Serikali toeni hizo Combination za Dini hii siyo nchi ya kidini

Ndiyo maana tumeanza kushuhudia magaidi na mitume feki ya kikristo kwa sababu ya huu upumbavu ushabiki wakidini hadi mashuleni ..miaka ya nyuma huu upuuzi ulikuwa ni ngumu sana kufanyika
 
Wasiwasi wako ni nini?, je ingewekwa comb. ya dini moja siungepasuka.
 
Masomo yalikuwa kama ziada sio rasmi sasa hivi yamekuwa rasmi shida wengine sijui hata kama form six mlipita......sasa hivi yamewekea na combi ndo tuna pinga hapo
Bado Sijapata mantiki ya hoja ya kupinga tahasusi mpya.Ina maana mwanafunzi anaposoma Somo la dini na masomo mengine mawili tena Kwa hiyari yake ni madhara gani hutokea?.Mbona wanapoenda vyuo vikuu zipo shahada zinazohusu dini.Nilidhani labda watakosa maarifa ya awali wanapoanza shahada zao lakini hujagusia hilo.
 
Hii ni philosophy nafkir ipo kwen general studies.
 
Hivi serikali inafundisha dini ili iwaje?
 
Jambo usilolijua mtoa mada dini aiwezi tengna na siasa kwani dini na siasa za utawala mpango wao ni mmoja.
 
Kodi zikikusanywa huwa zina alama hii imetoka kwa mwabudu mawe, hii kwa muislamu, hii kwa mkristo..kodi ninayotoa mimi mkristo sitaki itumike kulipa mshahara wa mwalimu anayefundisha dini nyingine..lakin pia, kwa vile ni utashi wa mwanafunzi kuchagua combi inaweza tokea wanafunzi wa dini moja wanaosoma dini yao ni wachache halafu wanaosoma dini nyingine ni wengi matokeo ni km watu wa dini yenye wanafunzi wachache wanagharimia masomo ya dini isiyo yao ambayo ina wanafunzi wengi!
 
Zibaki hapo hapo,

Mungu ana umuhimu ktk maisha yetu,

Wazazi hawana muda wa kukaa na watoto, huko mashuleni nahisi ni muhimu wakafundishwa.
 
Ndg tunapambana na kufufua maadili kuanzia ngazi ya familia hadi shule chuo.
Ufisadi usiomithirika wa sasa tumekubaliana chanzo ni tamaa na ubinafsi uliopitiliza kwa kukosa hofu ya Mungu!
(kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa)
Hadi kiongozi/mtumishi anaiba kiasi hata asichojua ni cha nini!
....Nashauri pia serkali tuliwekee mkazo wa kimtaala somo la saikolojia na sociolojia ili kupamabana na kiasi kikubwa cha tatizo la afya ya akili nchini!
Ukienda makanisani hasa yanayojinasibu kwa miujiza ndo utaelewa ukubwa wa tatizo! kuanzia wasomi hadi mbumbumbu wanahangaika na miujiza! sio tena kuutafuta ufalme wa Mungu wala baraka katika utendaji wao!(kuna kanisa Pastor anapiga simu mbinguni Mungu anatuma muamala na waumin wanaamin na kuwasha simu kama fiesta)
 
Zibaki hapo hapo,

Mungu ana umuhimu ktk maisha yetu,

Wazazi hawana muda wa kukaa na watoto, huko mashuleni nahisi ni muhimu wakafundishwa.
Mfundishiwe katika makanisa na misikiti yenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…