GSM sasa tena kwa kufanya Kimya Kimya / kwa Siri wameamua Kuvidhamini Vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu yaani NBC PREMIER LEAGUE ili zikiwa zinacheza na Yanga SC yao ipate Unafuu wa Ushindi ila Vilabu hivyo vikiwa vinacheza na Wapinzani wao wakubwa Simba SC viwe vinaikazia kwa ama Kuifunga au hata tu kutoka nayo Sare.
Ama kweli Aden Rage hakukosea aliposema mashabiki wa
Makolo ni Mbumbumbu:-
GSM hawajaanza kudhamini hivyo vilabu leo, sasa hiyo fair competition imeanza sasa?
Halafu eti wamefanya udhamini kwa siri...
Ingekuwa siri, media zingeripoti?!
Kusoma hujui, ina maana hatapicha za logo za GSM huzioni kwenye jezi?!
Unadhamini vipi kwa siri halafu hapo hapo unaweka logo yakoopenly ?
Btw, hivi unatakiwa kukumbushwa kwamba pamoja na udhamini huo wa GSM, bado Yanga msimu uliopita walipigwa na Coastal, tena kwenye mechi muhimu kweli kweli?!
Au wewe ni mfuatiliaji wa soka la Instagram?
Kinachonisikitisha zaidi Uhuni na Upumbavu huu usio na Haki katika Ushindani Michezoni unafanywa na GSM halafu Serikali kupitia Wizara ya Michezo imekaa Kimya, TFF na Bodi ya Ligi wamekaa Kimya na Wahusika Wakuu wa Kupambana na Kuzuia Rushwa na Dalili zake zote TAKUKURU wamekaa Kimya.
Hao walioko serikalini sio mbumbumbu kama mashabiki wa Makolo!
Akitokea tu Mtu Mmoja au Klabu Moja ikajipanga vyema kwa Sheria na Ushahidi wa Kutosha juu ya Uhuni na Upumbavu huu wa GSM katika Kuvidhamini Vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu kwa nia ya kupata Unafuu ikicheza nazo na akaenda Kushtaki FIFA kuna uwezekano mkubwa NBC Premier League ikaingia matatizoni, Klabu Moja kubwa Kufungiwa, huyu Mdhamini wao Mkuu GSM Kushtakiwa na hata Mpira wa Tanzania Kuharibika rasmi.
Povu na matusi yote ya nini, Kolo?!
Azam Media wana Content Contract na Yanga...
Azam FC na Azam Media ni baba mmoja, mama mmoja...
Nini Kolo kinakufanya uone GSM kudhamini Yanga na Coastal ni Upumbavu unaofumbiwa macho lakini unaona sawa kwa Azam kufanya kitu kile kile?! Au kwa sababu na Makolo mnanufaika na Azam?
Hakuna Mfanyabiashara Mstaarabu na Muungwana Tanzania hii kama Mzee Bakhressa na Kampuni yake ya Azam. Na hakuna pia Kampuni ambayo ni Tajiri Tanzania nzima kama ya Azam.
Azam Wana Timu yao ya Azam FC ila kwa miaka Saba sasa wanapambana Kuwa Mabingwa ila bado hawajafanikiwa. Lakini sijawahi ama Kuona au Kusikia mahala popote pale Azam wakizihonga Timu mbalimbali za Ligi Kuu ya Tanzania ili ziiachie na iwe Bingwa japo ina uwezo wa Kifedha maradufu ya hawa Matapeli wa GSM ila wameamua Kupambana kwa Kucheza tu Uwanjani.
Kweli we Kolo...
Kwahiyo Azam Media iliyoingia mkataba wa content na Yanga, hapo Yanga wamehongwa?!
Kama GSM kweli walikuwa na nia ya Kuvidhamini Vilabu vya Ligi Kuu ya Tanzania NBC PREMIER LEAGUE walikuwa wapi Kujitokeza pale TFF na Bodi ya Ligi walipokuwa wanatafuta Wadhamini?
Umeanza lini kufuatilia soka kiasi kwamba unashindwa kutofautisha kati ya mdhamini wa ligi na mdhamini wa vilabu?
Hivi leo hii Mo Dewji na Kampuni yake / Kampuni zake angeamua nae Kufanya Uhuni na Upumbavu huu usio wa Haki unaofanywa na GSM kwa Kuvidhamini Vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu tena Kisirisiri / Kimya Kimya na kuwaambia wawe wanaikamia tu Yanga SC ila zikiwa zinacheza na Simba SC wawe wanailegezea FAIR COMPETITION ingekuwepo?
Ndo tatizo la kuwa na Think Tank Shaffii Dauda
Sasa kama unatamba kuwa na Kikosi kizuri na unasema msimu huu Kombe ni lako kwa Soka Kubwa unalocheza kwanini unahangaika Kuvidhamini Vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu kisha unavipa Ahadi ya Tsh Milioni 15 vikiishinda Simba SC na Tsh Milioni 10 vikitoka nayo Sare mpaka unasababisha Wachezaji wa hizo Timu Kuikamia Simba SC, Kuwaumiza kwa Makusudi Wachezaji wake na pale Wakifungwa baada ya Filimbi ya mwisho badala ya kuondoka Uwanjani wanaanza Kuangua Vilio, Kugombana na Kulaumiana mno?
Hapa ndo umethibitisha ile kauli ya Aden Rage...
Dhambi ni kuhonga wachezaji au kuhonga waamuzi ili wahujumu mchezo lakini hakuna dhambi yoyote kuwapa motisha wachezaji...
Btw, mechi mbili mlipata goli dakika ya 99 kwa sababu wachezaji wa timu pinzani waliahidiwa pesa na GSM; vipi kuhusu zile 3 mlizotandikwa pale Mkapa na timu ambayo nchini kwao ligi imemesimama kwa zaidi ya miezi 18?
Hivi kule Morocco ambako mliweka kambi, mkafikia kucheza hadi na timu ya daraja la 3; mlishinda mechi ngapi kule?
Msimu uliopita mlishinda mechi ngapi ambazo Chama hakuwepo uwanjani?
GSM wameshaiharibu Ligi Kuu ya NBC.
Ina maana GSM ndo anawafanya muwe mnashinda kwa mbinde, au?
Ni GSM nde anawafanya mfungaji wenu pekee mnayemtegemea muwe mnamuingiza dakika 30 za mwisho, au?
Au ndo nyie ambae Think Tank wenu ni Shaffi Dauda?!
Nimekuwekea hapo YouTube link inayoonesha GSM amekuwa akividhamini hivyo vilabu tangu msimu uliopita, lakini kwavile watu wenyewe nyinyi ni "hoya hoyaa" ndo mnazadhani huo udhamini umeanza mwaka huu, huku bila aibu ukisema eti kawadhamini kisirisiri!!