Serikali na Hatima ya Tamthilia za kigeni zilizo lugha ya Kiswahili kwa Kizazi Chetu

Serikali na Hatima ya Tamthilia za kigeni zilizo lugha ya Kiswahili kwa Kizazi Chetu

Ukiona katika nchi kila kinachoonekana kwenye vyombo vya habari vinaathiri mwenendo wa jamii husika, manake ni kwamba jamii hiyo katika nchi husika ni vilaza katika kusimamia yaliyo ya kwao.Dunia ya leo huwezizuia mambo hayo ukizingatia viongozi hawajui wanasimamia nini wala hawajui kwanini wapo kwenye nyadhifa zao.
Hii ni hatari sana ndugu, ila nafikiri Azam analipwa pesa nyingi kwa kuonesha hizo Tamthilia
 
Binafsi nasikitika kuona Tamthilia hizi za Kituruki, kihindi, kikorea, kichina, kiarabu n.k zilizotafsiriwa kwa lugha yetu ya Taifa kiswahili zinazooneshwa sana mda mwingi katika chanel zetu maarufu nchini hasa Azam kila nikiingia nyumbani, saloon, bar, hotel n.k.

Serikali hasa Wizara ya sanaa na michezo tunaomba simamisheni kuonesha hizi Tamthilia sababu hakuna faida ya hizi Tamthilia kwa jamii yetu na kama Kuna faida za kimapato au kimaadili tunaomba jamii ielezwe.

Kwanza kinachoonesha kwenye hizo Tamthilia hakiendani kabisa na Mila, desturi, utamaduni wetu n.k kuanzia mazingira, location, nidhamu, mavazi n.k kinachoonesha katika hizo Tamthilia ni kuifanya jamii ya kitanzania iamini kwamba maisha wanayoishi hao watu ni Bora na ya maana kuliko maisha ya kitanzania mfano mtoto mdogo atataka kuiga tabia za mtoto wa kwenye Tamthilia kuliko kufuata kile anachoambiwa na wazazi wake.

Kwa kifupi hizo Tamthilia zinasababisha mmonyoko mkubwa wa maadili kwa jamii nzima, kitu kibaya zaidi hizo Tamthilia zinaoneshwa mda wote kuanzia asubuhi Hadi usiku, utasikia hiki ndio kipindi haya ni marudio n.k ila zinaoneshwa siku nzima.

Serikali Kuna mambo mengi yakuonesha jamii kwenye chanel zetu ikiwemo kilimo, biashara, ufundi, fursa nje ya nchi n.k

Hata kama jamii inapenda lakini mda mwingine inawezekana jamii inapenda sababu ya nguvu inayotumika kuonesha kwamba hizo Tamthilia zina maana kumbe ni ujinga mtupu.

Wito wangu kwa serikali simamisheni hivyo vipindi sababu havina faida yeyote kwa jamii.
familia zetu zinapaswa kupata chakula bora, mavazi na maradhi, ili kujenga kizazi bora kijacho, hili ni jukumu la baba, mama na wanajamii
 
Azam ni mfanyabiashara na mfanyabiashara anajali faida tu, Lakini lazima ana baraka za serikali kupitia wizara husika.
Inawezekana, hawa jamaa wanatumika sana na kufanya Dili chafu kwenye jamii.
Ukianzia kwenye energy drink, Tamthilia n.k ni hatari tupu
 
familia zetu zinapaswa kupata chakula bora, mavazi na maradhi, ili kujenga kizazi bora kijacho, hili ni jukumu la baba, mama na wanajamii
Umesahau kwamba kwenye kujenga maadili na serikali inahusika kutokana na utandawazi jinsi ulivyo
 
Bongo muvi mnazingua ndiomana hatupendi kuwaangalia, jini linavuka barabara huku linatazama kushoto na kulia kweli??
 
Maadili ya kitanzania ni kujiepusha na maadili ya hovyo kama ushoga, kuwa na heshima kwa wazazi n.k
Kwanini iwe heshima kwa wazazi na isiwe kuheshimiana kati ya watu wote?vile vikundi vya ngoma vinavyochezaga nusu uchi, wasanii especially wa kike wanaovaa nusu uchi, vipi hayo ni maadili ya kitanzania na kama sio kwanini yamehalalishwa?
 
Bongo muvi mnazingua ndiomana hatupendi kuwaangalia, jini linavuka barabara huku linatazama kushoto na kulia kweli??
Upo sahihi, ila huu uzi hauhusiani na bongo movie.
 
Kwanini iwe heshima kwa wazazi na isiwe kuheshimiana kati ya watu wote?vile vikundi vya ngoma vinavyochezaga nusu uchi, wasanii especially wa kike wanaovaa nusu uchi, vipi hayo ni maadili ya kitanzania na kama sio kwanini yamehalajishwa?
Ni jamii ngapi za kitanzania zinafanya hilo jambo ukiacha watu wenye asili ya pwani kama wazaramo, wakwere, waruguru?
Unajua kwamba hizo Tamthilia za kigeni zinaangaliwa nchi nzima kwenye TV?
 
yana madhara makubwa kwa jami
Sure ndugu yangu, athari ni kubwa mno, watu wengi wana focus kwenye hizo tamthilia hata taarifa ya habari hawana haja nayo .

Kijana wa makamo anakuelezea mwelekeo wa tamthilia kwa ufasaha lakini hana taarifa yoyote ya kitaifa.

Juzi tu kijana mmoja wa kike hajui kama sera mpya ya elimu ipoa imesha anza kazi kwamba elimu ya msingi sasa ni miaka kumi, hilo hajui ila anakuelezea barabara tamthilia za kituruki kana alikua miongoni mwa walio iandaa!
 
Sorry umeandika elimu ya msingi ni miaka sita au kumi?
 
Ni jamii ngapi za kitanzania zinafanya hilo jambo ukiacha watu wenye asili ya pwani kama wazaramo, wakwere, waruguru?
Unajua kwamba hizo Tamthilia za kigeni zinaangaliwa nchi nzima kwenye TV?
Apana! Bila shaka utakua unazungumzia vigodoro lakini mimi simanishi hivo japo navyo ni kichefuchefu. Kuna vile vikundi ambavyo hata mgeni wa heshima akija katika nchi hupokelewa na vikundi hivyo vya ngoma airport.Vilevile tuna wasanii wetu wa kike wanavaa nusu uchi na wasanii wetu wa kiume wanatoboa pua, kuvaa hereni, kusuka nywele, kuvaa nguo za kina dada n. k , hayo yote yanachigiza hayo mambo ya ushoga na tabia zingine chafu. Huoni kwamba kabla ya kutaka tamthilia za nje zikemewe tuanzie ndani kwanza?
 
Hii tamth

Hii tamthilia inaitwa PRIMA DONAS inaonyeshaa na AzamTv, **** muhusika mmoja ni mwanafunzi wa kiume anasoma na mtoto mwenzie anaitwa BRIANNA, huyo mwanafunzi wa kiume naona kama ana itikadi za KISHOGA kabisa, kuanzia ongea na mpaka alivyo na jinsi anaweka mikono yake akiwa ana ongea.

Sijui watoto wa kiume wana jifunza nini wakiona hizi tamthilia hasa hako kavulana.
Ndo nia kuu ya huu uzi kujadili ushoga, kwan mashoga wote hawa walianza kwa kutazama tamthilia?

Huwa hamna hoja nyingine?
 
Maadili ya kitanzania ni kujiepusha na maadili ya hovyo kama ushoga, kuwa na heshima kwa wazazi n.k
Yaan nia yako kupinga ushoga, jamani ushoga hata hauenezwi na tamthilia, polee wee
 
Apana! Bila shaka utakua unazungumzia vigodoro lakini mimi simanishi hivo japo navyo ni kichefuchefu. Kuna vile vikundi ambavyo hata mgeni wa heshima akija katika nchi hupokelewa na vikundi hivyo vya ngoma airport.Vilevile tuna wasanii wetu wa kike wanavaa nusu uchi na wasanii wetu wa kiume wanatoboa pua, kuvaa hereni, kusuka nywele, kuvaa nguo za kina dada n. k , hayo yote yanachigiza hayo mambo ya ushoga na tabia zingine chafu. Huoni kwamba kabla ya kutaka tamthilia za nje zikemewe tuanzie ndani kwanza?
Upo sahihi kwa upande huo ila hayo mambo yanamatokeo mabaya kidogo kwa sababu jamii haioni kila siku.

Hizo Tamthilia nazungumzia sababu jamii inaona kila siku kuanzia asubuhi Hadi usiku hivyo imegeuka kama ndio mtindo wa maisha wa Kitanzania
 
Back
Top Bottom