Serikali msijisahau katika hili la daktari kumtibia mtu wa jinsia tofauti na yeye

Jinsia nyingi ni zipi hizo...mi naziona 2 tu!!
 
Bado hoja iko pale pale kuwa tuzalishe madaktari wengi wa kike ili kuoumguza tatizo
Nilikuwa sijaona signature yako!! kumbe tatizo ni mimi. Nakushauri ikikupendeza usipenyeshe tamaduni ulizo karirishwa dhidi ya jinsia nyingine, waache waamue wao! wana midomo???

km hawataki kusomea hayo??
 
km hawataki kusomea hayo??
Wapo wanaotaka wanakwamishwa na sababu mbalimbali.
waache waamue wao! wana midomo???
Ili waamue lazima wawepo na hao madaktari wa kike,hapo ndo uamuzi utakuwepo.

Yani umepika ugali tu alafu umemuweka mtu na njaa unamuambia achague chakula anachotaka alafu kuna ugali tu,lazima acjague huo ugali uliokuwepo

Ili waachiwe waamue basi na hao madaktari wa kike wawepo kwa wingi alafu tuone watachagua wapi.

Sasa hivi hata wakichagua bado wanaume ni wengi,na huko sio kuchagua,hata mimi naumwa naenda spitali nakuta daktari wa kike nachagua nini sasa zaidi ya kutibiwa na huyo huyo mwanamke ?
 
Kma umegraduate Univer. yeyote unajua idadi ya wanafunzi Madaktari ke'' waliopo kwenye vyuo vikuu vya tiba hata Leo hii, ni wengi kuliko me''

TMK Hospital Asha Mahita ndo mkuu alifanya vizuri pale kabla hajamwachia Malima,
Mganga Mkuu wa wilaya Sylvia Mamkwe demu!
Bado wakuu wa Idara wote wanawake, TMK OBGY dr Khadija Muarabu.

bado Mganga Mkuu mkoa ni Mdada hapo ni Bongo tu unataka idadi ipi?? uridhike??

Dr Beatrice mganga mkuu Dharula DSM me wanaongozwa na Ke'' mbona hawaja lalamika?
 
Hatuangalii nani anaongoza idara mkuu.

Kuongoza wanawake vitengo hivyo hakufanyi uhitaji wa madaktari wa kike zaidi upungue.

Na mimi sijazungumzia wala kutaka wanawake wawe viongozi katika vitengo mbalimbali hilo ni laako wewe mkuu.
Kma umegraduate Univer. yeyote unajua idadi ya wanafunzi Madaktari ke'' waliopo kwenye vyuo vikuu vya tiba hata Leo hii, ni wengi kuliko me''
Sio vyote,pengine vichache viko hivyo na vingi vina idadi ndogo.

Laiti ingekuwa mambo yapo kama unavyosema basi tusingekuwa na uhaba wa madaktari wengi wa kike.

Unalosema pengine ni uhalisia wa vyuo viwili vitatu ama kwa mwana fulani na fulani lakini sio kwamba ni jambo la miaka yote
 
Hoja yako kilojiki(mantiki) imekaa vizuri sana ila kiuhalisia(reality) haiko sawa
Mmoja ka comment humu kuwa vigezo vya udaktari kuusomea vipunguzwe.Naomba nimjulishe kuwa fani ya udaktari ni ngumu mno na fani yake sio fani ya kisiasa kusema vigezo vipunguzwe.
Madaktari wanaweza kuanza kozi 30 wakamaliza 10 au 15.Ukisema vigezo vipunguzwe kwenye maksi za ufaulu kidato cha sita maana yake kwanza hawatamaliza hiyo kozi kwa miaka mitano watafeli wote.Pili akiweza kukatiza utakuwa na daktari feki ambayo vile maisha ya binadamu ni muhimu ni hatarishi sana kupoteza maisha ya watu.
Pia nimjulishe mdau kuwa kuna kozi mfano inaitwa Anasthesia au kiswahili taaluma mtaalamu wa dawa ya usingizi.Hospitali ya Agakakhani pale dar wako watatu tu kati yao hao wawili walikuwa ni waajiriwa jeshini wastaafu.Kwa Tanzania nzima idadi yao haifiki 15 kwa level ya udaktari bingwa na wote ni wanaume.
Kwa vyovyote mwanamke akipatwa na tatizo lazima wanaume ndio wahusika.Ni hivyi kwenye ugonjwa habari ya ujinsia haina mashiko sana Dr ameshakutana na vitu vingi mno yeye anaona kawaida.Mimi niliugua Agakhani dar waliokuwa wananiogesha ni wanawake nikiwa sina fahamu na hata nilivyopata fahamu bado wakawa wao tu.Hali ikiwa ngumu kwenye kumfungua mwanamke mja mzito wanawake ujasiri unatoweka hata kama ni msomi wa taaluma husika hapo wanaume ndio umuhimu wao unapokuja.
Hili la ujinsia kwa kukaguliwa na polisi liko sawa.
 
Shida wewe umeleta dini kwenye mambo makubwa kama haya. Hebu muulize mkeo au dada yako angependa kutibiwa na daktari wa kike au kiume?
 
Shida wewe umeleta dini kwenye mambo makubwa kama haya. Hebu muulize mkeo au dada yako angependa kutibiwa na daktari wa kike au kiume?
Haya ni maoni yako kwa sababu sijataja dini sehemu yeyote.

Na kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni hapa jamvini,siwezi kutumia nguvu kuuuuuubwa kukupinga,it's your opinion😀
 
Wingi wa kesi za madaktari wa kiume kuwaingilia wagonjwa wa kike,zinatosha kutenganisha matibabu kwa jinsia. Muda Sasa, wa kuwa na huduma za afya kwa mujibu wa jinsia Kama ambavyo wodi zao zimetofautishwa
 
Sasa Daktari amespecialize kwenye mambo ya uzazi kwa wanawake
 
Takbiiiiiiiiiiiiiiiiiir.
Allahu Akbar!!!!!!!!!

Mtoa mada isije ikawa ni wale watu wanataka wake zao wazalishwe na madaktari wa kike lkn binti yake/mkewe kusoma na kufanya kazi ni marfuku na wanaamini mwanamke sehemu salama kwake ni nyumbani.
 
Achana na mila kitaaluma hairuhusiwi daktari kujitibu mwenywe au kumtibu Mtu wake wa karibu bila ku consult daktari mwenzake. Kuna kitu inaitwa conflict of intrest.
 
Wanawake wangapi wanakidhi vigezo vya kuwa wabobevu katika magonjwa kada wa kadha??
 
Allahu Akbar!!!!!!!!!

Mtoa mada isije ikawa ni wale watu wanataka wake zao wazalishwe na madaktari wa kike lkn binti yake/mkewe kusoma na kufanya kazi ni marfuku na wanaamini mwanamke sehemu salama kwake ni nyumbani.
Hha hapana mkuu.

Kuna siku nilijadili kwa upana sana na bwana mkubwa humu yeye akiwa na msimamo kama ambao umeutaja hhataki wanawake wasome fani kama za udaktari na wakati huo anaona haifai mwanaume kumtibu mwanamke ana kinyume chake.

Nitakuwa mpumbavu sana ikiwa nataka dokta wa kike atibu mwanamke wakati huo huo nakataa mwanamke asisome haha
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kuna watu wanashambulia utadhani jamaa amesema kwamba mgonjwa anaona aibu wakati jamaa kaweka wazi kabisa hoja zake

Hili ni pendekezo au wazo tu mshkaji ametoa kwamba kwanini na kwenye tiba wasiweke utaratibu wa kuwa asitibiwe mgonjwa na tabibu wa jinsi tofauti (tena akaongezea kabisa "kama kuna tabibu wa jinsi yake eneo husika") ili kulinda heshima ya utu wa mgonjwa kama ilivyo kwenye polisi na kwingineko?

Sasa wewe unakurupuka tu ooh hujaumwa wewe mara mwingine ooh ugonjwa hauna aibu... sasa kwani kuna sehemu hapo kaandika kuwa anashauri hivyo kwakuwa mgonjwa anaona aibu?
 
Mkuu ndo wana jf tulivyo na nimeshaona tatizo hilo ndio maana siwi kimya kujibu kwa sababu ya kutetra ninachosema.

Nilichoshauri kama madaktari wa kike hawatoshi basi mikakati ipangwe kuongeza madaktari,na kama wapo hao wa kike wa kutosha basi serikali itilie mkazo na kuweka sheria ambazo zitazuwia jambo hili.

Watu wanakuja wananiuliza maswali mengine kabisa,ila ndo JF ukitegemea hoja yako aikubali kila mtu basi inaweza kutukana kila mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…