Blender
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 4,870
- 8,035
Kitendo cha kuvibonyeza, kuvikandamiza vichwa vya watoto wachanga ili kuzuia kichogo, bila kutumia wataalamu wa afya, hii inaweza kusababisha hitilafu ya ubongo Kwa Mtoto. Na Kwanza kitabibu hairuhusiwi kufanya kitendo kama hicho.
Serikali kupitia wizara ya AFYA, toeni elimu ya kutosha, hasa visiwani Zanzibar (Pemba, Unguja).
Hospitali ya Muhimbili kitengo cha watoto na kitengo cha ubongo, inawapasa kutoa elimu ya AFYA ya Mtoto hasa huko visiwani Zanzibar.
Wizara ya ustawi ya jamii jinsi na watoto, elimisheni jamii, kwamba Mtoto kuwa na kichogo sio ukilema. Bali ni maumbile ya kawaida Kwa ukuaji wa mtoto pamoja na afya yake.
Maana wana wanyanyasa watoto vichanga, haya yote ni matokeo ya ukosefu wa elimu na Imani potofu huko visiwani Zanzibar.
Mtoto kuwa na kichogo Sio Kwamba atakuwa na muonekano mbaya AU Kwamba atachekwa na wenziwe shuleni, lahasha Bali, ni maumbile halisi ya kibinaadamu.
Wenyeji wa huko visiwani, heshimuni haki za watoto.