Serikali shirikisheni kampuni binafsi za ukaguzi za "Big Four" kudhibiti ukwepaji kodi

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Mnachotakiwa kufanya ni kila mwaka kuwapa kandarasi mmojawapo Big four wa audit ambao ni KPMG, E&Y, PWC au Delloite wafanye ukaguzi wa nje "External Audit" kwa wafanyabiashara wakubwa 1000 na wa wakati 1000 ambao mahesabu yao ya kodi tayari yameshapitishwa na TRA.

Hao wafanyabiashara wakubwa na wa kati wanakuwa wanachaguliwa kupitia bahati nasibu "Randomly" kila mwaka na kila mwaka mnakuwa mnabadilisha kampuni ya nje ya ukaguzi kati ya hizo big four.
 
Hao Big4 watakuwa wanafanya tax audit ipi ambayo TRA haifanyi? Kumbuka auditors ni wabongo tu ambaye akipata fursa anapiga. Kwa jinsi kodi yetu inavyoliwa na CCM hata mimi mkinipa nitapiga tu. Tunakazania kodi tu halafu matumizi yake hatuna time nayo. Mzee wa skafu anatumia kununua timu tu, anabadili timu kama shati
 
Hiyo hela ya Kuwalipa hizo kampuni za Mabilionea, ni sawa na hela inayokwepwa na Wafanyabiashara mafisadi wa Tanzania. Watatuingiza mkenge tu-Wanaupendeleo

Hii ya kwamba suluhisho la matatizo yetu yatatatuliwa na "Wazungu" tuondekane nayo kabisa-hapendwi mtu. Tuachane na hizi fikra.

Hata hivyo kama wao ndio wameweza kuwa suluhisho la kukusanya kodi zao huko, kwanini Wakuu wa nchi kubwa za Kiuchumi, bado wanataka wafanyabiashara wakubwa watozwe 15% ya mapato yao?

Sio, kila kitu Wazungu tu.
 
Cha kufanya Serikali iimarishe mifumo iliyonayo ya ukusaji mapato.

Iondoe watu na ijenge mifumo imara ya ufuatiliaji mapato.

Iwekeze kwenye mifumo ya udhibiti iliyo thabiti.

Iwe na mfumo wa kumfatilia Kila mfanyabiashara kutoka ofisini.
 
Hao Big4 watakuwa wanafanya tax audit ipi ambayo TRA haifanyi? Kumbuka auditors ni wabongo tu ambaye akipata fursa anapiga. Kwa jinsi kodi yetu inavyoliwa na CCM hata mimi mkinipa nitapiga tu. Tunakazania kodi tu halafu matumizi yake hatuna time nayo. Mzee wa skafu anatumia kununua timu tu, anabadili timu kama shati
Big4 ni kampuni za kimataifa na wanakuwa regulated kwenye nchi zenye sheria kali za kodi. Sio rahisi kukubali kuhongwa kuharibu hadhi yao kirahisi.
 
Bora mama angekuwa serious na hao ambao wanaiba hela, wanaweka matumizi yasiyo ya lazima na huku mama mjamzito huko Kijijini anakosa huduma nzuri za kujifungulia. Yaani veiti inunuliwe Ila mwanafunzi akae chini pia mwalimu wa hesabu akosekane ama awepo mmoja shule nzima ya watt alfu mbili. Ama kweli jambazi anao unafuuu kuliko mwanasiasa. Unaofurahia hela za dhuluma, wizi , miktaba mibovu. Yaani hata ukiwa unakufa unajua kabisa una amani kuwa uliwaibia watanzania. Mbona dp world mwanzoni mlitaka wasilipe Kodi so nani atailipa na huku bado kwenye miamala mnakamua mnasema kuwa watazoea
 
Hiyo hela ya Kuwalipa hizo kampuni za Mabilionea, ni sawa na hela inayokwepwa na Wafanyabiashara mafisadi wa Tanzania. Watatuingiza mkenge tu-Wanaupendeleo

Hii ya kwamba suluhisho la matatizo yetu yatatatuliwa na "Wazungu" tuondekane nayo kabisa-hapendwi mtu. Tuachane na hizi fikra.

Hata hivyo kama wao ndio wameweza kuwa suluhisho la kukusanya kodi zao huko, kwanini Wakuu wa nchi kubwa za Kiuchumi, bado wanataka wafanyabiashara wakubwa watozwe 15% ya mapato yao?

Sio, kila kitu Wazungu tu.
Tutafute basi makampuni ya ukaguzi ya Waarabu au Wachina kama tunavyowapa kandarasi za kujenga barabara na kuendesha bandari na mwendokasi.
 
Mnachotakiwa kufanya ni kila mwaka kuwapa kandarasi mmojawapo Big four wa audit ambao ni KPMG, E&Y, PWC au Delloite wafanye ukaguzi wa nje "External Audit" kwa wafanyabiashara wakubwa 1000 na wa wakati 1000 ambao mahesabu yao ya kodi tayari yameshapitishwa na TRA.

Hao wafanyabiashara wakubwa na wa kati wanakuwa wanachaguliwa kupitia bahati nasibu "Randomly" kila mwaka na kila mwaka mnakuwa mnabadilisha kampuni ya nje ya ukaguzi kati ya hizo big four.
wasiishie tu kwenye kodi na ukaguzi wa matumizi ya pesa kwenye mashirika ya serikali pia uhusishe external international auditors.

NB: Kwa heshima na nia njema, naomba upitie wasifu wangu na unisaidia ktk hitaji langu la ajira.
Mimi ni kijana mchapakazi na mwaminifu, miaka 32, makazi yangu Dar es Salaam. Nina shahada ya utawala, na uzoefu wa miaka 8 katika usimamizi wa miradi, utafiti, data entry, na usimamizi wa mitandao ya kijamii, pia nina ujuzi na uzoefu kwenye customer care, masoko, na mauzo. Naweza kusaidia katika kuandika maandiko mbalimbali ya kiofisi, miradi, tafsiri, na kubuni nakutengeneza tovuti kwa ubora.
Ninaomba fursa ya ajira na nipo tayari kufanya kazi mara moja mahali popote nchini.
Nipigie/text kwa 0769 055050. Asante!
 
Inabidi tutafute definition ya wakwepa kodi
Nina hakika kodi zikikusanywa kwa usahihi na zikatumika kwa usahihi walau 85% ndio itakuwa mwisho wa CCM.

Imagine kila baada ya miaka 5 wananchi wanaenda kudanganywa tumewaletea maji hapa , umeme , tumejenga madarasa na wanapiga makofi kushangilia bila kujua sio hisani bali ndio matumizi ya kodi zao.

Angalia msafara wa Makonda akiwa mwenezi magari mpaka ya serikali yamo kwenye msafara who should be held accountable for such misappropriation??
 
Tutafute basi makampuni ya ukaguzi ya Waarabu au Wachina kama tunavyowapa kandarasi za kujenga barabara na kuendesha bandari na mwendokasi.
Hiyo sio hoja yangu. Usikwazike.

Fees zitakazo lipwa kufanya ukaguzi huo, zitakuwa ni sawa na pato linalopotea kwa ukwepaji wa Kodi.

Tuondokane na Fikra za Ukuu wa Wazungu.

Kwa yeyote anayetaka kuelewa haya Makampuni yanavyofanya kazi, watafute Jinsi sakata lile Evergrande group, ilivyokuwa. Hawa wanalala na Matajiri.
 
Mnachotakiwa kufanya ni kila mwaka kuwapa kandarasi mmojawapo Big four wa audit ambao ni KPMG, E&Y, PWC au Delloite wafanye ukaguzi wa nje "External Audit" kwa wafanyabiashara wakubwa 1000 na wa wakati 1000 ambao mahesabu yao ya kodi tayari yameshapitishwa na TRA.

Hao wafanyabiashara wakubwa na wa kati wanakuwa wanachaguliwa kupitia bahati nasibu "Randomly" kila mwaka na kila mwaka mnakuwa mnabadilisha kampuni ya nje ya ukaguzi kati ya hizo big four.
Acha ulevi Wafanyabiashara Wakubwa Ndio wamo serikalini humo humo

Unawaza kizamani sana
 
Back
Top Bottom