Serikali kuweka siku ya jumamosi kuwa siku ya Usaili ni kuwakosea Haki Wahitimu waumini wa kisabato

Hapana mkuu sikumaanisha hivyo....

Hapana mkuu siungi mkono nchi kuongozwa kidini na kiimani.....

Hoja yangu ni kusikilizana na ile "inclucivity" tu....

Mbona sisi waislamu tuliiomba serikali ituruhusu watoto na dada zetu wawe na sare za hijabu(headscarves) na serikali ikatukubalia ilihali sare ya wanafunzi haikuwa na mwongozo wa kiimani ?!!
 
Tatizo lako ni moja kile unachoandika humu unakigongelea msumali kama sheria na lazima sio ombi. Akitokea mtu kukuchallange kidogo unatoka nje ya mstari na kujivalisha vazi la uvictim. Sabato njema

Suala la HAKI ni lazima na ndio maana utanitsfsiri hivyo.

Mimi nimeishauri serikali itende HAKI kwa hao Wasabato.

Mimi sio Victim ila ninaelezea mambo ya victims.

Ninachoshangaa ni wewe kama muwakilishi(nimekupa uwakilishi) wa wapingaji wa Haki za wengine(hapa ni Wasabato) wakati haikuumizi Wala kukuathiri popote. Hiyo inasababishwa na nini?

Ni Kama Ile Kesi ya Mahakama ya Kadhi Wakristo walivyoipinga Kipindi kile. Unajua Mpaka Leo najiuliza ni Roho gani hiyo
 

Alikuwa mshenzi
Mbinafsi.

Ndio walewale
 
Nadhani ni tabia mbaya tu inayofanywa na baadhi ya wanadini lakini si ukristo kwani dini haifundishi MAADILI MABOVU NA UMIMI WA KUKOSA SIMILE KWA WENGINE.....

Dunia inakwenda kasi mno ,wanadini wa dini nyingi duniani wanapoteza TRANQUILITY na HUMBLENESS ya dhati......
 

Kuna Mmoja anasema kumbe kuna Wasabato wanapondaga Dini zingine ndio maana analipa Kisasi hapa😂😂
 
Umimi hutokana na kukosa kujali , dharau na kudogosha wengine.....
 
Kuna Mmoja anasema kumbe kuna Wasabato wanapondaga Dini zingine ndio maana analipa Kisasi hapa😂😂
Ha ha ha hiyo ni "argumentum ad hominem...."

Ushabiki koko wa maandazi ya nazi kule Kilwa.....

Yaani msabato mmoja anaposimamia hoja yake basi iwe ni hoja ya wasabato wote ulimwenguni?!!

Chambilecho Mtibeli , uelewa nusu kijiko..."ha ha ha
 
UTIBELI unahusu upendo, kupenda wengine
HAKI
Kuwapa wengine Haki na kutetea HAKI yako.
UKWELI
Kuupenda ukweli na kuufanya
....haya ndiyo mapenzi ya Mwenyezi Mungu kutuumba na kutuweka hapa duniani....

Unaijengaje dunia kwa chuki ,ubaguzi na utetezi wa haki binafsi ?!!

#Do Not Do Harm !
#Altruism !!
 
Wewe sio serikali huwezi elewa nazungumzia Jambo gani
Kumbe Muda wote nilikuwa napoteza Muda kama ulikuwa unafikiri nasema ihairishe 😂😂😂

Kingereza kingi uelewa nusu kijiko
Umeishiwa hoja unaleta viroja.

Yani unachotaka wewe ni sawa na wanafunzi wa kiislamu waishinikize serikali kwamba Ijumaa wasiende shule kwa vile wanafunzi wenzao wa kikristo hawaendi shule jumapili.

Unataka haki kwa namna hiyo hapo.

Serikali haifanyi kazi kwa kuangalia imani za watu.

Imani zako za kidini usilete kwenye mambo ya kiserikali.
 
Serikali ndio yenye maamuzi na mamlaka.

Kila mtu akitaka serikali ifuate imani zake kwa kigezo cha haki. Hatuwezi fika mahali.

Hata mimi naweza nikatafuta kikundi changu cha watu kama yule Yesu wa Tongareni nchini Kenya, tukaunda imani yetu kisha tukaanza kuishinikiza serikali isikilize matakwa yetu.

Tunaweza tukaamua siku ya Jumanne ndio siku yetu ya ibada, Halafu serikali ikipanga ratiba zake Jumanne, Tuanze kulalamika kwamba ni uonevu hatutendewi haki.

Ndicho anachofanya huyu mleta mada.
 
Ni kweli serikali ndiyo yenye maamuzi na mamlaka....

Ni vipi serikali hiyohiyo ilitukubalia waislamu ombi letu la hijabu kwa wanafunzi na leo hii isitake kuwasikiliza wengine na hoja zao ?!!

Mkuu umeamua kujipa usemaji wa serikali ?!! Ha ha ha
 
Ha ha ha ha....
....uelewa nusu kijiko..
Mleta mada ndio mwelewa nusu kijiko.

Anataka serikali ifanye kazi kwa kuangalia imani za watu.

Serikali haifanyi kazi kwa kuangalia imani za watu.

Mambo ya kiserikali yakishapangwa yamepangwa.

Kama imani yako ni bora sana kuliko usaili, Nenda ibadani.

Maelfu ya watu hawawezi kuahirishiwa usaili wao eti kisa kuna kikundi cha watu wachache ni siku yao ya ibada.

Hakuna kitu kama hicho.
 
Ni kweli serikali ndiyo yenye maamuzi na mamlaka....

Ni vipi serikali hiyohiyo ilitukubalia waislamu ombi letu la hijabu kwa wanafunzi na leo hii isitake kuwasikiliza wengine na hoja zao ?!!

Mkuu umeamua kujipa usemaji wa serikali ?!! Ha ha ha
Lazima hilo ombi lako lifanyiwe tathmini kuangalia kama lina athari kwa wengine au halina.

Kuvaa hijabu hakuna athari yeyote kwa wengine.

Huo ni uhuru wenu wa kikatiba kuvaa chochote mkipendacho.

Lakini kuahirishwa kwa usaili eti kisa kuna kikundi cha watu fulani ni siku yao ya ibada, kutaathiri maelfu ya watu wengine ambao watahitaji kufanyiwa usaili siku hiyo hiyo.

Serikali haiwezi kuacha kufanya mambo yake kwa kigezo cha imani za watu.
 
Mkuu una points ila unatumia nguvu kubwa sana yenye msukumo wa kijazba hivi....

Well....mbona hoja yangu ya hijabu hujaidadavua?!!

Serikali yetu ni sikivu mno ,hebu ona hili...."birthday ya mtume Muhammad SAW" iko kalendani na mapumziko juu....hili jambo halikuwepo huko nyuma....na labda lingeingizwa miaka ya nyuma basi wako wengi wangejitokeza kulipinga kama upingavyo wewe....

Maana yake ni nini ?!!

Huko mbele tuendako basi hata hizo hoja za SDA zitachukuliwa kiutekelezaji.....ha ha ha

Usiku mwema mkuu wangu ,amina !!
 
Ni kweli kuvaa hijabu ni haki ya kikatiba kimavazi ila hiyo haki iko wapi ?!!

Haki hii ipo katika SARE za wanafunzi ?!!

Kwa hiyo hijabu zinazivaliwa na wanafunzi haziko katika kundi la SARE ?!!

Kama sivyo basi ni sare gani yenye taswira tofauti kwa "wanasare" wamoja ?!! Ha ha ha mbona haturuhusu hayo katika sare za MAJESHI yetu ?!!

Alamsiki binnuur!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…