Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo taarifa hii inaidhinisha kifo chake (kwa sababu alikuwa na maradhi mengine) Ina maana asingekuwa na maradhi mengine basi Corona isingetoa uhai wake?.....Kumbe alikuwa anasumbuliwa na maradhi mengine..........kabla ya COVID-19.
Jamaa kazikwa na jeshi hakuna ndugu kusogea karibu
Mmmghhhh kweli ibilisi wa mtu ni MTU. Wapi nimekejeli? Yeye ndio alianzisha Uzi hapa au ni kujipendekeza tu???Inaelekea unakejeli juhudi za Rais na serikali katika mapambano dhidi ya Corona
hatariHuyu jamaa inasemekana alikua fine hadi ijumaa na ni mtu wa watu kwa maana kwamba ni mtu wa kukutana na watu.
Baada ya kuanza kujisikia vibaya akalazwa na jumamosi akapelekwa ICU maana yake vitu vilisha anza kufeli.
Leo jumanne kaaga ina maana jamaa alikua na corona wiki nzima pengine iliyo pita.
Naogopa hadi kutoka nje.. corona dar ipo.
Sent using Jamii Forums mobile app
So pamoja na campaign ya Stay at Home bado aliendelea kukutana na watu?Huyu jamaa inasemekana alikua fine hadi ijumaa na ni mtu wa watu kwa maana kwamba ni mtu wa kukutana na watu.
Baada ya kuanza kujisikia vibaya akalazwa na jumamosi akapelekwa ICU maana yake vitu vilisha anza kufeli.
Leo jumanne kaaga ina maana jamaa alikua na corona wiki nzima pengine iliyo pita.
Naogopa hadi kutoka nje.. corona dar ipo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa ukiulizwa kwanini kafa na wengine wamepona corona?ndio tunarudi kulekule kwenye maradhi mengine.Endeleeni kukebehi tu lakini hatujui ya kesho. Marehemu alikuwa na asili ya pumu na siyo kama alikuwa kwenye hali mbaya kabla ya kuugua. Alilazwa hospital ya Agha khan na watu wengi walikuwa wanamtembelea hospitalini kabla hajahamishwa.
Ni hivi afsa: Ugonjwa wa corona unaweza kumuua mtu yeyote hata yule mwenye afya kabisa. UK kulingana na data za leo kuna watu 28 wamefariki ambao hawakuwa na ugonjwa mwingine wowote. Yaani walikuwa wazima kabisa. Japokuwa kwa wenye magonjwa mengine na wazee ni rahisi zaidi kuathirika au kufariki lakini hata wazima kabisa wapo wanaofariki. Italia wamefariki madaktari 60 mpaka sasa hivi. Unataka kuniambia hawa madaktari wote walikuwa na magonjwa mengine?Sasa ukiulizwa kwanini kafa na wengine wamepona corona?ndio tunarudi kulekule kwenye maradhi mengine.
Daaaaah, mi najua sasa ndugu, mambo ni moto🙏🙏🙏🙏🙏
Mkuu iko DarPwani
Hapo wameacha utata mkubwa sana.
Mkuu tunaona watu wanavyokufa huko ulaya kutokana na corona,hivyo sioni haja ya kufichaficha mambo ikitokea watu kuhoji kuhusiana na hivyo vifo vya corona kwa kupata uelewa zaidi.Ushauri wangu kwa wizara ya Afya: kusema mgonjwa alikuwa na magonjwa mengine ni kupunguza makali ya corona na wananchi watadhani corona yenyewe haiwezi kuua. Zingatieni tafadhali.