Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Inapotokea mfanyakazi wa taasisi fulani amefanya kosa mbele za umma na akaonywa mbele za umma pia, tunatarajia taasisi anayofanyia kazi kuwajibika, kwanza kwa kukubali kuwa kosa limefanywa, kuomba radhi kwa umma, na kuchukua hatua za kinidhamu kama kanuni za maadili zinavyowaelekeza kulingana na taasisi hiyo.
Kilichofanywa na Oscar Oscar pamoja na Makonda ni udhalilishaji na uvunjivu wa haki za binadamu, Wasafi na Serikali kwanza walitakiwa kukubali kwanza kilichofanyika sio sawa na Serikali kama mtetezi mkuu wa haki za binadamu pamoda na Wasafi kama wadau wanaotetea haki za binadamu ilibidi watoe neno na kumtaka aliyefanya ukiukaji huu aombe radhi kwa umma pamoja na kuwachukulia hatua za kinidhamu.
Lakini inashangaza Oscar Oscar hajatoa neno kuomba radhi na taasisi inayomsimamia nayo imekaa kimya wala haijajigusa. Vivyo hivyo kwa Makonda, amedhalilisha mtu afu anakuja kujitapa hawa wananipiga kelele tu nizidi kusonga mbele na kuwashughulikia wajinga. Hakuna mtu anayekubali uzembe, rushwa wala ubadhilifu, lakini unatakiwa kutumia njia sahihi kufanya hivyo.
Ni aibu, huzuni inatia hasira na kinyaa kwamba mpaka sasa serikali haijatoa tamko lolote kumkanya Makonda na kuomba radhi kwa jambo alilofanya. Mnajenga viongozi wa namna gani? Leo Makonda kafanya hili limenyamaziwa kesho litafanyanika kubwa zaidi, ndio mnataka hii iwe norm? Kwakuwa mtu ana mamlaka basi afanye atakavyo?
Mnakuja na hoja za kijinga na kipumbavu kabisa, eti mbona kuna matukio yalitokea nyuma hayakupigiwa kelele, kwahiyo hilo linafanya jambo alilofanya Makonda kuwa sawa? Kwahivyo kila mtu akidhalilishwa hii ndio itakuwa scapegoat (upenyo wa kuchomokea) na kuhalalisha kosa ulilofanya?
Embu tuweni serious basi, serikali msituangushe tukazidi kupoteza imani na nyie zaidi ya hapa tulipofikia, mnatengeneza bomu ambalo hamtaweza kulitegua mbeleni.
====
Pia soma:
- LHRC yamuonya Makonda kwa kumdhalilisha Mtumishi wa Kike mbele ya Umati wa Wananchi
- Makonda ashtakiwe kwa udhalilishaji alioufanya kwa mwanakamati huyu