Serikali: Mgonjwa wa Corona afariki dunia Mloganzila Hospital

Serikali: Mgonjwa wa Corona afariki dunia Mloganzila Hospital

Take personal responsibilities.
Corona IPO.
tapatalk_1585586453673.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania hospitali pekee yenye respiratory ventilators ni Muhimbili tu. Sina uhakika ni ngapi lakini **** mtu aliwahi kusema kuwa ni 4 tu. Sijui kama ni kweli. Lakini hospitali zetu nyingine, hazina.

Siyo kila ICU ina respiratory ventilators. Kama ulivyosema, mgonjwa ambaye mapafu yake yameshambuliwa kwa kiasi kikubwa na covid-19, bila ventilator machine, must go.

Na pia wataalam waku-operate hizi machine, hata tukipewa, naambiwa tunao wachache sana hapo Muhimbili. Kungine huko hawapo.
Mkuu so sad,bila hizo Ventilators ni tatizo kubwa,angalau tungekuwa na 15000 kwa kuanzia.
Nimemsikia Governor Andrew Cuomo wa New York akiomba kwa uchungu sana msaada ventilators 30000.
Siombi yatokee lakini dawa muhimu kwetu ni kinga ;ya kutosogeleana(Social distancing)kwa karibu,kunawa mikono mara kwa mara na kupunguza safari zisizo muhimu.kufunga mipaka yote ya nchi.
 
TANZIA
Familia ya Marehemu Alhaj Brigedia Generali Hashim Mbita kwa huzuni kubwa inasikitika kuarifu msiba wa mdogo wetu mpendwa IDDI HASHIM MBITA uliotokea usiku wa kuamkia leo hospitalini Mloganzila.
Kutokana na tatizo lililopelekea kifo chake, CORONA, serikali itamzika mpendwa wetu leo mchana. Wawakilishi wachache sana wa familia wataruhusiwa kuhudhuria mazishi. Hakutakuwa na msiba wala matanga ya pamoja kuepuka kueneza maambukizi. Kila mtu aomboleze kwake.
Dua nyingi tumuombee Iddi Allah amuweke pema peponi. Amina.
 
Waziri wa afya Ummy Mwalimu ametangaza kifo cha mgonjwa wa Corona kilichotokea leo asubuhi katika kituo cha Mlonganzila.

Anakuwa mgonjwa wa kwanza nchini kutangazwa kufa kwa ugonjwa huu.

"Nasikitika kutangaza Kifo cha Kwanza cha Mgonjwa wa COVID-19 hapa nchini Kilichotokea alfajiri ya Leo katika Kituo cha Matibabu ya wagonjwa wa COVID-19 kilichopo Mloganzila DSM. Marehemu ni Mtanzania Mwanaume Miaka 49 Alikuwa akisumbuliwa na Maradhi Mengine"
Waziri Ummy Mwalimu

RIP ndugu yetu, na Mungu awafariji wafiwa wote!
 
Mie nimeguswa na sehemu inayosema mgonjwa mmoja amepona. Najiuliza Mwana FA, Isabella ama meneja wa Diamond yupi alopona?

Wale waliomwambia Mwana FA assme ameugua Corona kisha aseme amepona walikusudia nini?

Waziri Ummy alionekana kumpongeza na kumsifu Mwana FA, alijua anachokifanya?

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kubisha mkuu kisarawe haianzii pale, ilipo hospital ni jimbo la kibamba ambapo mbunge ni mnyika
ingia kwenye map zone ya DSM mkuu utaona mipaka,sibishi ila ndio uhalisia ulivyo...
 
Back
Top Bottom