Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
- Thread starter
- #41
Unafaa kivipi? Ziliungana nchi mbili - Zanzibar na Tanganyika. Halafu zikazaa Tanzania. Kinachoshangaza ghafla Tanganyika ikawa Tanzania Bara lakini Zanzibar ikabaki Zanzibar. Kwanini haikuwa Tanzania Visiwani ili jina Zanzibar nalo life? Sasa ama tuwe na Tanzania Bara na Visiwani au Tanganyika na Zanzibar halafu JMT.
Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
Kwahiyo wewe shida yako ni jina tu? Tanganyika imepoteza nini embu nikuulize? Logically muungano wa serikali tatu hauwezekani pasipo muungano kuvunjika. Hatuwezi kuwa na sovereign state ya tanganyika pasipo kuleta mgawanyiko hivi vitu viko in perfect harmony. Hauwezi kuiondoa zanzibar kwenye muungano Tanganyika ikabaki salama na kinyume chake ni sahihi. Hivi vitu viko deep sana mpaka utafakari kwa kina ndio utakapo pata ukweli. Mwalimu nyerere alikuwa yuko sahihi. Na kama tusipo msikiliza tutapata tabu. Believe me you must have spiritual insight to understand this. Lakini sio wajibu wangu kukuaminisha; wajibu wangu kusema ukweli na nimeusema kama mtauchukua au mtaukataa ni juu yenu..