Tetesi: Serikali mbioni kuchapisha noti mpya, kuna hatari ya kuelekea kwa Mugabe, harufu ya tenda za kifisadi zatawala

BAADA ya uchumi wa nchi kuyumba na maisha ya wananchi kuwa magumu, Rais John Magufuli anahaha kufyatua noti mpya.

SAUTI KUBWA inatambua kwamba tayari serikali imeshaanza mradi wa ufyatuaji wa noti hizo.

Hata hivyo, mradi huo umekwama kwa muda kwa sababu ya kugubikwa na sintofahamu kati ya rais na washauri wake; na miongoni mwa kampuni zilizoingia katika mchakato huo.

Kampuni za kimataifa ambazo zimetambulika kuingia katika mzozo huo ni De la Rue International, Oberthur Fiduciare, na M/s Crane Currency.

Vyanzo vinataja ufisadi katika mchakato kama sababu mojawapo iliyosababisha mzozo huo. SAUTI KUBWA inafuatilia habari za kina kuhusu mzozo huo.

Baadhi ya washauri wa serikali wanapinga ufyatuaji wa noti mpya wakidai utaongeza mfumuko wa bei, utashusha zaidi thamani ya shilingi ya Tanzania; na utafanya maisha ya wananchi yawe magumu zaidi.

Baadhi ya wachambuzi na wachumi waliozungumza na SAUTI KUBWA wanasema iwapo serikali itachapisha noti hizo nchi inaweza kukumbwa na mdororo wa kiuchumi kama uliokumba Zimbabwe katika utawala wa Robert Mugabe.

Mchambuzi mmoja amesema: “Itasababisha mfumuko wa bei za kila kitu kwa namna itakayoifanya shilingi yetu isiwe na thamani kabisa. Hiki ndicho alichokifanya Mugabe miaka ya nyuma baada ya kunyang’anya wazungu mashamba yao na vitega uchumi kutoka nje kukauka.

“Matokeo yake ni kwamba Zimdollar ilipoteza thamani hadi ikabidi ifutwe kabisa. Leo Zimbabwe haina sarafu yake yenyewe, na wananchi wanalazimika kutumia dola ya Marekani na rand ya Afrika Kusini kwa ajili ya manunuzi ya kila aina. Huko ndiko Magufuli anapotaka kupeleka Tanzania. Ataharibu kila kitu kilichobaki.”

Mchumi mmoja anayeheshimika nchini, ambaye SAUTI KUBWA haitataja jina lake, amezungumzia mfumuko wa bei na mzunguko wa fedha. Anasema:

“Mfumuko wa bei uko chini ya asilimia nne (4%). Si mbaya sana. Mzunguko wa hela ni kidogo. Hii ni mbaya. Kuchapisha hela ni uamuzi mbaya kiuchumi. Ujazo wa fedha katika uchumi lazima uendane na kiwango cha shughuli za uzalishaji katika uchumi. Kuchapisha hela ni njia ya ‘kiswahili’ ya kukabiliana na changamoto ya kiuchumi.”

Uamuzi wa Magufuli kuagiza ufyatuaji wa noti mpya, unaakisi kituko cha Idi Amini (dikteta wa Uganda 1971-1979) ambaye alipoelezwa juu ya upungufu wa fedha katika mzunguko, aliamuru benki kuu: “fyatua nyingi zaidi.”

Akijadili hali hii, mhadhiri wa uchumi anayeishi Marekani, anasema kwa kirefu:

Kwanza, tuanze na kujua sababu za lazima za kuchapa pesa. Hii ni kweli kuwa serikali haina fedha za kuendesha shughuli zake na kulipa madeni.

Pili, ni kwa nini serikali haina fedha? Kwa kawaida, ukiacha misaada, serikali ina vyanzo vikubwa viwili vya mapato: (1) Kodi, (2) kuuza dhamana au bonds.

Kwa hiyo, yawezekana ukusanyaji wa mapato ya kodi umepungua Ila serikali haisemi ukweli ili kijipatia sifa za kijinga.

Pia dhamana za serikali huenda haziuziki kama ilivyokuwa awali.

Mambo yote mawili, kupungua kwa mapato ya kodi na dhamana hutokea iwapo uchumi umesinyaa: hakuna uzalishaji wa kutosha kutokana na kudorora kwa uzalishaji kiuchumi.

Nini hufanyika? Serikali ingeweza kukopa zaidi. Huenda wakopeshaki hawapo tayari kwa kuwa kiwango cha uaminifu wa serikali kimeshuka. Utakupunga credit rating ya Tanzania imeshuka sana kwa sasa.

Pia, serikali ingeweza kubana zaidi matumizi yake. Lakini hili nalo Ni gumu sana kwa sasa kwa kuwa tayari imebana hadi ukomo wake. Kumbuka pia kubana matumizi ya serikali hupunguza ukuaji wa uchumi. Kudorora kwa sekta binafsi ni matokeo ya serikali kupana matumizi.

Nini matokeo ya kuchapa pesa? Uchapaji fedha huwa na madhara hasi kiuchumi iwapo uzalishaji haukui. Yaani, kutakuwa na fedha zaidi kwenye mzunguko zisizo na thamani. Matokeo yake ni mfumuko mkubwa wa bei. Kumbuka kilichotokea Zimbabwe kwa utawala wa Mugabe.

Mfumo wa bei usioendana na kipato halisi cha watu, utapunguza uwezo wa kutumia (purchasing power) na matumizi (consumption). Hapo uchumi utaendelea kuelekea shimoni zaidi.View attachment 853999View attachment 854386
Hapa hamna hoja, ni upotoshaji na uchochezi. Hamna madhara yeyote yanayotokana na kuprinti pesa. Isitoshe, kila nchi huwa ina printi pesa kwaajili ya matumizi ya ndani yanchi. Na wala hiki sio kilichotokea Zimbabwe.

Kuna utofauti wa kuprinti kwa maana ya kupelekea pesa nyingi kwenye uchumi, zaidi ya upatikanaji wa huduma na bidhaa sokoni. Printing ya namna hii ndio iliotokea Zimbabwe, na ndio hii ina madhara kiuchumi.

Printing ambayo imeongelewa hapo kwa barua wala sio ile yenye madhara, hii ni ile ya utengenezaji wa pesa, yaani kuzalisha kutoka kiwandani. Ambapo pesa hizi mara baada kutengenezwa sio lazima ziingizwe kwa mzunguko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania.
Hii nchi yetu sote mkuu sio ya chama chochote cha siasa.
Nchi ikiwa hovyo wote tunateseka na kama sio sisi basi kiazazi chetu kitateseka mbeleni.
Kwa bahati mbaya walala hoi ndio tutateseka zaidi.

kuanzia leo ieleweke kwamba "Tecno sio Simu"
Mlidhani matajiri wakishuswa mtapanda wapi,matajiri wana exposure wamevuka BODA wanaendelea kuingiza chapaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi si Mchumi ila nitakusaidia hili kulingana na Wataalamu wa Uchumi wa Jf walivyojibu.

Suala lipo hivi, Rais anataka kuchapa noti hizi hizi zinazotumika sasa hivi kwa maana aziongezee ujazo ziwe nyingi kwenye mzunguko. Wataalamu wa Uchumi wanasema huko ni kudidimiza uchumi, kwa sababu uchumi unabidi ujiendeshe wenyewe. Kuongeza idadi ya noti kwenye mzunguko pesa zitakuwa nyingi ila hazitosadifu ule mzunguko unaotakikana yaani kama umeu' pump mzunguko.

Matokeo yake pesa zitakuwa nyingi kwenye mzunguko ila hazito akisi thamani halisi ya kitu, ili ziendane na thamani ya kitu wenye bidhaa wataongeza bei. Kitakachofuata kwenye manunuzi itaongezwa idadi ya noti ili kujaza lile gap la thamani halisi. Kwa hiyo, kama manunuzi ya kitu flani yalikuwa ni 10,000 ili iendane na thamani halisi ya mambo yalivyo, wata' pump nao bei. Kwaa mantiki hiyo, bidhaa ya namna hiyo inaweza uzwa 30,000 mpaka 40,000.

Kwa hiyo, thamani ya pesa imeshuka.
Mkuu kwani notes zikishakuwa printed huwa zinaendelea kubaki idadi hiyo hiyo? Zinapoharibika au kuchakaa n.k huwa zinajitengeneza zenyewe? Wadau humu wamefanfanua vizuri kabisa kwamba yawezekana serikali inaprint notes mpya lakini za muonekano wa sasa ili kuziba pengo la zile notes zilizopotea, kuharibika au kuchakaa na kadhalika. Au inawezekana wanaprint notes mpya ili kuongeza ujazo wa notes kwa maana ya kuprint notes zaidi ili wazipump kwenye mzunguko wa fedha. Na mwisho inawezekana wanaprint notes zenye muonekano mpya kwa ajili ya kubadili tu sura ya notes zetu. Hizo zote ni options lakini usikomalie hiyo option moja tu kana kwamba wewe una uhakika 100% ya sababu za kuprint hizo notes za TZS.
 
Kuna tatizo moja ambalo tunashindwa hapa
Kuna wasomi wa uchumi ambao wapo wengi mpaka mawaziri wastaafu lakini wanashindwa hata kulizungumzia au kutoa rai mbele ya camera au kwa simu.

Wanaoongea nao wanaogopa kutajwa that's a shame

Bado tuko nyuma sana likifika suala la kuelezea mambo makubwa na ya msingi katika taifa.
Huku wenzetu waandishi wa habari watawatafuta wahusika au mpaka wastaafu na kuwauliza kuhusu chochote kinachotokea na huwezi kukuta hata mmoja anajibu eti mimi sio msemaji wa serikali

Watu wanajibu wanachoelewa na ni rai tu na uelewa wao kutokana na wanachokijua.

Hela zipo ila zinaelekezwa kwenye miradi mikubwa lakini mradi unaweza ukaenda polepole na huku hela zingine zinatumika kwa kulipa mishahara nk huku tukitafuta zingine kwa kuendeleza miradi

Kuchapisha hela sio suluhu ila kuzalisha zaidi na kupeleka bidhaa nje kwa wingi ndio sehemu nzuri ya kupambana
Kama livestock wanapelekwa kwa wingi nje ni kuongeza maradufu na tujifunze pia kusafirisha matunda yetu na mboga kwa wingi nchi za maghribi na middle East

Hilo tumefeli sana siwasifii Kenya ila wako vizuri kwa hili na May kilichompeleka huko ni mambo kama haya akifikiria brexit itakuwaje anaanza kujiandaa

Ifike mahali tuwe aggressive likifika suala la kujitanua kibiashara na tuache uswahili mwingi

Sent from my SM using Tapatalk
Nchi zao hazikomoi kuwasomesha no watu wao,bali uwatengenezea mazingira watu wao kusimama,sisi tunawawekea mikwamo watu wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumwache muheshimiwa sana raisi wetu Dr. Magufuli. Inawezekana anataka hela zichapishwe ili tulipe deni la Stanbic na ESCROW
 
Kuna vitu havikuwa na haraka wala tija Kwa sasa mfano kuhamia Dodoma, passport za kielectronic, marudio ya chaguzi, kununua ndege,vimekausha hela kweli, kweli ambapo hizo hela zingeingizwa kwenye kuwajengea wananchi uwezo wa kuzalisha zingesaidia sana uchumi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa hamna hoja, ni upotoshaji na uchochezi. Hamna madhara yeyote yanayotokana na kuprinti pesa. Isitoshe, kila nchi huwa ina printi pesa kwaajili ya matumizi ya ndani yanchi. Na wala hiki sio kilichotokea Zimbabwe.

Kuna utofauti wa kuprinti kwa maana ya kupelekea pesa nyingi kwenye uchumi, zaidi ya upatikanaji wa huduma na bidhaa sokoni. Printing ya namna hii ndio iliotokea Zimbabwe, na ndio hii ina madhara kiuchumi.

Printing ambayo imeongelewa hapo kwa barua wala sio ile yenye madhara, hii ni ile ya utengenezaji wa pesa, yaani kuzalisha kutoka kiwandani. Ambapo pesa hizi mara baada kutengenezwa sio lazima ziingizwe kwa mzunguko.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama kuna mtu hatakuelewa basi tena. Lakini hii ndio maana halisi ya hio barua, na huu utaratibu umekuwepo siku zote na ni majukumu halali ya BOT. Japo kila mtu ana uelewa wake, ila ulichoandika ndio maana halisi ya hio barua. Nimefuta hata nilichokuwa naandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukikopa sana Kwa ajili ya miradi kisha mda wa marejesho umefika kabla ya miradi kuanza kuleta faida itabidi utumie vyanzo vingine kulipia mikopo hio ili kuepuka kupanda Kwa riba.Na miradi isipolipa au kuchelewa kuanza kulipa hali itazidi kuwa ngumu zaidi na zaidi, kama alivotabiri Bushiri 2015.Siasa inapochukua nafasi ya utaalamu tutapata tabu sana.Mwanasiasa anachojali ni political will sifa za kisiasa bila kujali manufaa ya wengi.Tutembee kifua mbele.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa hiyo uzalishaji ukipanda maana yake hakuna ukuaji wa uchumi!!?..au umeamua kuharisha tu humu na chuki zako
 
Nchi zao hazikomoi kuwasomesha no watu wao,bali uwatengenezea mazingira watu wao kusimama,sisi tunawawekea mikwamo watu wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo ndio tatizo kwetu
Yaani mtu anaamua kupitisha kimagendo kahawa iende Uganda kwa sababu tu atapata kwa bei nzuri.

Hatujui strategy za biashara na hawataki kubadilika
Tutabaki hivi hivi wakati nchi nyingi zinatamani wangekuwa hata na ardhi kama yetu

Laiti ningejua kwa nini tuko hivi

Sent from my SM using Tapatalk
 
BAADA ya uchumi wa nchi kuyumba na maisha ya wananchi kuwa magumu, Rais John Magufuli anahaha kufyatua noti mpya.

SAUTI KUBWA inatambua kwamba tayari serikali imeshaanza mradi wa ufyatuaji wa noti hizo.

Hata hivyo, mradi huo umekwama kwa muda kwa sababu ya kugubikwa na sintofahamu kati ya rais na washauri wake; na miongoni mwa kampuni zilizoingia katika mchakato huo.

Kampuni za kimataifa ambazo zimetambulika kuingia katika mzozo huo ni De la Rue International, Oberthur Fiduciare, na M/s Crane Currency.

Vyanzo vinataja ufisadi katika mchakato kama sababu mojawapo iliyosababisha mzozo huo. SAUTI KUBWA inafuatilia habari za kina kuhusu mzozo huo.

Baadhi ya washauri wa serikali wanapinga ufyatuaji wa noti mpya wakidai utaongeza mfumuko wa bei, utashusha zaidi thamani ya shilingi ya Tanzania; na utafanya maisha ya wananchi yawe magumu zaidi.

Baadhi ya wachambuzi na wachumi waliozungumza na SAUTI KUBWA wanasema iwapo serikali itachapisha noti hizo nchi inaweza kukumbwa na mdororo wa kiuchumi kama uliokumba Zimbabwe katika utawala wa Robert Mugabe.

Mchambuzi mmoja amesema: “Itasababisha mfumuko wa bei za kila kitu kwa namna itakayoifanya shilingi yetu isiwe na thamani kabisa. Hiki ndicho alichokifanya Mugabe miaka ya nyuma baada ya kunyang’anya wazungu mashamba yao na vitega uchumi kutoka nje kukauka.

“Matokeo yake ni kwamba Zimdollar ilipoteza thamani hadi ikabidi ifutwe kabisa. Leo Zimbabwe haina sarafu yake yenyewe, na wananchi wanalazimika kutumia dola ya Marekani na rand ya Afrika Kusini kwa ajili ya manunuzi ya kila aina. Huko ndiko Magufuli anapotaka kupeleka Tanzania. Ataharibu kila kitu kilichobaki.”

Mchumi mmoja anayeheshimika nchini, ambaye SAUTI KUBWA haitataja jina lake, amezungumzia mfumuko wa bei na mzunguko wa fedha. Anasema:

“Mfumuko wa bei uko chini ya asilimia nne (4%). Si mbaya sana. Mzunguko wa hela ni kidogo. Hii ni mbaya. Kuchapisha hela ni uamuzi mbaya kiuchumi. Ujazo wa fedha katika uchumi lazima uendane na kiwango cha shughuli za uzalishaji katika uchumi. Kuchapisha hela ni njia ya ‘kiswahili’ ya kukabiliana na changamoto ya kiuchumi.”

Uamuzi wa Magufuli kuagiza ufyatuaji wa noti mpya, unaakisi kituko cha Idi Amini (dikteta wa Uganda 1971-1979) ambaye alipoelezwa juu ya upungufu wa fedha katika mzunguko, aliamuru benki kuu: “fyatua nyingi zaidi.”

Akijadili hali hii, mhadhiri wa uchumi anayeishi Marekani, anasema kwa kirefu:

Kwanza, tuanze na kujua sababu za lazima za kuchapa pesa. Hii ni kweli kuwa serikali haina fedha za kuendesha shughuli zake na kulipa madeni.

Pili, ni kwa nini serikali haina fedha? Kwa kawaida, ukiacha misaada, serikali ina vyanzo vikubwa viwili vya mapato: (1) Kodi, (2) kuuza dhamana au bonds.

Kwa hiyo, yawezekana ukusanyaji wa mapato ya kodi umepungua Ila serikali haisemi ukweli ili kijipatia sifa za kijinga.

Pia dhamana za serikali huenda haziuziki kama ilivyokuwa awali.

Mambo yote mawili, kupungua kwa mapato ya kodi na dhamana hutokea iwapo uchumi umesinyaa: hakuna uzalishaji wa kutosha kutokana na kudorora kwa uzalishaji kiuchumi.

Nini hufanyika? Serikali ingeweza kukopa zaidi. Huenda wakopeshaki hawapo tayari kwa kuwa kiwango cha uaminifu wa serikali kimeshuka. Utakupunga credit rating ya Tanzania imeshuka sana kwa sasa.

Pia, serikali ingeweza kubana zaidi matumizi yake. Lakini hili nalo Ni gumu sana kwa sasa kwa kuwa tayari imebana hadi ukomo wake. Kumbuka pia kubana matumizi ya serikali hupunguza ukuaji wa uchumi. Kudorora kwa sekta binafsi ni matokeo ya serikali kupana matumizi.

Nini matokeo ya kuchapa pesa? Uchapaji fedha huwa na madhara hasi kiuchumi iwapo uzalishaji haukui. Yaani, kutakuwa na fedha zaidi kwenye mzunguko zisizo na thamani. Matokeo yake ni mfumuko mkubwa wa bei. Kumbuka kilichotokea Zimbabwe kwa utawala wa Mugabe.

Mfumo wa bei usioendana na kipato halisi cha watu, utapunguza uwezo wa kutumia (purchasing power) na matumizi (consumption). Hapo uchumi utaendelea kuelekea shimoni zaidi.View attachment 853999View attachment 854386
Inawezekana pia kwasababu mfumuko wa bei uko chini serikali inataka kufuta noti ya 10000, 5000 na 2000 tubakiwe na noti ya buku tu au 2000

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyaraka za serikali zinavuja vuja tu kiholela. Na hakuna wa kuwajibishwa. Ni lini tumeona nyaraka za ndani za kenya na uganda?
 
Back
Top Bottom