KERO Serikali, mna mpango gani na Usafiri wa Treni? Mnatuwekea siku maalum ya kukata tiketi, halafu tukifika kukata, mnasema nafasi zimeisha?

KERO Serikali, mna mpango gani na Usafiri wa Treni? Mnatuwekea siku maalum ya kukata tiketi, halafu tukifika kukata, mnasema nafasi zimeisha?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
KUFA NI KUFA TU NA MLAANIWA NI MLAANIWA TU
 
Attachments

  • Screenshot_20241211-065436_Google.jpg
    Screenshot_20241211-065436_Google.jpg
    149.3 KB · Views: 3
Wana JF mmelala?

Jamani hivi hizi train zipo kwaajiri Gani? Ukiachana na SGR Kuna Train inaitwa Deluxe, watu WA kigoma mwanza Tabora mtakuwa mnanielewa.

Hii Train inaelekea mkoani kutoka dares salaam, mara Moja Kwa week, ambayo ni Alhamis. Na nauli Huwa ni elfu 36 third class na elfu 48 second class ila sasahivi nauli zimebadilika third class ni 48 na second class ni 65😟😟. Je hii ni Kwa maelekezo ya TRC?

Hii Train zimewekwa siku maalumu ya abiria kwenda kukata tiketi, nayo ni J.Nne na J Tano Tu, ukienda tofauti na hapo haupati tiketi.

Sasa tuseme hii ni sheria imewekwa, mbaya na ya kusikitisha zaidi ni kwamba ukienda J.nne ambayo ndio siku ya kukata tiketi unaambiwa train imejaa!

Mi hii nilihisi ni uongo, ila Leo Nimeenda Jana nilienda kukata tiketi ya kuelekea mwanza nikaambiwa siku ya kukata tiketi ni J nne na J.tano, Leo Nimeenda saa3 naambiwa train imejaa😟😟😟.

How comes??? Yaani siku ya Leo ndio ya kukata tiketi halafu saa3 tayari imejaa? Halafu nikataka kukata tiketi ili nisafiri Alhamis ijayo naambiwa siruhusiwi kukata mpaka J.nne ya week ijayo,

hivi jamani, mnajaribu kuelewa hili suala?? Hii inamaanisha nini?

Kama Serikali inaweka huduma halafu inahudumia inavyotaka maana yake Nini?

Hii inaumiza watu wengi wanaotumia usafiri WA Train, hizi tiketi tunazoambiwa zimeisha zinaenda wapi?

Serikali Ina mpango Gani na hizi huduma za Train za ajabu?
Siku nyingine kata.online siku yoyote afu wapeleeke uone kama wanaikataa. Online Hakunaga siku.maaluumu ilimradi train IPO.

Wafanyakazi wa.pale station wanadhani kila anayesafiri na MGR ni mchunga ng'ombe Wana madharau sana

Nakubaliana na weww mtoa mada bongo tuna watendaji wapumbavu kupitiliza..maajabu baadhi ya mabehewa ya second class fan na charger za simu hazifanyi KAZI
 
Mambo mawili makuu
  1. Rushwa
  2. Hujuma
Kwanini hawataki kudigitize hiyo huduma ya ticketing
No unakataa online. Sema watumiaji wengi es MGR ndo hivyo Tena wanaliwa sana hela na station masters Kwa kuiziwa seat
 
Huu upuuzi hata kwenye treni ya TAZARA kipindi hicho ulikuwa unafanyika sana. Sijui siku hizi kama wamebadilika.

Imagine unaenda stesheni na hela yako ya kutosha tu!
Unawaambia unataka second class au super seater, halafu wanakuambia eti nafasi zimejaa! Na ukikata 3rd class ambako nafasi huwa hazijai, umekwisha! Maana huko kuna vibaka wengi mpaka basi. Ukijisahau tu na kusinzia, ukishtuka wamekuibia kila kitu.
 
Siku nyingine kata.online siku yoyote afu wapeleeke uone kama wanaikataa. Online Hakunaga siku.maaluumu ilimradi train IPO.

Wafanyakazi wa.pale station wanadhani kila anayesafiri na MGR ni mchunga ng'ombe Wana madharau sana

Nakubaliana na weww mtoa mada bongo tuna watendaji wapumbavu kupitiliza..maajabu baadhi ya mabehewa ya second class fan na charger za simu hazifanyi KAZI
Dah Asante sana, sitokuja kurudia kunichanganya kuplan kusafiri Kwa train😏😏😏. Yaani kumbe hadi second class Kuna ujinga hovyoooo
 
Huu upuuzi hata kwenye treni ya TAZARA kipindi hicho ulikuwa unafanyika sana. Sijui siku hizi kama wamebadilika.

Imagine unaenda stesheni na hela yako ya kutosha tu!
Unawaambia unataka second class au super seater, halafu wanakuambia eti nafasi zimejaa! Na ukikata 3rd class ambako nafasi huwa hazijai, umekwisha! Maana huko kuna vibaka wengi mpaka basi. Ukijisahau tu na kusinzia, ukishtuka wamekuibia kila kitu.
3 class ni balaa tu usilogwe, labda kama unafanya utafiti maalumu na uende umejiandaa kisela sela
 
Back
Top Bottom