Serikali na Wadau wa afya sikieni kilio hiki cha NHIF

Wanaona wanaokoa hela ya mfuko, lakini in return matokeo ni kuongeza gharama zaidi. Mtu anapewa mojawapo ya hitaji, nyingine anaenda kuitafuta kesho kwa consultation nyingine.

Mambo haya yameleta uoga kwa matabibu, kiasi kwamba kila mtu anadonoa donoa tu.

Kama watu walikuwa wanaona paracetamol za siku tano ni nyingi, mtu anapewa za siku tatu. Baada ya hapo, siku tatu homa ya viral bado ipo. Mtu anaenda tena kituoni anakwambia dawa ya kushusha homa imeisha. Hapo lazima review ifanyike tena, ili kujiridhisha ingawa likely it was a viral from the beginning ila kwa sababu hukumuona wewe inabidi kupata uhakika.

NB: Mentality ya watendaji wa NHIF kuwa wameshika mpini inabidi kubadilike. Wao wenyewe wakiumwa hawako tayari kutendewa kama wanavyojaribu kuhimiza wenzao watendewe, maana yake kuna walakini katika wanayoyahimiza.

Nadhani mifuko mingine ya afya ingekuwa ya kwanza kulalamika kwani hawana restrictions kama NHIF. Kuna haja ya kujitafakari wao pia.
 
Nchi ya majizi hii, nawe jitahidi tu kukwapua hapo ulipo….. hakuna namna.
Tutazama wote mwisho wa siku.
Ni vyema kushauriana ili kutatua tatizo na si kutoboa mtumbwi.
Hayo ni mawazo ya aliyekata tamaa.
 
Una ushahidi au ni mhemko wako tu?

Sent from my SM-N986B using JamiiForums mobile app
1: Nimefanya kazi na NHIF, huu mwaka wa 10.
2: Nilishafanya trainning yao kuwa Quality officer.

NB: Tunapoongea hapa ni kujaribu kuwapa mawazo yanayoweza kuwasaidia ili waende vyema na si kwa nia mbaya. Wakiona yapo ya kuwasaidia watachukua, wakiona hayasaidii wanayaacha. Maana kwenye vikao tumekuwa tukieleza haya. Ni vyema kuendelea kuwaeleza kuliko kukaa kimya wanapopiga mayowe ya msaada.
 
Kwa walichofanywa wamasai Ngorongoro mtu pekee wa kuingilia hili ni MrusiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Wanaume wapo Sri Lanka na huko Guinea, kote huko Sudan , Libya, Somalia ndo kuna watu wanaojitambua
 
Uko vizuri
 
NHIF inapigwa peupe, nimempeleka dogo hosp anabima natumiwa msg na NHIF eti jumla ya matibabu ni tshs. 34,000 ilibd nicheke dawa zenyewe za mafua mbili ambazo pharmacy haizid 10k[emoji23][emoji23].

Kuna haja serikali kuunda mfumo bora lasivyo watapigwa sana.
 
Simple serikali iandae utaratibu mteja awe anapewa copy yake ya matibabu na ispecify huduma alizopewa mfano dawa alizopewa, vipimo pamoja na gharama zake. Mteja asaini na hospital isaini mteja aondoke na copy yake afu ile copy itumwe NHIF.

Nhif kuna wapigaji kule na haya malalamiko yameanza kipindi cha walamba asali.
 
Hili la CO, AMO n.k kutofahamua dawa za level za juu limeliona sana Halafu hata hawajishtukii wanaendelea kuziandika tu na kumuacha mgonjwa kwenda kupambana huko nje na 2C(hizi kwenye Health Center hazijafutwa)
 
Kwenye NHIF udanganyifu ni mwingi mnoo..
Kwa sababu hamna mfumo wa kuzuia udanganyifu.

NHIF inatakiwa watafute mfumo thabiti wa kuzuia udanganyifu.

Hivi nchi za wenzetu mifumo yao ikoje?(hapa nahitaji kuingia chimbo nione wenzetu mifumo yao ilivyo)
 
Kwa sababu hamna mfumo wa kuzuia udanganyifu.

NHIF inatakiwa watafute mfumo thabiti wa kuzuia udanganyifu.

Hivi nchi za wenzetu mifumo yao ikoje?(hapa nahitaji kuingia chimbo nione wenzetu mifumo yao ilivyo)
Nadhani kwa wenzetu, uwepo wa mifumo ambayo ni linked national wise inasaidia.

1: Mgonjwa akionwa kituo chochote, anaonekana kwenye mfumo wa taifa kwani anatumia namba yake ya kuzaliwa, ambayo ni unique mfano kwa hapa ni zile za NIDA.

2: Mgonjwa ni lazima aanzie kwenye kaya yake kwa family physician au mtoa huduma wa chini na apewa rufaa kama shida ni kubwa. Ataanzia juu kama ni emergency tu.

Si mtu anatoka nyumbani anaenda kumsaka daktari bingwa wa uzazi au mishipa ya fahamu. Kumbe tatizo lake angeweza kuhudumiwa na watoa huduma wa kawaida. Hivi vingesaidia tracing za wagonjwa wetu na matumizi ya bima kwani wengi wa wagonjwa wanaonyesha kutokujali. Mtu anakuja anatoa kadi, akifika kwa daktari unamweleza kuwa kwa huduma hii hukustahili kutoa kadi yako kulipia.
Jibu: Si nimelipa kumwona daktari shida iko wapi??
 
Huyo mlevi alinipita hapa TikTok anaenda kuongeza
 

Nadhani hapa ndo sisi wenye bima/wachangiaji tulitakiwa kuhakiki kiasi cha gharama za huduma dhidi ya ile iliyopelekwa kwaajili ya malipo.

Ni haki yako kupata risiti ya maelezo ya aina ya huduma na gharama zake. Kama haziendani then uwajulishe, hili ndili lengi kuu la ule ujumbe. Maana wewe ndiye uliyepata huduma.
 
Nchi za Afrika zina kundi la watu wanaokula nchi na walalahoi.mtapiga kelele sana
 
Na wagonjwa siku hizi tuna-google, ukinitibu hivyo nakuona hufai kwenye taaluma yako na wewe ni kajanja! Nikija kwenye kituo chako na dawa fulani nikakosa najua kituo ni cha wababaishaji, sitajua kuwa haiwezekani kituo kikawa na dawa zote zinazohitajika kwa matibabu. Nikikukuta zahanati au kituo cha afya ukashindwa kunipa pantoprazole nitakushangaa (kumbe inatakiwa kutolewa na MD na wewe ni CO), ukiniambia basi kanunue au lipia unisaidie napiga simu NHIF nawaambia kituo kinanitoza pesa ili kiniibie! Nikija na kidonda Polyclinic na ukakataa kunifanyia dressing napiga simu NHIF kuwaambia mmekataa kunipa huduma mnataka pesa yangu (kumbe dressing haipo kwenye kitita kwa polyclinic).

Mtandao wa NHIF ukisumbua mkaniambia hebu subiri utengamae ili unipe huduma nasonya na kuwaambia nyie ni wababaishaji! halafu napiga simu NHIF kulalamika, NHIF wanakuwa wakali na kutaka mimi na wenzangu tupewe huduma ila tuache kadi. Lahaula tukiondoka na mtandao ukarudi unakuta mimi au mwenzangu kadi zetu zimekuwa rejected na tumeshatibiwa, kama umepata hasara shauri yako NHIF hawatakulipa.

Halafu kuna madaraja ya wagonjwa hatujui, nikija kutibiwa na akaja mwanachama wa fast track kama BOT, NMB au TRA anapitiliza moja kwa moja kwa daktari maalum huku nikiwa nimepanga foleni na wenzangu (naanza kulaumu jinsi watoa huduma walivyo na upendeleo na kujali rushwa) hee, kumbe mwongozo wa NHIF fasttrack anatakiwa apewe upendeleo maalum kwa sababu alilipa NHIF mpunga mrefu! Ghafla naona analazwa chumba cha peke yake na mimi nipo wodi ya jumuiya, nalalamika kwa daktari kwa nini aniweke wodi ya jumuiya wakati mteja mwingine wa NHIF kawekwa private ward. Hatari!!
 
Haaahaaaa
Mkuu ww ni emdii
Unayajua ya mtungini yooteee
Basi Acha tuendelee na eeenhechiaiefuuu
 
Naunga mkono hoja yako mkuu ya kuwa na unique namba kama za NIDA na mgonjwa akitibiwa sehemu inabidi visit yake ionekane National wise na pawepo na udhibiti endapo atataka kwenda kituo kingine bila sababu ya msingi yenye kuonesha ulazima wa kwenda huko.

Pia nilikuwa nawaza, hivi hamna namna pawepo na fingerprint ambazo zitalimit utoaji wa fomu za bima ili mgonjwa ahudumiwe, yaani ili mgonjwa ahudumiwe inatakiwa atumie finger print yake ili kuwezesha fomu yake kutolewa electronically ndipo iweze kujazwa na kusainiwa na pande zote mbili(Daktari na Mgonjwa). Hii itadhibiti mtindo wa fomu kusainiwa pasipo na huduma yeyote kama yanyofanyika kwenye Polyclinic ambapo Specialist anaenda kusaini tu fomu halafu hamna huduma yeyote ile.
 

Hii itasaidia sana ikiunganishwa na live registration/authorization na finger print pia ni njia mwafaka ya kuhakiki gharama halisi za matibabu, maana wahudumiwa wanaonyesha kutokujali sana. Hasa kwa sababu kwenye mfumo wa sasa wanasaini kuandikishwa na si kuthibitisha gharama husika.

Nadhani kwa mfumo wa sasa wa electronic, ilitakiwa kuwepo namna zile gharama kwa kuwa ni electronic basi mtu asaini mwishoni akiwa anaona jumla ya gharama na si kuthibitisha kujisajili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…