Serikali kuweka siku ya jumamosi kuwa siku ya Usaili ni kuwakosea Haki Wahitimu waumini wa kisabato

Hawa Wasabato waliwahi kuwa deregisterd pale SAUT kipindi cha VC Father Dk. Kitima na DVCA (Sasa Baba Askofu) Dk. Bernidine Mfumbusa walipokataa kufanya mitihani yao ya UE siku ya Jumamosi!
Nakumbuka miaka kadhaa nyuma kuna wanafunzi wasabato wa Kilakala sekondari morogoro na wao waligoma kufanya masomo/mitihani/kazi za shule siku ya jumamosi wakaambiwa waombe radhi yaishe wakagoma wakasema wanaamini wako sahihi basi wakatimuliwa. Haikupita hata miezi 6 toka watimuliwe wakapata ufadhili wa kuendelea na masomo canada kupitia wasabato wenzao wa huko canada kwa kuwa wameilinda imani yao!. Mambo ya imani ni magumu sana wakati mwingine! ni si vitu vya kuiga!
 
Kutenga siku moja tu kwa ajili ya manufaa yako inaathiri nini dini yake
 
Mwongozo wao unawataka wakaswali mida wa swala lakini wengine wanakua kwenye majukumu wanashindwa. Wasabato punguzeni kujidekeza utadhani mbingu mmeandikiwa nyie tu kumbe hellen na kikundi chake ndo watunga sheria zote hizo
Ellen hakutunga Biblia Wala Quran
Sabato imetajwa kwenye Biblia na Quran
Huyo Ellen hata kujulikana atazaliwa hakujulikana.

Kwamba muislam azuiwe na shughuli au majukumu Mpaka ashindwe kuswali?
Huyo sio muislam unazungumzia mtu mwingine

Hatujidekezi ila tunaona Hatari ya baadhi ya wananchi kunyimwa Haki za msingi za Kupata Fursa za Ajira Kisa dini Yao.

Kwa nini isiwe siku za Kazi kama jumatatu, jumanne, jumatano au alhamisi?
 
Nakumbuka miaka kadhaa nyuma kuna wanafunzi wasabato wa Kilakala sekondari morogoro na wao waligoma kufanya masomo/mitihani/kazi za shule siku ya jumamosi wakaambiwa waombe radhi yaishe wakagoma wakasema wanaamini wako sahihi basi wakatimuliwa. Haikupita hata miezi 6 toka watimuliwe wakapata ufadhili wa kuendelea na masomo canada kupitia wasabato wenzao wa huko canada kwa kuwa wameilinda imani yao!. Mambo ya imani ni magumu sana wakati mwingine! ni si vitu vya kuiga!
Mungu anisamehe. Kama ningelikuwa na kampuni yangu binafsi na naweza kuajiri watu mmoja,wawili na kuendelea, siwezi kuajiri Msabato! Very stubborn!
 
Serikali kuweka siku ya jumamosi kuwa siku ya Usaili ni kuwakosea HAKI Wahitimu waumini wa kisabato.​

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Sabato Njema. (itikia Njema Sana).

Wahitimu wa kisabato wanasikitika baada ya baadhi Yao kukosa kwenda kwenye Usaili kutokana na siku iliyowekwa kwaajili ya Usaili ni siku ya ibada. Sikukuu ya Mungu wao wanaomuamini.

Ikumbukwe kuwa Sabato kwa waumini wa kisabato ni Moja ya amri kubwa na kuu wanaamini wameagizwa kuifuata na Mungu wao wakirejelea Torati ya Musa katika Biblia, katika Kutoka 20:8-11

Tunafahamu kuwa serikali huenda ilifanya kwa bahati mbaya kwa kusahaukundi hili la Wasabato. Na hatutaki kuamini kuwa imefanywa makusudi bila kujali au kwa kudharau Wasabato kwa Sababu zozote zile.

Wasabato sio Watu wakujihusisha na mambo ya siasa na kiserikali na hii huenda ni Moja ya sababu ya wao kusahaulika hata kwa mambo muhimu kama ya Ajira.

Mimi Kama Taikon Master, ambaye ni Msabato. Baada ya kupewa taarifa hiyo kwa kweli nilisikitika Sana. Nikaona kuinyamazia inaweza kujirudia na kuwafanya Wananchi wa Kitanzania, wanaoabudu katika dhehebu la Wasabato wanaweza kukosa Haki Yao kwa wakati Mwingine.

Serikali kupitia Wizara husika, ifuatilie Jambo hilo na kulifanyia marekebisho.

Taikon Acha nipumzike sasa.

Kesho tukutane, KANISA LA MWENGE SDA, DAR ES SALAAM.

SABATO NJEMA
Wagalatia mna deka sana
 
Kutenga siku moja tu kwa ajili ya manufaa yako inaathiri nini dini yake

Unajaribu kueleza nini?
Tunazungumzia Imani. Imani ipo ndani ya mtu. Dini ni Ramani ya Nje tuu.

Wewe kwa uelewa wako kama serikali haithamini Imani yako utaona inakuthamini?
 
Serikali kuweka siku ya jumamosi kuwa siku ya Usaili ni kuwakosea HAKI Wahitimu waumini wa kisabato.​

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Sabato Njema. (itikia Njema Sana).

Wahitimu wa kisabato wanasikitika baada ya baadhi Yao kukosa kwenda kwenye Usaili kutokana na siku iliyowekwa kwaajili ya Usaili ni siku ya ibada. Sikukuu ya Mungu wao wanaomuamini.

Ikumbukwe kuwa Sabato kwa waumini wa kisabato ni Moja ya amri kubwa na kuu wanaamini wameagizwa kuifuata na Mungu wao wakirejelea Torati ya Musa katika Biblia, katika Kutoka 20:8-11

Tunafahamu kuwa serikali huenda ilifanya kwa bahati mbaya kwa kusahaukundi hili la Wasabato. Na hatutaki kuamini kuwa imefanywa makusudi bila kujali au kwa kudharau Wasabato kwa Sababu zozote zile.

Wasabato sio Watu wakujihusisha na mambo ya siasa na kiserikali na hii huenda ni Moja ya sababu ya wao kusahaulika hata kwa mambo muhimu kama ya Ajira.

Mimi Kama Taikon Master, ambaye ni Msabato. Baada ya kupewa taarifa hiyo kwa kweli nilisikitika Sana. Nikaona kuinyamazia inaweza kujirudia na kuwafanya Wananchi wa Kitanzania, wanaoabudu katika dhehebu la Wasabato wanaweza kukosa Haki Yao kwa wakati Mwingine.

Serikali kupitia Wizara husika, ifuatilie Jambo hilo na kulifanyia marekebisho.

Taikon Acha nipumzike sasa.

Kesho tukutane, KANISA LA MWENGE SDA, DAR ES SALAAM.

SABATO NJEMA
Kweli kabisa, wasabato wote TUSIENDE KWENYE USAILI.

J. Mosi ni siku yetu ya ibada, HATUJI kwenye USAHILI.

Bora tukose Ajira tu..
 
Mungu anisamehe. Kama ningelikuwa na kampuni yangu binafsi na naweza kuajiri watu mmoja,wawili na kuendelea, siwezi kuajiri Msabato! Very stubborn!

😃😃😃

Fikiria muislam naye awaze kama wewe.
Mlutheri awaze kama wewe
Msabato awaze kama wewe.

Mnapofikiri mtumie AKILI

Unafikiri watu hawawezi kuishi bila kutegemea serikali au dini zingine?
Lakini ni Kwa sababu haina Tija.
Sheria zinawekwa ili kuwaleta watu pamoja wenye tofauti za kimtazamo, akili, nguvu, Itikadi, fedha n.k.
 
Hizo siku ulizotaja ni za ibada kwa imani zingine au ndo vile ushakariri dini ni mbili tu duniani.

Interview iwe scheduled ijumaa saa sita mpaka saa saba atapata wapi muda wa kwenda ibada. Kama wao wanaweza kuhairisha muda wa ibada na nyie igeni huko

Kila mtu akitaka kuvutia siku yake haitaleta maana na pia wengi wanapata mapumziko jumamosi kuliko siku zingine. Upeleke interviews jumatatu siku ngumu, usafiri mgumu ni mateso. Weekend tulivu purukushani zinakua chache, na wasimamizi wa interviews nao wana majukumu mengine nje ya hizo sahili
Ellen hakutunga Biblia Wala Quran
Sabato imetajwa kwenye Biblia na Quran
Huyo Ellen hata kujulikana atazaliwa hakujulikana.

Kwamba muislam azuiwe na shughuli au majukumu Mpaka ashindwe kuswali?
Huyo sio muislam unazungumzia mtu mwingine

Hatujidekezi ila tunaona Hatari ya baadhi ya wananchi kunyimwa Haki za msingi za Kupata Fursa za Ajira Kisa dini Yao.

Kwa nini isiwe siku za Kazi kama jumatatu, jumanne, jumatano au alhamisi?
 
Mwambie rafiki jambo.....

Mwambie sabato njema!

Tuu marafiki milele, kwa pendo lake Yesu

Mwambie rafiki jambo,

Mwambie sabato njema eeeeh tuma rafiki milele kwa pendo lake Yesu

mzabzab
 
Hizo siku ulizotaja ni za ibada kwa imani zingine au ndo vile ushakariri dini ni mbili tu duniani.

Interview iwe scheduled ijumaa saa sita mpaka saa saba atapata wapi muda wa kwenda ibada. Kama wao wanaweza kuhairisha muda wa ibada na nyie igeni huko

Kila mtu akitaka kuvutia siku yake haitaleta maana na pia wengi wanapata mapumziko jumamosi kuliko siku zingine. Upeleke interviews jumatatu siku ngumu, usafiri mgumu ni mateso. Weekend tulivu purukushani zinakua chache, na wasimamizi wa interviews nao wana majukumu mengine nje ya hizo sahili

Ukiambiwa ulete rejea utatoa?

Embu chukua Biblia au Quran, alafu urejelee maoni yako.

Wasabato na Wayahudi jumamosi au Sabato dini Yao inawakataza kufanya Kazi.

Ni dini gani nyingine inakataza Jambo hilo.

Waislam wao Sheria Zao zipo bayana.
Wapo humu watajieleza.

Wewe dini inayosali inakuambia siku unayosali usifanye Kazi yoyote?
Uje na rejea
 
Na bado ukifika muda wa makambi ruhusa ni lazima sio ombi. Shaaa anaondoka zake

Mbona siku ya Christmas au Maulid, au Idi, au pasaka ni holiday?

Makambi ni sikukuu kubwa kwa Wasabato.
Ni lazima kusherehekea sio Ombi.
IPO kwenye Biblia.
 
Back
Top Bottom