Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Yamenikuta najuta kuwa na kibanda, wiki iliyopita mvua ilinyesha usiku na kubomoa choo cha nyumba yangu cha mtindo wa pasipoti sasa hivi, asubuhi kulipokucha nikaenda kununua simenti na matofali na kuamua kukijenga upya, hamadi serikali ya mtaa kumbe nao wanajua watatupata, wakanidaka.
Baada ya kunifikisha ofisini kwa nikidhani naenda kupewa msaada nikaambiwa ninajenga bila kibali!
Nikajiuliza hiyo mvua imebomoa bila amri ya mahakama mimi naamniwa adhabu yangu nilipe shilingi laki mbili! Sijui nitazitoa wapi huku nikiwaza kwanini wao wasinipe msaada huo lakini jamaa hawna utani nilipe hizo hela.
Hili limenikuta lakini je, ni watanzania wote waliobomokewa na nyumba zao watalipa pesa za kibali cha ujenzi au bahati yangu mimi kuiingizia mapato serikali wakati huu wa mvua?
Nimesimamisha ujenzi na sina choo inabidi nitumie cha jirani wakati wa mchana na usiku kuna lile kopo letu la jadi maarufu kwa jina la sululu.