Serikali na Hatima ya Tamthilia za kigeni zilizo lugha ya Kiswahili kwa Kizazi Chetu

Serikali na Hatima ya Tamthilia za kigeni zilizo lugha ya Kiswahili kwa Kizazi Chetu

Unachoongea ni kweli ila ume exaggerate sana
Japo hata mimi niliwahi kuwaza kama wewe hasa katika nyanja ya kuathiriwa kitamaduni
Vibinti vingi vimekuwa brainwashed na tamthilia hadi vinakataa utu wao kiafrika na kuona kuwa mwafrika ni laana, wengi wanatamani kuwa na watoto weupe na huwapa majina ya kituruki
Yaani jamii ishakuwa brainwashed sana, nadhani tamthilia za hapa nyumbani zingepewa kipaumbele maana zinagusa dhima halisi ya maisha ya kitanganyika
Mfano wa tamthilia bora kwangu ni hii MTAA WA KAZAMOYO na ZAHANATI YA KIJIJI
Asante kwa huo ushuhuda uliouona kwa watoto wako, kwa kifupi asilimia kubwa ya jamii nzima ipo kama hao watoto wako.
Nini Hatima ya Kizazi Chetu cha Kitanzania kuwaiga hao watu wa kwenye Tamthilia?
 
Hii tamth
Binafsi nasikitika kuona Tamthilia hizi za Kituruki, kihindi, kikorea, kichina, kiarabu n.k zilizotafsiriwa kwa lugha yetu ya Taifa kiswahili zinazooneshwa sana mda mwingi katika chanel zetu maarufu nchini hasa Azam kila nikiingia nyumbani, saloon, bar, hotel n.k.

Serikali hasa Wizara ya sanaa na michezo tunaomba simamisheni kuonesha hizi Tamthilia sababu hakuna faida ya hizi Tamthilia kwa jamii yetu na kama Kuna faida za kimapato au kimaadili tunaomba jamii ielezwe.

Kwanza kinachoonesha kwenye hizo Tamthilia hakiendani kabisa na Mila, desturi, utamaduni wetu n.k kuanzia mazingira, location, nidhamu, mavazi n.k kinachoonesha katika hizo Tamthilia ni kuifanya jamii ya kitanzania iamini kwamba maisha wanayoishi hao watu ni Bora na ya maana kuliko maisha ya kitanzania mfano mtoto mdogo atataka kuiga tabia za mtoto wa kwenye Tamthilia kuliko kufuata kile anachoambiwa na wazazi wake.

Kwa kifupi hizo Tamthilia zinasababisha mmonyoko mkubwa wa maadili kwa jamii nzima, kitu kibaya zaidi hizo Tamthilia zinaoneshwa mda wote kuanzia asubuhi Hadi usiku, utasikia hiki ndio kipindi haya ni marudio n.k ila zinaoneshwa siku nzima.

Serikali Kuna mambo mengi yakuonesha jamii kwenye chanel zetu ikiwemo kilimo, biashara, ufundi, fursa nje ya nchi n.k
Hata kama jamii inapenda lakini mda mwingine inawezekana jamii inapenda sababu ya nguvu inayotumika kuonesha kwamba hizo Tamthilia zina maana kumbe ni ujinga mtupu.

Wito wangu kwa serikali simamisheni hivyo vipindi sababu havina faida yeyote kwa jamii.
Hii tamthilia inaitwa PRIMA DONAS inaonyeshaa na AzamTv, **** muhusika mmoja ni mwanafunzi wa kiume anasoma na mtoto mwenzie anaitwa BRIANNA, huyo mwanafunzi wa kiume naona kama ana itikadi za KISHOGA kabisa, kuanzia ongea na mpaka alivyo na jinsi anaweka mikono yake akiwa ana ongea.

Sijui watoto wa kiume wana jifunza nini wakiona hizi tamthilia hasa hako kavulana.
 
Bado haujaelewa, Kuna nguvu kubwa inayotumika kutangaza hivyo vipindi ila jamii iamine ni vipindi vizuri.
Unajua kitu kinaitwa culture transmission?
Au unaweza kutuambia faida ya hivyo vipindi kwenye jamii yetu?
Kwani culture ni nini?

Nahisi ni mambo ya utamaduni mila desturi.

Kuiga utamaduni wa mtu mwingine kama umeona kuwa ni mzuri na una faida ni vibaya?

Ni lazima ung'ang'anie utamaduni wako hata kama umegundua ma mila mengine ni kwa sababu ya kukosa elimu na ni ya hovyo?

Nimeuliza hivyo kwa sababu nimehisi kuwa wasiwasi wako ni kupotea kwa culture zetu na kuigwa kwa tamaduni za kigeni.
 
Hehe kuna trend ya kutoa majina ya watoto siku hizi siielewi,,,tamthilia kweli zina nguvu
Hiki ni kitu kibaya sana ndugu, imefika kipindi wanawake hawataki watoto weusi, wanataka watoto weusi wanaofanana na wenye kwenye Tamthilia
 
Unaweza usieleweke na wengi ila hoja yako ina maana kubwa na inatakiwa kuungwa mkono.
Athari ni kubwa mno , na haswa kizazi kinachokuja.
Kuna mambo ya ajabu yanafanyika ila kwa sababu serikali haiyakatazi yanaonekana ni kawaida ila kwa ufupi yana madhara makubwa kwa jamii hasa hizi Tamthilia za kigeni kwa kiswahili
 
Your an idiot with inferiority complex
Respond with facts,.. your response determines the level of your stupidity.

Eti tamthilia za kigeni zisioneshwe, kwanza unanipotezea muda tu hapa, nacheki Golden Boy, ikiisha inakuja Barbarosa
 
Kwa kesi kama hiyo ndo utaona siku zikianza kuingizwa ajenda mbaya za nje jamii itaathirika sana nadhani tunapaswa kuulinda utambulisho wetu kama watanzania hizi tamthilia za nje zimezidi sana siku hizi ukiwa na mtoto mweusi atatengwa
Ukizaa mweupe utasikia "katoto kako kazuri kama mturuki au mkorea"

Vibinti vya siku hizi haviamini unaweza kuwa mbantu na ukawa mrembo
Hiyo ni hatari sana kwa mabinti zetu
 
Ukiona katika nchi kila kinachoonekana kwenye vyombo vya habari vinaathiri mwenendo wa jamii husika, manake ni kwamba jamii hiyo katika nchi husika ni vilaza katika kusimamia yaliyo ya kwao.Dunia ya leo huwezizuia mambo hayo ukizingatia viongozi hawajui wanasimamia nini wala hawajui kwanini wapo kwenye nyadhifa zao.
 
Hii tamth

Hii tamthilia inaitwa PRIMA DONAS inaonyeshaa na AzamTv, **** muhusika mmoja ni mwanafunzi wa kiume anasoma na mtoto mwenzie anaitwa BRIANNA, huyo mwanafunzi wa kiume naona kama ana itikadi za KISHOGA kabisa, kuanzia ongea na mpaka alivyo na jinsi anaweka mikono yake akiwa ana ongea.

Sijui watoto wa kiume wana jifunza nini wakiona hizi tamthilia hasa hako kavulana.
Ndugu, ni hatari sana.
Binafsi nahisi Azam analipwa pesa nyingi sana kwa kuonesha hizo Tamthilia.
Haiwezekani kuanzia asubuhi Hadi usiku Tamthilia ni hizo hizo hazina maadili wala heshima za kiafrika
 
Kwani culture ni nini?

Nahisi ni mambo ya utamaduni mila desturi.

Kuiga utamaduni wa mtu mwingine kama umeona kuwa ni mzuri na una faida ni vibaya?

Ni lazima ung'ang'anie utamaduni wako hata kama umegundua ma mila mengine ni kwa sababu ya kukosa elimu na ni ya hovyo?

Nimeuliza hivyo kwa sababu nimehisi kuwa wasiwasi wako ni kupotea kwa culture zetu na kuigwa kwa tamaduni za kigeni.
Culture ni kudumisha heshima ya jamii ikiwemo kuwa na heshima kwa wazazi wako, kujiepusha na vitendo vya aibu kama ushoga, kujiuza n.k
 
Naunga mkono hoja hizi tamthilia zinachangia pakubwa ongezeko la, wadangaji aka ombaomba na mario.
Watu hawajui tu ndugu, hizi Tamthilia zinaharibu jamii pakubwa sana, humo Kuna ushoga n.k
 
Back
Top Bottom