Serikali: Ndoa za jinsia moja hata wanyama hawana

Serikali: Ndoa za jinsia moja hata wanyama hawana

Msimamo wa nchi tofauti na uliopo kwenye katiba?? Au mnataka kusikia na mtafurahi tu mkisikia amerejea kifungo hicho cha katiba?
Dr. Mpango kama kiongozi wa nchi anapaswa kutoa tamko ambalo litataeleza msimamo wa nchi na siyo kuishia kutoa ushauri
 
Wewe ndio umeiua kabisa hoja yake!
Sasa kama wanyama wanaweza kujamiiana watoto kwa wazazi wao au ndugu na ndugu kuna haja gani ya kutolea mfano wa wanyama kupinga ushoga?!
Maana yangu na yake ni kwamba..

Sisi wanadam tumepewa ufaham wa kujua hiki tunachofanya ni kibaya.

Wanyama hawana hiyo, ndio maana wanakulana mtoto Mbuzi anamla Mamabuzi, Baba Mbuzi anamla mtoto.

Hivo Kwa hoja ya mchangiaji kua wapo wanyama wanaume Kwa wanaume wanakulana, bado tunarudi palepale kwamba wanyama walinyimwa ufahamu.
 
Sasa Mpango anapsema "hata wanyama hawafanyi hivi" anamaanisha nini??
Maana yangu na yake ni kwamba..

Sisi wanadam tumepewa ufaham wa kujua hiki tunachofanya ni kibaya.

Wanyama hawana hiyo, ndio maana wanakulana mtoto Mbuzi anamla Mamabuzi, Baba Mbuzi anamla mtoto.

Hivo Kwa hoja ya mchangiaji kua wapo wanyama wanaume Kwa wanaume wanakulana, bado tunarudi palepale kwamba wanyama walinyimwa ufahamu.
 
Dr. Mpango kama kiongozi wa nchi anapaswa kutoa tamko ambalo litataeleza msimamo wa nchi na siyo kuishia kutoa ushauri
Haya mambo yanahitaji ushirikiano wa viwango vya juu sana miongoni mwa wana jamii. Hiki ndicho VP kakiomba.
Lkn pia km kiongozi katumia lugha rafiki kukemea huozo huo ("hata wanyama hawafanyi") na uwasilishaji wa ujumbe wake umeendana na mahala alipokuwa ijapo inaeleweka wazi kuwa NDOA ZA JINSIA MOJA Tz ni marufuku km ambavyo mpango kasisitiza. Mnao mpinga mnatetea upande gani?
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Wazazi na Walezi kuwalea Watoto na Vijana kwa kuzingatia maadili ya kitanzania pamoja na kuongeza umakini katika maudhui yanayooneshwa katika Televisheni.

Dr. Mpango ameyasema haya wakati akiongea na Waumini wa Kijiji cha Kasumo Mkoani Kigoma baada ya kushiriki Ibada ya kawaida ya katikati ya wiki katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Amani Kijiji hapo ambapo
amesema kumekuwepo na mmomonyoko wa maadili ikiwemo ndoa za jinsia moja ambazo hazipo hata kwa Wanyama hivyo Wazazi waangalie Watoto na Vijana wanaangalia nini ili kuondokana na kuwa na Taifa la ajabu.

“Hili ni gumu kweli, maadili ya Nchi yetu yameporomoka sana, yaani na mengine hata kuyasema ni ngumu, ndoa za Wanaume wawili?, ndoa za Wanawake wawili? mliziona wapi? hata Wanyama hawafanyi hivi”

Kwa upande mwingine, Dr. Mpango amewaasa Wananchi wa Kasumo na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla kutoa ushirikiano wakati huu ambapo Serikali inafanya ujenzi wa miundombinu ya Barabara katika Mkoa huo ambao ni nyenzo muhimu kwa biashara na urahisi wa kufikia huduma za jamii kama vile Hospitali na Shule na kuzingatia pia kuwapa Wawekezaji ushirikiano ikiwemo kuzingatia bei halisi za ardhi katika maeneo yao ili kutowapoteza.
Kama Mungu Muumba wa mwanadamu aliyaona kuwa ni nachukizo mbele ya macho yake, hata akafikia kiwango cha kukosa subira na kuiangamiza kwa moto miji ya Sodoma na Gomora, sasa binadamu ni nani hata ahalalishe kufuru hiyo kuu!?

Kama Neno la Mungu limehalamisha jambo hilo, basi azimio la UN ambalo linatambua haki za LGBTIQA ni batili, hata kama nchi yetu na nchi nyingine wanachama waliridhia. Kaa chonjo kwani hizi ni nyakati za mwisho wa dunia.
 
Dr. Mpango kama kiongozi wa nchi anapaswa kutoa tamko ambalo litataeleza msimamo wa nchi na siyo kuishia kutoa ushauri
Kwa nchi yetu ambayo asilimia kubwa watu wanaishi vijijini na wanaishi kiukoo hizi habari za ushoga ni kuwaumiza masikio bure. Habari hizi waambiwe wamjini wanaopenda uzungu
 
Serikali imejipanga vipi kukomesha Ushoga na Usagaji huko magerezani? Huko nako ndio chanzo cha Ushoga,Mtu alishakuwa na basha/Shoga wake huko gerezani akitoka anaanza kutafuta mabasha/Mashoga mitaani,Zifungwe sheria basi mfungwa akipatikana na kosa la ushoga apelekwe tena mahakamani na kusomewa mashtaka.
 
Yeye ni mkatoliki na papa mkuu wa kanisa anasema mapenzi ya jinsia moja ni haki
Tumsililize yupi?
Yeye Mpango kama nia yake ni ya dhati na sii unafiki kwa kuwa yeye ni kiongozi mwandamizi wa serikali ya jamhuri ya Tanzania apeleke muswaada bungeni wa kupinga ushoga kama Museni wa ugandaView attachment 2562995
Huo ni uwongo. Papa hajawahi kutoa kauli ya namna hiyo. Waliobadilisha kauli ya Papa, bila shaka wana ajenda yao.

Papa alisema:

"Homosexuality is a sin but not a crime"

Kwa tafsiri rahisi:

"Ushoga ni dhambi ila siyo uovu"

Francis said there needed to be a distinction between sin and a crime when it came to homosexuality. The Catholic Church considers homosexual acts “intrinsically disordered” and a sin, but believes that people in the L.G.B.T.Q. community should be welcomed with respect and sensitivity.

Na alisistiza kuwa Kanisa kamwe halitaweza kubariki dhambi. Lakini akasema kuwa Kanisa lisiwatenge mashoga. Na hiyo inaeleweka. Kanisa halijitengi na wadhambi, maana Kristo mwenyewe alisema kuwa, "aliye mzima hahitaji tabibu, bali aliye mgonjwa"
 
Hakunaga maadili ya watanzania wala utamaduni wa watanzania. Tanzania ina makabila.zaidi ya 100 na watu hufuata utamaduni wa makabila yao. Wale ambao hawafuati utamaduni wa makabila yao hawana utamaduni kwa sababu Tanzania kama nchi haijawahi kuwa na mila, desturi na utamaduni wake
 
Wanasiasa huwa wanapenda kuongea maneno makubwa makubwa yenye ombwe
Hakunaga maadili ya watanzania wala utamaduni wa watanzania. Tanzania ina makabila.zaidi ya 100 na watu hufuata utamaduni wa makabila yao. Wale ambao hawafuati utamaduni wa makabila yao hawana utamaduni kwa sababu Tanzania kama nchi haijawahi kuwa na mila, desturi na utamaduni wake
 
Serikali isipepese macho na unafiki. Isiseme Kwa mafumbo na hitaji la maudhui. Serikali kupitia kunywa Cha Samia aseme mchana kweupe hadharani, "Tanzania haturuhusu ndoa ya jinsia moja" Ili Dunia ijue sio Sanaa za kina Mpango. Tuwe kama Museveni.
 
Huo ni uwongo. Papa hajawahi kutoa kauli ya namna hiyo. Waliobadilisha kauli ya Papa, bila shaka wana ajenda yao.

Papa alisema:

"Homosexuality is a sin but not a crime"

Kwa tafsiri rahisi:

"Ushoga ni dhambi ila siyo uovu"

Francis said there needed to be a distinction between sin and a crime when it came to homosexuality. The Catholic Church considers homosexual acts “intrinsically disordered” and a sin, but believes that people in the L.G.B.T.Q. community should be welcomed with respect and sensitivity.

Na alisistiza kuwa Kanisa kamwe halitaweza kubariki dhambi. Lakini akasema kuwa Kanisa lisiwatenge mashoga. Na hiyo inaeleweka. Kanisa halijitengi na wadhambi, maana Kristo mwenyewe alisema kuwa, "aliye mzima hahitaji tabibu, bali aliye mgonjwa"
Kama anamaanisha USHOGA ni DHAMBI, iweje afungishe NDOA na Kuhalalisha dhambi?

He is a Devil in human body.
 
Anaongea hivyo ktk vijiji visivyokuw na mbele wala nyuma Media coverage 1.0℅ aje aongee Dodoma au DSM Temeke pale
 
Wewe ndio umeiua kabisa hoja yake!
Sasa kama wanyama wanaweza kujamiiana watoto kwa wazazi wao au ndugu na ndugu kuna haja gani ya kutolea mfano wa wanyama kupinga ushoga?!
Figures of speech.....
"Hata wanyama hawafanyi hivyo"......
Unaweza ukashare nasi baadhi ya hizo " tafiti za kisayansi" ? Ili tujifunze pia....
 
Back
Top Bottom