Serikali: Mgonjwa wa Corona afariki dunia Mloganzila Hospital

Serikali: Mgonjwa wa Corona afariki dunia Mloganzila Hospital

Waziri wa afya Ummy Mwalimu ametangaza kifo cha mgonjwa wa Corona kilichotokea leo asubuhi katika kituo cha Mlonganzila.

Anakuwa mgonjwa wa kwanza nchini kutangazwa kufa kwa ugonjwa huu.

"Nasikitika kutangaza Kifo cha Kwanza cha Mgonjwa wa COVID-19 hapa nchini Kilichotokea alfajiri ya Leo katika Kituo cha Matibabu ya wagonjwa wa COVID-19 kilichopo Mloganzila DSM. Marehemu ni Mtanzania Mwanaume Miaka 49 Alikuwa akisumbuliwa na Maradhi Mengine"
Waziri Ummy Mwalimu

".........ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine." Sentensi kama hizi zina ujumbe wa aina fulani ktk ubaya wa corona.
 
nimeona hiyo habari clouds tv kipndi cha 360, wanasema alikuwa na umri wa miaka 49.
duuh! hii habari imenipa hofu sana
Mlishaambiwa msali pia muendelee na shughuli za kujenga taifa maogopa nini
 
Huyu jamaa inasemekana alikua fine hadi ijumaa na ni mtu wa watu kwa maana kwamba ni mtu wa kukutana na watu.


Baada ya kuanza kujisikia vibaya akalazwa na jumamosi akapelekwa ICU maana yake vitu vilisha anza kufeli.


Leo jumanne kaaga ina maana jamaa alikua na corona wiki nzima pengine iliyo pita.

Naogopa hadi kutoka nje.. corona dar ipo.

Sent using Jamii Forums mobile app


Hizi taarifa nusu nusu zinatia wasi wasi sana - watu wangapi aliwahi kukutana nao majuma mawili kabla, wangapi walimtembelea alipo lazwa Agha Khan, nyumbani kwake alikuwa anaishi na watu wangapi?

Kwa nini Wizara haianzishi kipindi cha TV na Radio kinacho wasihi watu wote walio wahi kukutana na victim socially au mazingira mengine, wajitokeze ili wapimwe kwa manufaa yao wenyewe na Watanzania wenzao kwa jumla - mbinu hizi nilikuwa naziona kwa wenzetu wa magharibi, kila wiki wanaendesha kipindi maalum kwenye TV kinacho julikana kama "Crime watch" kipindi hiki usaidia sana Polisi kukamata criminals walio shindikana - Polisi ufanya zoezi hilo kupitia kwa waigizaji ambao upewa majukumu ya kuigiza matukio ya kiharifu ili kufanya watazamaji wa TV wakumbuke kama waliwahi kuona tukio kama hilo la kiharifu lakini hawakuliwekea maanani, hivyo Polisi uwakumbusha watazamaji kwamba kama kuna mtu au watu walio wahi kuona tukio kama hilo, basi wafike kituo cha Polisi kutoa ufafanuzi wa tukio - mbinu hizo zimesaidia sana ku-solve crimes ambazo hapo mwanzo zilikosa ushahidi wa kutosha. Sasa kwa nini napendekeza mbinu hizo zitumike hapa kwetu? Jibu ni kwamba Wizara ya afya ikitekeleza mbinu hizo zitaiwezasha kubaini watu wote walio wahi kukutana/tembelea victim wa ugonjwa unao tokana na coronavirus - watu watajitokeza tu mradi Wizara iwe wazi kutaja jina na kuweka picha ya victim ili watu wakumbuke ni wapi walikutana nao na kwa muda gani? - hapa na maanisha victim walio ambukizwa virusi humu humu nchini bila ya kutoka nje ya nchi, tusipo fatilia kwa karibu nyenendo za watu kama hao, basi maambukizi yanaweza kuongezeka kwa kiwango cha kutisha.
 
Huu nao Sasa uzembe kwa marehemu, Yaani miaka 49 alishindwa kumalizia mmoja TU afe akiwa na Miaka 50.

Lakini Sawa
"HAKUNA KABURI LA MJINGA".
 
Kwani ukiwa unawahisha mgonjwa wa malaria hospitali katika ambulance, halafu hiyo ambulance ikapata ajali mgonjwa akafa utasema kafa kwa sababu gani?
a. Kafa kwa malaria kwa sababu bila malaria asingekimbizwa hospitali kwa ambulance hiyo aliyopatia ajali
b. Kafa kwa ajali kwa sababu bila hiyo ajali angeweza kufika hospitali akapona
c. Kafa kwa uzembe wa dereva wa ambulance kwa sababu hiyo ambulance ingeendeshwa na dereva mwingine angefika hospitali salama
d. Kafa kwa uzembe wake mwenyewe kwa sababu angewahi kwenda hospitali kabla hajazidiwa asingehitaji kukimbizwa hospitali kwa ambulance ya dharura

Jibu ni ....................
jibu ni. Ambulance huwa haipati ajari hovyo hovyo.
 
Hili siyo suala langu peke yangu.
Hakuna mwenye lake katika suala la corona. Corona Hana dini,hana chama, hana tajiri hana masikini, hana Daktari hana mgonjwa.

Ulikatazwa kufanya hizo hatua stahiki?

"Inna li Llahi wa Inna Ilayhi Rajiun" ni Aya ya Qur'an. Tunaisoma Qur'an kutwa mara tano kwa uchache leo miaka zaidi ya 1400 hatujachoka na hatutachoka daima. Soma...

الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ - 2:156

Who, when disaster strikes them, say, "Indeed we belong to Allah, and indeed to Him we will returnable."
 
Bongo raha sana watu badala ya kuchukua tahadhari kila mtu anamlilia marehemu.. Nilipoona steve nyerere analia mara rafiki mara kaka umeenda mapema nikaona kabisa kuna upigaji wa rambi rambi
 
Kiukweli najiuliza Sana Juu Ya watu wanaohangaika na idadi ya walioambukizwa corona au idadi ya vifo kuwa hivi nia yao au lengo lao ni lipi?

Leo waziri Mwalimu ametoa taarifa ya kifo kimoja kilichotokea kwa wagonjwa waliokuwa wamelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa corona, katika twitter Ya zito kabwe ameuliza kuwa mheahimiwa huyu ni wa kwanza Au ni wapili?

Akimaaanisha kuwa kuna mwingne kafichwa, hivi wafiche ili isaidie nini? Kwa nini mnalazimisha idadi ya uongo akina zito?

Hivi kila aliekufa kwenu nyie mnadhani kafa kwa corona? Watu wanakufa hospitalini na wanaojua wamekufa kwa kifo gani ni madaktari na wapo wanokufa wakiwa na Dalili zooote za corona Lakini sio corona iliyowauwa, yapo magonjwa mengne yanayofanana na corona kidalili mfano dengue na magonjwa mengne, halafu sidhani Kama kuna sababu ya watu kurazimisha kifo cha mgonjwa aliekufa kwa marelia kitangazwe kuwa kimeyokana na corona, halafu mbona zito kabwe unalazimisha? Kwa nini unalazimisha?

Mimi nadhani faida kubwa ni kutotangaza idadi kubwa ya vifo, anaesema kuwa kutangaza idadi kubwa ndio suruhisho anatakuwa anafikiria kisiasa tu, majanga Kama vifo kwenye Vita hupaswi kuweka wazi, watu watakufa wengi kutokana na hofu, msikimbilie kutangaza vifo vingi, ikiwezekana vicha,

watanzania wana mawazo Sana ukianza kutangaza vifo utauwa watu Kwa mawazo zito, acha kukaaa unasubiria vifo, usifananishe wazungu na waafrika, acha kushabikia vifo zito kabwe serikali inashughulikia hili swala kwa tahadhali kubwa ikijua kuwa ikikurubuka itaumiza zaid! Acha siasa zito kwenye mambo ya msingi tuuungane kwenye janga tuangalie ni kipi cha unafuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani nasoma kama naongea
 
Idd Mbita nakuombea heri upumzike kwa Amani upate raha na pumziko lisilo na Mawaa!
 
Back
Top Bottom