CONSISTENCY
Senior Member
- Feb 16, 2023
- 135
- 309
Binafsi nasikitika kuona Tamthilia hizi za Kituruki, kihindi, kikorea, kichina, kiarabu n.k zilizotafsiriwa kwa lugha yetu ya Taifa kiswahili zinazooneshwa sana muda mwingi katika chanel zetu maarufu nchini hasa Azam kila nikiingia nyumbani, saloon, bar, hotel n.k.
Serikali hasa Wizara ya sanaa na michezo tunaomba simamisheni kuonesha hizi Tamthilia sababu hakuna faida ya hizi Tamthilia kwa jamii yetu na kama Kuna faida za kimapato au kimaadili tunaomba jamii ielezwe.
Kwanza kinachoonesha kwenye hizo Tamthilia hakiendani kabisa na Mila, desturi, utamaduni wetu n.k kuanzia mazingira, location, nidhamu, mavazi n.k kinachoonesha katika hizo Tamthilia ni kuifanya jamii ya kitanzania iamini kwamba maisha wanayoishi hao watu ni Bora na ya maana kuliko maisha ya kitanzania mfano mtoto mdogo atataka kuiga tabia za mtoto wa kwenye Tamthilia kuliko kufuata kile anachoambiwa na wazazi wake.
Kwa kifupi hizo Tamthilia zinasababisha mmonyoko mkubwa wa maadili kwa jamii nzima, kitu kibaya zaidi hizo Tamthilia zinaoneshwa mda wote kuanzia asubuhi Hadi usiku, utasikia hiki ndio kipindi haya ni marudio n.k ila zinaoneshwa siku nzima.
Serikali Kuna mambo mengi yakuonesha jamii kwenye chanel zetu ikiwemo kilimo, biashara, ufundi, fursa nje ya nchi n.k
Hata kama jamii inapenda lakini mda mwingine inawezekana jamii inapenda sababu ya nguvu inayotumika kuonesha kwamba hizo Tamthilia zina maana kumbe ni ujinga mtupu.
Wito wangu kwa serikali simamisheni hivyo vipindi sababu havina faida yeyote kwa jamii.