Serikali pangisheni yaliyokuwa majengo ya Wizara na Taasisi mbalimbali DSM vijana tupate ofisi na ninyi mpate kodi

Lowassa aliwahi kusema tatizo la serikali ya wabongo hamnaga mwenye maamuzi wala vision, nakumbuka walivyoua Embassy hotel kifala tu hadi likawa gofu, na hizo ofisi ndicho kitakachofuata
Umenikumbusha mbali sana mkuu
Embassy Hotel nililala mwaka 1987 wakati huo ilikuwa na hadhi ya kimataifa
 
Mkuu hayo ni majengo ya watu binafsi, yanahudumiwa kwa usafi - hayachakai na hoja yangu sio kuwa, Posta kuna uhaba wa majengo ya kupanga. Mimi nazungumzia majengo ya serikali yaliyojengwa kwa kodi za wananchi. Yanavyobaki wazi ni hasara kwa wananchi, ni kama vile kodi yetu inakua imetupwa tu, jengo linachakaa na halizalishi chochote. Ndio natoa mbadala kuwa serikali wayapangishe ili yasaidie wananchi na pia yaokolewe yasiendelee kuchakaa.
Kwani aliyekwambia hayo majengo ya serikali hayapangishwi nani.
Mengi yapo yanapangishwa mengine wamekidishiwa banks and offices.
 
Isiwe ligi mkuu, nafikiri hatuelewani. Usichanganye majengo ya NHC, ya TBA na majengo ya wizara za serikali. Hayo ni NHC na TBA ni ya serikali na yanapangishwa, ila mimi nimezungumza majengo yaliyokuwa yakitumiwa na wizara mbalimbali na sasa yapo wazi.

Hakuna jengo la wizara au taasisi lililopangishwa benki bali yapo baadhi walibadilisha taasisi, mfano jengo ilipokua wizara ya elimu kwa sasa ni tume ya vyuo vikuu (TCU), jengo lililokuwa wizara ya mambo ya nje sasa hivi ni mahakama kuu ya Tanzania kitengo cha ardhi.

Mengi yaliyobaki yapo wazi hayatumiki..hoja ni kuwa yatumike, na kutumika ni pamoja na kupangishwa
 
Yataje hayo majengo ambayo yako wazi tuyafahamu
 
Kwa Kodi ya kiasi gani, na kwa kufanya shughuli gani na wateja wa sehemu gani ?

Au wauze mitumba kwenye vyoo na kuendesha bodaboda kwenye corridor
 
Ni zaidi ya miaka 5 sasa toka Rais JPM alipoagiza Wizara zote za Serikali kuhamia jijini Dodoma yalipo makao makuu ya nchi. Agizo la rais ni sheria, hibyo lilitekelezwa kwa ukamilifu na sasa Wizara karibu zote zimehamia Dodoma ambapo zina majengo katika mji wa serikali Mtumba.

Kwa miaka yote hiyo zaidi ya 5, majengo yaliyokuwa yakitumiwa na wizara hizo jijini Dar es Salaam yamebaki wazi, hayatumiki na yamekuwa kama magofu. Maana nyumba isiyotumika ni lazima ichakae.

Sasa basi ninaona ni muda muafaka, serikali ipangishe majengo haya kwa bei nafuu ili vijana wengi wanaojiajiri wapate ofisi wajiongezee thamani kwa kazi zao na pia wajipatie kipato.

Tunajua kuwa ofisi ni anuani, mteja anakuwa na amani akifanya kazi na mtu ambaye anakua na ofisi. Wekeni viwango hata vya Tshs. 10,000/= kwa skwea mita, mtakua mmetatua tatizo la ajira, mtakua mmeinua vijana na wakati huohuo mtaongeza chanzo cha mapato (kodi).

Kuna majengo kama lile lililokuwa likitumiwa na Wizara ya Katiba na Sheria lenye takribani ghorofa 10 hali yake kwa sasa inasikitisha, vioo vinavunjika, madirisha hayafungi ilhali lilikuwa ni jengo zima kabisa.

Pangisheni lile. Na pale ofisi za Takwimu yalipokua makao makuu ya NIDA kuna jengo limechoka vibaya kwa sasa lakini zamani lilikua vyema kabisa, pangisheni. Hata pale ilipokuwa wizara ya Kazi, jengo limebaki tu. Fanyeni hivyo kwa majengo yote yaliyobaki wazi na yanaendelea kuchakaa.

Tunaomba serikali mlifanyie kazi hili, kama mtakosa nguvu kazi ya kusimamia, niteueni mimi nifanye kazi hiyo, majengo yarudi kwenye ubora na vijana wapate ofisi.

Mhe. Dkt. Gwajima D wizara yako inahusika kabisa kwa upande wa maendeleo ya vijana, naomba ufikishe hili kwenye vikao vya baraza la mawaziri. Ahsante

Ubepari ni ushetani .

Hakuna bepari anayewaza mambo mbali na familia yake na maisha yake binafsi .
Ukiwauliza wanasema wanatafuta mwekezaji . Baadae wanajiuzia wenyewe kwa bei ya hasara halafu watoto wa maskini wanabaki kuendesha bodaboda .

Hii nchi bila kufanya maamuzi magumu vijana zaidi ya milioni 12 watabaki kama machawa na waandamanaji wasio na ajira maalumu. Wachache kama wasanii na Makada wa CCM na Chagadema wanatumika kuwaaminisha vijana zaidi ya mil 12 kuwa wawekezaji watawapa ajira lakini wawekezaji wenyewe ni wachina wanaouza mbao na mkonge badala ya kazi hizo kufanywa na vijana wa kitanzania .

Kuna mtu namsubiri ashinde uchaguzi nimpe mipango na mikakati 10 ya kumaliza tatizo la ajira na kuinua uchumi wa Watanganyika ndani ya miaka 10.

Huu ubepari wa kuuza nchi haufai kamwe ni udalali mbaya sana utakaowaacha vijana wengi kujiingiza kwanye uhalifu mkubwa kama ilivyo sasa mpaka wanawake wanaiba watoto na kuua kwa imani za kishirikina ili kutafuta pesa . Nyumba za ibada kila kona kuanzia misikiti na mazinagogi ya wakristo bandia . Wanasiasa hawajali mana wao wamejilimbikizia mali na wenza wao na watoto wao.

Bado tu CCM ishinde na Mbowe akiwa Mwenyekiti wa CHADEMA wapeleke mswada Bungeni wa kuwalipa watoto wa viongozi mishahara kama kifuta machozi kutokana na kuishi katika mazingira magumu ya kudhalilishwa na kuchafuliwa .
Huo ndio ubepari .
Ubepari haujali kuwa kuna watu wanakufa kwa kukosa huduma za figo japo mashinde zimenunuliwa kwa kodi za wananchi . Hawajali ,wanachoangalia ni madaraka kama Mbowe na Samia . Huko mitaani walinzi wa amani hawana magari hata Suzuki za kuzunguka mijini na vijijini kwenye ulinzi lakini mabosi wanaokaa ofisini wanatembelea magari ya mil. 400 na mwakani yakitoka yanayopaa anagani watayapaki hayo ya sasa yaliyotengenezwa 2024 watatafuta mengine kwa bil.Moja alimradi serikali utenge mabilioni ya kununulia mabosi magari waishi maisha ya anasa kama matajiri binafsi wakati wanalia ofisi za umma na kuhakikisha jamii inapata huduma bora za Afya ,elimu,maji na umeme
 
Mkuu, yaani umeandika kizalendo sana, kwa dhamira safi kabisa kila atayesoma, ikiwa ni pamoja na mabepari wenyewe wataona ukweli huo uliouzungumza.

Hawa watu ni wabinafsi sana. Mali za serikali zinachezewa sana
 
Ni zaidi ya miaka 5 sasa toka Rais JPM alipoagiza Wizara zote za Serikali kuhamia jijini Dodoma yalipo makao makuu ya nchi. Agizo la rais ni sheria, hibyo lilitekelezwa kwa ukamilifu na sasa Wizara karibu zote zimehamia Dodoma ambapo zina majengo katika mji wa serikali Mtumba.

Kwa miaka yote hiyo zaidi ya 5, majengo yaliyokuwa yakitumiwa na wizara hizo jijini Dar es Salaam yamebaki wazi, hayatumiki na yamekuwa kama magofu. Maana nyumba isiyotumika ni lazima ichakae.

Sasa basi ninaona ni muda muafaka, serikali ipangishe majengo haya kwa bei nafuu ili vijana wengi wanaojiajiri wapate ofisi wajiongezee thamani kwa kazi zao na pia wajipatie kipato.

Tunajua kuwa ofisi ni anuani, mteja anakuwa na amani akifanya kazi na mtu ambaye anakua na ofisi. Wekeni viwango hata vya Tshs. 10,000/= kwa skwea mita, mtakua mmetatua tatizo la ajira, mtakua mmeinua vijana na wakati huohuo mtaongeza chanzo cha mapato (kodi).

Kuna majengo kama lile lililokuwa likitumiwa na Wizara ya Katiba na Sheria lenye takribani ghorofa 10 hali yake kwa sasa inasikitisha, vioo vinavunjika, madirisha hayafungi ilhali lilikuwa ni jengo zima kabisa.

Pangisheni lile. Na pale ofisi za Takwimu yalipokua makao makuu ya NIDA kuna jengo limechoka vibaya kwa sasa lakini zamani lilikua vyema kabisa, pangisheni. Hata pale ilipokuwa wizara ya Kazi, jengo limebaki tu. Fanyeni hivyo kwa majengo yote yaliyobaki wazi na yanaendelea kuchakaa.

Tunaomba serikali mlifanyie kazi hili, kama mtakosa nguvu kazi ya kusimamia, niteueni mimi nifanye kazi hiyo, majengo yarudi kwenye ubora na vijana wapate ofisi.

Mhe. Dkt. Gwajima D wizara yako inahusika kabisa kwa upande wa maendeleo ya vijana, naomba ufikishe hili kwenye vikao vya baraza la mawaziri. Ahsante

Hata wangewapa bure tu ingetosha
 
Na hapo ndio kipimo cha akili za wanalumumba unapoziona.
 
Back
Top Bottom