Serikali Toeni Elimu Visiwani waache Tabia ya kuzuia watoto wachanga Wasipate VISOGO!

Serikali Toeni Elimu Visiwani waache Tabia ya kuzuia watoto wachanga Wasipate VISOGO!

Niliwahi kusikia kuwa wanawake wa kizanzibar na Pemba hawazalii huku bara!
Siku chache kabla ya kujifungua wanakimbizwa kwa boti Zanzibar! Inaweza kuwa kweli wanawahishwa ili watoto wao wabonyezwe visogo?
 
Kwani wadhani bara vichwa havibandwi?..tungekua na machogo kama ugali wa jela ikiwa tusingebandwa
Inatokea labda kuna tatizo limetokea wakati wa fungua AU mtoto akiwa tumboni Kwa mama yake,
Na hiyo urekebishwaji wa kichwa hufanyika hospital Kwa uangalizi wa waataamu wa AFYA.

Tofauti kabisa na Zanzibar, mtoto akazaliwa Tu na kichogo ni kosa , anatafutwa mtaalamu Tu wa jadi anaanza kugandamiza kichogo. Haya ni mazoe na tamaduni za hovyo Tu
 
Kitendo cha kuvibonyeza, kuvikandamiza vichwa vya watoto wachanga ili kuzuia kichogo, bila kutumia wataalamu wa afya, hii inaweza kusababisha hitilafu ya ubongo Kwa Mtoto. Na Kwanza kitabibu hairuhusiwi kufanya kitendo kama hicho.

Serikali kupitia wizara ya AFYA, toeni elimu ya kutosha, hasa visiwani Zanzibar (Pemba, Unguja).

Hospitali ya Muhimbili kitengo cha watoto na kitengo cha ubongo, inawapasa kutoa elimu ya AFYA ya Mtoto hasa huko visiwani Zanzibar.

Wizara ya ustawi ya jamii jinsi na watoto, elimisheni jamii, kwamba Mtoto kuwa na kichogo sio ukilema. Bali ni maumbile ya kawaida Kwa ukuaji wa mtoto pamoja na afya yake.

Maana wana wanyanyasa watoto vichanga, haya yote ni matokeo ya ukosefu wa elimu na Imani potofu huko visiwani Zanzibar.

Mtoto kuwa na kichogo Sio Kwamba atakuwa na muonekano mbaya AU Kwamba atachekwa na wenziwe shuleni, lahasha Bali, ni maumbile halisi ya kibinaadamu.

Wenyeji wa huko visiwani, heshimuni haki za watoto.
Wala hakandamizwi mtoto.

Mtoto anafungwa fungwa asijigeuze kulalia ubavu wa kichwa.

Hiyo watu wa Pwani tunafanya sana, siyo Zanzibar tu.

Mtoto atavaaje baraghashia akiwa na chogo kama isuzu za zamani?
 
Wala hakandamizwi mtoto.

Mtoto anafungwa fungwa asijigeuze kulalia ubavu wa kichwa.

Hiyo watu wa Pwani tunafanya sana, siyo Zanzibar tu.

Mtoto atavaaje baraghashia akiwa na chogo kama isuzu za zamani?
Kwa nini asitengenezewe baraghashia kulingana na komwe lake? Otherwise no comment!😀😀
 
Wala hakandamizwi mtoto.

Mtoto anafungwa fungwa asijigeuze kulalia ubavu wa kichwa.

Hiyo watu wa Pwani tunafanya sana, siyo Zanzibar tu.

Mtoto atavaaje baraghashia akiwa na chogo kama isuzu za zamani?
Kwani kuvaa baraghashia ni lazima Kwa Mtoto,? Mbona munanishangaza nyie,

Haki ya Mtoto ni chakula Bora, AFYA bora, Elimu Bora, malazi Bora, Sio kuwalaza watoto watano kitanda kimoja.

Kwani mtume anasemaje kwenye hili swala la kichogo Kwa Mtoto
 
Wanajinasibu kwa namna hiyo.
Haha haha itakuwa hawajitambui Hao kuwa walikuwa ni watumwa walio tolewa Bara kuja kufanya Kazi ngumu hapo Zanzibar.

History ya Zanzibar inaelekea haijulikwani Hata Kwa wanaojita wazanzibar
 
Back
Top Bottom