Serikali: Mgonjwa wa Corona afariki dunia Mloganzila Hospital

".........ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine." Sentensi kama hizi zina ujumbe wa aina fulani ktk ubaya wa corona.
 
nimeona hiyo habari clouds tv kipndi cha 360, wanasema alikuwa na umri wa miaka 49.
duuh! hii habari imenipa hofu sana
Mlishaambiwa msali pia muendelee na shughuli za kujenga taifa maogopa nini
 


Hizi taarifa nusu nusu zinatia wasi wasi sana - watu wangapi aliwahi kukutana nao majuma mawili kabla, wangapi walimtembelea alipo lazwa Agha Khan, nyumbani kwake alikuwa anaishi na watu wangapi?

Kwa nini Wizara haianzishi kipindi cha TV na Radio kinacho wasihi watu wote walio wahi kukutana na victim socially au mazingira mengine, wajitokeze ili wapimwe kwa manufaa yao wenyewe na Watanzania wenzao kwa jumla - mbinu hizi nilikuwa naziona kwa wenzetu wa magharibi, kila wiki wanaendesha kipindi maalum kwenye TV kinacho julikana kama "Crime watch" kipindi hiki usaidia sana Polisi kukamata criminals walio shindikana - Polisi ufanya zoezi hilo kupitia kwa waigizaji ambao upewa majukumu ya kuigiza matukio ya kiharifu ili kufanya watazamaji wa TV wakumbuke kama waliwahi kuona tukio kama hilo la kiharifu lakini hawakuliwekea maanani, hivyo Polisi uwakumbusha watazamaji kwamba kama kuna mtu au watu walio wahi kuona tukio kama hilo, basi wafike kituo cha Polisi kutoa ufafanuzi wa tukio - mbinu hizo zimesaidia sana ku-solve crimes ambazo hapo mwanzo zilikosa ushahidi wa kutosha. Sasa kwa nini napendekeza mbinu hizo zitumike hapa kwetu? Jibu ni kwamba Wizara ya afya ikitekeleza mbinu hizo zitaiwezasha kubaini watu wote walio wahi kukutana/tembelea victim wa ugonjwa unao tokana na coronavirus - watu watajitokeza tu mradi Wizara iwe wazi kutaja jina na kuweka picha ya victim ili watu wakumbuke ni wapi walikutana nao na kwa muda gani? - hapa na maanisha victim walio ambukizwa virusi humu humu nchini bila ya kutoka nje ya nchi, tusipo fatilia kwa karibu nyenendo za watu kama hao, basi maambukizi yanaweza kuongezeka kwa kiwango cha kutisha.
 
Huu nao Sasa uzembe kwa marehemu, Yaani miaka 49 alishindwa kumalizia mmoja TU afe akiwa na Miaka 50.

Lakini Sawa
"HAKUNA KABURI LA MJINGA".
 
jibu ni. Ambulance huwa haipati ajari hovyo hovyo.
 
Hili siyo suala langu peke yangu.
Hakuna mwenye lake katika suala la corona. Corona Hana dini,hana chama, hana tajiri hana masikini, hana Daktari hana mgonjwa.

Ulikatazwa kufanya hizo hatua stahiki?

"Inna li Llahi wa Inna Ilayhi Rajiun" ni Aya ya Qur'an. Tunaisoma Qur'an kutwa mara tano kwa uchache leo miaka zaidi ya 1400 hatujachoka na hatutachoka daima. Soma...

الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ - 2:156

Who, when disaster strikes them, say, "Indeed we belong to Allah, and indeed to Him we will returnable."
 
Bongo raha sana watu badala ya kuchukua tahadhari kila mtu anamlilia marehemu.. Nilipoona steve nyerere analia mara rafiki mara kaka umeenda mapema nikaona kabisa kuna upigaji wa rambi rambi
 
Yani nasoma kama naongea
 
Idd Mbita nakuombea heri upumzike kwa Amani upate raha na pumziko lisilo na Mawaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…