Serikali kuweni makini; inakuaje mtoto ana A ya math, B ya Chemistry, B ya biology na B ya Physics halafu mnampangia combination ya Art?

Kudoba wepo baaah

Senior Member
Joined
May 12, 2024
Posts
155
Reaction score
461
Mbaya zaidi dogo hakuomba combination yoyote ya arts katika maombi yake ya uchaguzi (selform)..... machaguo yOte matano ye ni PCM, PCB AU CBG.

Kijana amepambana kwenye shule yake ya kata hadi amefikia hapo ili ndoto zitimie halafu mnataka kumsumbua na kumuathiri kisaikolojia kama hivyo.

Najua kuna kubadilisha, lakini hilo ni mchakato na kwakuwa amepelekwa shule isiyo na hizo combinations maana yake itamlazimu kugharamika huyo katika kutafuta shule nyingine, kuna wakuu miungu watu; maringo, rushwa n.k.

Halafu kama machaguo ya mtoto, ambayo hufanyika kwa kuwahusisha walimu pamoja wazazi/walezi, hayazingatiwi kuna haja gani ya kujazishwa?

Inakera sana!

====

Pia soma:

TAMISEMI wafafanua kinachopelekea wanafunzi Kupangiwa Tahasusi (Combinations) tofauti na machaguo yao

Mwanafunzi wa Kidato cha 5 fanya haya ikiwa unataka kubadili tahasusi tofauti na uliyopangiwa
 
Binafsi nauona huu uzembe.
 
selection za mwaka huu ni selectuioin mbovu kuwahi kutokea tangu balaza liundwe
 
Hili ni tatizo la muda mrefu sana, even serikalini mtu ni mtaalam wa hiki anapewa ofise opposite kabisa na professional yake, matokeo waste of talents
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…