Siyo kweli. Hayo makampuni yanajulikana kwa Rushwa. Itoshe hamtaki Tanzania iwe na sheria kali. Kipindi cha nyuma tuliona Jinsi hizihizi sheria zetu zilivyosimamiwa kwa ukamilifu, ulisikia urahisi wa kuhongwa au kutoa hongwa?
Hizo kampuni Zimeshiriki katika sakata za Rushwa na ubadirifu, na hadhi zao zinalindwa kwa kutumia pesa na influences walizonazo kwa watu wanao wachangia kwenye uchaguzi zao, Wanasiasa. Usiwaoshe. Umetumwa?
Ujiulize tu, ikiwa nchi hizo zina sheria kali za Kodi inakuwaje hayo makampuni yanawasaidia Mabilionea kukwepa kodi? Hizo sheria zinakuwaga wapi wakiwa wanafanya hayo madudu yao?
Tusidanganyane, Sheria zetu, karibia nyingi za Fedha ni sheria hizo hizo za Ulaya na Marekani. Na iwa msingi huo , sheria zetu nazo ni "kali" sema hazifuatwi kwa Ukamilifu.
Na niongezee tu,Tanzania imekuwa ikifuata standards za Kihasibu za Nje, hata hivi majuzi CAG amegusia kuhusu kufuata utaratibu huo, point ni kwamba sheria zipo, kanuni na miongozo ipo, ila Rushwa imetamalaki.
Tunakukumbuka Comrade.