Serikali na Jeshi la Polisi kuweni Makini na Mnaponunua Risasi zenu. Hatari ipo kwetu

Serikali na Jeshi la Polisi kuweni Makini na Mnaponunua Risasi zenu. Hatari ipo kwetu

Watu mmekaa ki malalamiko sana, hujui kwamba risasi zinazopigwa juu zikirudi zinaweza kujeruhi mtu na hata kumuua?
Hata mlio tu baada ya kuwa risasi kufyatuka huwa unajeruhi
 
Inaonekana hizi risasi zinazotumika kwenye silaha zetu nyingine ni fake au zina tatizo flani. Mara kadhaa imetokea Polisi wanapiga Risasi Juu kutawanya watu. Yenyewe inakata kona na kwenda kumfuata mtu aliye chini.

Kuna haja Serikali iangalie hizi zinatengenezwa wapi. Isije ikawa ni za Kichina au wanatengeneza hapo Mbozi Mkoa wa Songwe. Inasikitisha. Tunajua makosa si ya Askari maana wao huwa hawahukumiwi kwa jambo hili. Basi angalau anayenunua hizo Silaha awe anawajibishwa.

View attachment 2232054

FF4A6C63-F89A-4B6F-847C-815D4FDE20A4.jpeg
 
Back
Top Bottom