Serikali kuwapatia viwanja Polisi ili wasifedheheke wakistaafu

Serikali kuwapatia viwanja Polisi ili wasifedheheke wakistaafu

Kama mimi ni mzaliwa wa Babati na kituo changu cha kazi ni Mtwara. Kiwanja nikipatiwa Mtwara itakuaje niki staafu?
Unaweza patiwa hata mabwepande, na hutakiwi kuhoji ni vitu vya bure hivyo unakubali popote
 
Polisi ni Watumishi wa UMMA kama Walivyo Watumisho Wengine kama Utaratibu ni kuwafanyia Wasiteseke Wakati wa Kustaafu hata hao Watumishi wengine nao Wapatuwe Viwanja kwani nao Watastaafu kwanini Kuwe na Upendeleo?
Ni heri wangesema waongeze mishahara na benefits kwa watumishi wa umma ili hata wanapostaafu waweze kujisimamia
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene, amesema kuwa wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi watajadiliana na kuangalia namna nzuri ya kuweza kuwapatia viwanja askari polisi ili kuwaepusha na fedheha wale wanaostaafu na kujikuta hawana kiwanja wala nyumba.

SIMBAAAA.jpg

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene

Kauli hiyo ameitoa Bungeni Jijini Dodoma hii leo Juni 8, 2021, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Agnesta Lambert, lililohoji umuhimu wa serikali kuweka utaratibu wa askari polisi kusamehewa kodi ya vifaa vya ujenzi na kupewa viwanja kwa bei elekezi ili kuwaepusha na njia za udanganyifu kwa kigezo cha kwamba wanajiandaa na maisha baada ya kustaafu.

"Askari polisi wanafanya kazi nzuri kwa taifa lao na pengine wanafanya hivyo katika mazingira magumu na wengine kulingana na vyeo vyao ni ngumu kujikomboa na kupata hata maisha mazuri baada ya kumaliza utumishi wao, nataka niseme tutajadiliana na wenzetu wa Wizara ya Ardhi tuone uwezekano wa kuwapatia viwanja, wengine wanastaafu na umri mdogo halafu hana hata nyumba wala kiwanja, tutaangalia namna ya kuwapatia viwanja angalau wale wa vyeo fulani fulani," amejibu Mh. Simbachawene.
Fedheha kwa polisi ni malipo ya dhuruma wanazofanya wakati wakiwa makazini. Hata wapewe mbingu kama hawatatubu na kuacha dhambi za kubambikiza, kuonea na dhuruma nyingine hakika fedheha kwao itakuwa ni stahiki yao na ndo mshahara wa dhambi na haitokaa iwaishe.
 
Back
Top Bottom