Tetesi: Serikali mbioni kuchapisha noti mpya, kuna hatari ya kuelekea kwa Mugabe, harufu ya tenda za kifisadi zatawala

Kwel bado kinatumika a level, always literature reflects what is happening in our society
 
Magufuli ni rais wa hovyo kabisa na mikononi mwake hii nchi inaenda kutumbukia shimoni,acha wajjnga kama magonjwa mtambuka,jingalao,Barbarosa,mudawote na wengineo wamshangilie huyu Dikteta lakini ukweli itafika mahali kila mtu atalia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
uchumi alianza kuuharibu jk
huyu alikuwa na nafasi ya kuurekebisha,bahati mbaya badala awaachie wachumi yeye mchmi maganda korosho akawa ndio mshauri mkuu wa kiuchumi,tena majukwaani!!!!
 
Naomba day and night afanye haraka Ku print hizi note ili tuone hayo mapaka yatasemaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu huyu ni rais pumbavu kuwahi kutokea,wakiongea mbele ya camera watatekwa ,wataitwa wasaliti wasioitakia mema nchi,wanajua Dikteta hatari yupo ikulu,Magufuli hana tofauti na Idd Amin,tofauti zao ni kidogo mno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwan Tulipobadilisha Elfu Kumi ya Blue kuingia Elfu kumi nyekundu Uchumi ulidodora.

Hizo Ramli Chonganishi zimekaa kijuha-Juha
Mimi si Mchumi ila nitakusaidia hili kulingana na Wataalamu wa Uchumi wa Jf walivyojibu.

Suala lipo hivi, Rais anataka kuchapa noti hizi hizi zinazotumika sasa hivi kwa maana aziongezee ujazo ziwe nyingi kwenye mzunguko. Wataalamu wa Uchumi wanasema huko ni kudidimiza uchumi, kwa sababu uchumi unabidi ujiendeshe wenyewe. Kuongeza idadi ya noti kwenye mzunguko pesa zitakuwa nyingi ila hazitosadifu ule mzunguko unaotakikana yaani kama umeu' pump mzunguko.

Matokeo yake pesa zitakuwa nyingi kwenye mzunguko ila hazito akisi thamani halisi ya kitu, ili ziendane na thamani ya kitu wenye bidhaa wataongeza bei. Kitakachofuata kwenye manunuzi itaongezwa idadi ya noti ili kujaza lile gap la thamani halisi. Kwa hiyo, kama manunuzi ya kitu flani yalikuwa ni 10,000 ili iendane na thamani halisi ya mambo yalivyo, wata' pump nao bei. Kwaa mantiki hiyo, bidhaa ya namna hiyo inaweza uzwa 30,000 mpaka 40,000.

Kwa hiyo, thamani ya pesa imeshuka.
 
Wakuu nafikri wanaomshauri Rais wetu ama wanamuogopa au hawamwambii ukwel, ama vyote viwili...

Hebu tuanze na kudolola kwa uchumi(tuachane na takwim za kiuchumi ambazo huwa za kisiasa) ni kwel kunakuyumba kwa uchumi kwa kiwango kikubwa na hasa kutokana na sector binafsi kutokupewa kipaumbele..

Nitoe mfano mdogo tu, kipindi cha awam ya nne, serikal za mitaa,(halimashauri, miji na majiji) yalipewa mamlaka ya kukusanya fedha, yakitumia makampun binafsi au wenyewe, hii ilipelekea kuwepo kwa mzunguko wa moja kwa moja fedha kwa kuwa fedha zilipatikana na kuzisaidia haljmashauri..

Isitoshe wasaidizi wa halimashauri(makampuni) yaliajiri watu wengi na hvyo nao kupitia mfumo huo wakapata fedha....

Sasa basi mfumo huo ukaja ukaonekana unashida kubwa si kwenye ukusanyaji bali kwenye matumizi na usimamizi, hii ilipelekea serikali kuzizuia halimashauri kwa aina furani ya tenda kutokuzitangaza..

Bila kujari matokea, halimashairi zikanyang,anywa mapato na kupelekea kuyumba sana... Wakiwa bado wanatafakari ikaja kubwa kuliko yote kuwa sasa si ukusanyaji tu lkn pesa zote ziwe kwenye mfuko mmoja, ili kulinda zisiibiwe..

Hapo ndipo mdololo umekuwa mkubwa sana, sasa hebu jiulize jambo moja ni familia ngap zilikuwa zinapata pesa kwa kutegemea hayo makampun ambayo sasa hayafanyi kazi na taasisi za serikali,

Ok, tufanye kwamba tatzo limetatatuliwa, la wizi na udhibiti wa matumizi ya fedha, je ni kwel kwamba hyo ndyo ilikuwa njia sahihi?

Huenda tulitumia njia ya kuchoma msitu kwa kuwa kuna nyoka ameingia msituni, na kweli tukafanikiwa kumuuwa, je tumepoteza viumbe asili vingapi kwa sabab ya kuongia kwa nyoka msituni?

Hapo ndipo mm nafikiri washauri wa rais walipaswa kumwambia ukwel Rais, kuwa hoja si kuzuia mapato kukusanywa na serikali, hoja ni kuhakikisha tunatengeneza mfumo imara wa usimamizi na ukaguzi ili kuziba minya ya pesa....


Ikumbukwe kwa sasa kunaupungufu mkubwa wa pesa hasa kwa wananchi wa chini, ambae alitegemea auze maandazi, vitumbua, matunda, mitumba n.k

Hii inamaana ipi?
Tunakwenda kwenye kuimalisha nchi ya viwanda tukuwa na wananchi ambao hawako tayri kuingia kwenye huo uchumi, tujue tu kuwa kwa kuwa hatuna katiba Ambayo inamsingi mzuri siku akitokea Rais mwingine ambae si wa sasa.(baada ya miaka ya uchaguzi)atakuja na kuubadili kabisa mfumo uliopo sasa,

Kwa maana hyo tutakuwa tumechelewa kwa miaka 10, lakini pia itatulazim tuanza na muundo mwingine kwa miaka 10tena.. Matokeo yake tutakuwa tunasafri kwa hatua kumi tunarudi kwa hatua 7, halafu tena tunaanza hatua za kwenda mbele..


Jambo la msingi kwa sasa Rais ashauriwe vizr ya kwamba huku chini bado hapako vzr, nia yake ni njema kabisa(sina shaka nayo) ila ajitahidi kuimalisha sector binafsi



Mwiaho niseme hiki, uchumi wa nchi hautegemei mtu mmoja au taasisi, uchumi wa nchi unamtegemea kila mtu, wajibu wa serikal ni kuweka mazingira rafiki, si shindani ili kuwawezesha watu wake kufaidi na kuijenga nchi yao...

Kwa pamoja tutajenga

Mr Bonny...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…