama Muroto na majigambo yote yale linakua hata halina kibanda baada ya kustaafu loh, na kwa jinsi yalivyo na roho mbaya yanatakiwa yakistaafu yasipate hata wa kuyatembelea wale jeuri yao ,wanapokua kazini wanasahau kama na wao ni binadamu na watafika kipindi watarudi kwenye jamii
Cheque no zinawapumbaza sn wanakuwa wajinga
 
Majizi yanapendelewa. Polisi ndio wanaongoza kwa rushwa, kisha mahakama.
Ikumbukwe wana mshahara, posho, kazi maalumu na haramu kama rushwa na kubambikia watu kesi.
Bado yanapendelewa!
 
Polisi ni Watumishi wa UMMA kama Walivyo Watumisho Wengine kama Utaratibu ni kuwafanyia Wasiteseke Wakati wa Kustaafu hata hao Watumishi wengine nao Wapatuwe Viwanja kwani nao Watastaafu kwanini Kuwe na Upendeleo?
Wanawafanyia hivo ili wawe loyal( watiifu) kwa serikali na sio kwa raia. Ni kama wana wa bribe
 
Usenge kabisa,,polisi,gani wanafanya kazi nzuri na kazi gani,,taasisi,imejaa rushwa tu .

Watu na pesa ya posho, wana mshahara leo tena wanawazia viwanja, kwa hiyo hii nchi polisi tu ndiyo wanashida.

Usenge kabis HUU
Kwa sababu wameshika silaha
 
Sisi watumishi wengine hatufanyi kazi nzuri?
Au tuna mishahara mikubwa?
Kama wanataka kutukwamua watumishi njia pekee ni kukopesha direct na serikali bila riba. Hatuwezi kulikimbia deni.
 
Majizi yanapendelewa. Polisi ndio wanaongoza kwa rushwa, kisha mahakama.
Ikumbukwe wana mshahara, posho, kazi maalumu na haramu kama rushwa na kubambikia watu kesi.
Bado yanapendelewa!
Watu walioshika silaha mshahara wao haujawahi kushuka
 
Kuna siku jamaa kanikamata eti nimepita taa nyekundu pale salender, ki ukweli nilipita kijani na nilipofika kati ikawaka ya njano, jamaa akanipiga bao....eti nimepita nyekundu - alikuwa kabana mbele kule anavizia..... siku hiyo nilikuwa nimechoka saana, watoto wapo hoi maana tulikuwa tumetoka mkoani baada ya sikukuu.

Yule jamaa nikamwambia kama una uhakika niandikie lakini hiyo hela itakuwa ni laana kwako - akaniambia usinitishe bwana wewe huna lolote - nikamwambia sawa...akaandika faini.

Hadi leo laana sijaiondoa na najua imeshaandikwa tayari kwa imani yangu.

Baadhi ya hawa jamaa ndiyo ambao wanastaafu hawana hata vibanda vya kuishi - laaana kubambikizia watu kesi, rushwa nk.
 
Mbona sie machinga tunajikongoja na 150k per month tunanunua viwanja na kujenga hao wenye mishahara na bonasi na mikopo kibao wanashindwa kujenga ?
 
Hawa wasomi mambo yao nachoka.
Waongezeeni mishahara hivyo viwanja watanunua tu,na sio polisi peke yao watumishi wote
 
Kama mimi ni mzaliwa wa Babati na kituo changu cha kazi ni Mtwara. Kiwanja nikipatiwa Mtwara itakuaje niki staafu?
Utambulisho wa kazi yako utakusaidia kuombea kiwanja sehemu ulikozaliwa au unayohitaji
 
Back
Top Bottom