Hismastersvoice using'ang'ane kusema mvua imekuharibia ndio wakusamehe, unachotakiwa kuhoji ni uhalali wa tozo za hivyo vibari na kukemea mambo ya tozo kwa kila kitu katika nchi yetu. Haya matozo yanafanya miji yetu iendelee kuwa kama mapango ya walanguzi, miji nyumba zimepauka rangi au nyumba fupi, hali ya uchumi kwasasa sio nzuri kabisa wachache wanaweza mudu gharama za ujenzi au ukarabati kwa mara moja sasa hawa/ambao hatuwezi ni lazima tujichange na tufanye kwa awamu, sasa kwa kila awamu tutakuwa tunalipia hizo tozo?.
Tunaponunua vifaa vya ujenzi wanachukua kodi, kwenye biashara wanachukua kodi na ushuru wa huduma tena pesa nyingi 0.3% ya turnover lakini hizo tozo zote hakuna cha maana wanachofanya kwamba wanajenga barabara zetu mitaani hapana, wanaboresha hali ya upatikanaji wa umeme hapana, kwamba wanawezesha wananchi kiuchumi hapana, kwamba wana boresha huduma za afya, maji na elimu hapana matokeo yake wanazidi kukukopa sana nje ya nchi na deni la taifa linazidi kupaa, wananunua ma V8 new model kila mwaka, wana neemeshana wao kwa wao na bado wanataka waendele kuchukua tozo kila mahali.
Ni wakati sasa na muhimu sana kuwakemea hawa viongozi kwasababu hawana tofauti na wanyang'anyi.
Tozo zinaangamiza hii nchi wala hazijengi kwasababu wakusanya tozo hawajui kuzitumia. Kuna rule ya 20/80% ni muhimu serikali iitumie.