Serikali kuweni makini; inakuaje mtoto ana A ya math, B ya Chemistry, B ya biology na B ya Physics halafu mnampangia combination ya Art?

Serikali kuweni makini; inakuaje mtoto ana A ya math, B ya Chemistry, B ya biology na B ya Physics halafu mnampangia combination ya Art?

Mbaya zaidi dogo hakuomba combination yoyote ya arts katika maombi yake ya uchaguzi (selform)..... machaguo yOte matano ye ni PCM, PCB AU CBG.

Kijana amepambana kwenye shule yake ya kata hadi amefikia hapo ili ndoto zitimie halafu mnataka kumsumbua na kumuathiri kisaikolojia kama hivyo.

Najua kuna kubadilisha, lakini hilo ni mchakato na kwakuwa amepelekwa shule isiyo na hizo combinations maana yake itamlazimu kugharamika huyo katika kutafuta shule nyingine.........kuna wakuu miungu watu; maringo, rushwa n.k.

Halafu kama machaguo ya mtoto, ambayo hufanyika kwa kuwahusisha walimu pamoja wazazi/walezi, hayazingatiwi kuna haja gani ya kujazishwa?!!!!!!

Inakera sana!
Usivunjike moyo mpambanie kijana.
 
kama ni kweli, hayo ni makosa ya ajabu kabisa
Kuna uwezekano wanaopangia watoto hizo combination ni watu wa Arts;
Kwa kawaida mtu wa sayansi hawezi kufanya makosa ya waziwazi kama hayo!
 
Kumbe ndo inakoanzia ee?!!
Well limekuwa likifumbiwa macho na wahusika. Mfano mtoto kasoma science na kafaulu vizuri akifika chuo ghafla anapelekwa uhasibu, arts, sasa science alisoma ya nini?

Elimu yetu inatakiwa iwe structured kumuandaa kijana kubobea kwenye science au arts based ya combination alizosomea, hii itamjengea foundation nzuri.
Haya mambo ya kuchanganya na kuwaweka watu mahali ambapo hawajabobea ndio maana maofisin hawa perform vizuri
 
enzi zangu performers zilikuwa nzuri sana

A+ basic mathematics
A+ geography
A+ basic science
A+ English Britain language
A+ somo la kiswahili
A+ general history
 
Kama una moyo wakufuatilia nenda kwa Afisa elimu sehemu ulipo aandike barua akiambatanisha na matokeo yake sijui mengi zaidi ila kuna mtu aliambiwa hivyo ili afanyiwe mchakato.
 
Back
Top Bottom