Serikali toeni hizo Combination za Dini hii siyo nchi ya kidini

Serikali toeni hizo Combination za Dini hii siyo nchi ya kidini

Sawa nimeandika maoni yangu kama msomi nisiyependa taifa letu liweke mambo imani ya ukristo au uislam kwenye mambo ya kiserikali ni hatari mno ... naamini watu wenye nia njema wameona hili ila hawana la kufanya....
aliekuambia wewe ni msomi nani?
 
Wazazi wengi wanachotaka ni "kufaulu" Kwa, watoto wait ma A kibao, na kamserereko ni huko kwenye masomo ya dini,

Mtoto atapata ma D matupu,lakini mashekh na maustadh watampa As tupu kwenye islamic knowledge! Hakuna wakupinga! Huyooo anapata mkopo akachezee, sasa unasoma bible knowledge, au islamic Studies, unataka kuwa mchungaji au shekh wa msikiti!?

Yaani upoteze miaka minne ya chuo kusomea dini?!
Kuna mchepuo serikali imecheza kama Pele,

Zamani tulikuwa na PCM, physics chemistry na maths, sasa kutwkuwa na PMC, physics, maths, na computer studies, hii safi Sana, ila tungeweka zaidi masomo ya IT, kilimo, political sayansi,
Wewe ni mpumbavu na hujui unachokiongea. Vyuo vikuu maarufu huko Ulaya vinatoa digrii za masomo ya dini wewe kilaza uliye huku mwishoni mwa dunia ndiyo uhoji kama nani?
 
Ndo maana pwani ya africa mashiriki hakuna maendeleo sababu ya watu kama wewe
Hatuwezi kusikiliza wapumbavu kama wewe ,hakuna kitu utafanya kwa uoga wako...Atheist wengi hamjitambui ,kama huamini si uache.
Wafanyakzi wa serikali mpaka Raisi ana dini ,wewe kajamba 8 nenda kweny nchi zenye Atheists wenzio.!
 
Wewe ni mpumbavu na hujui unachokiongea. Vyuo vikuu maarufu huko Ulaya vinatoa digrii za masomo ya dini wewe kilaza uliye huku mwishoni mwa dunia ndiyo uhoji kama nani?
Kwenye shule za umma kulitakiwa kuwe na Religious studies, wanafunzi wajifunze kuhusu dini zote, sio kusoma kidini kama kanisani au msikitini.
 
kama mtaala unao boreshwa ndo huu Bora tubaki na wazaman tumetoka kwny technical school zeny electrical, mechanic,plumbing, drawings na computer tunaenda kwenye divinity na Islamic
Inasikitisha sana
 
Selikali pumbavu ya ccm haiwezi kuelewa maana tujiulize tu hao walimu watakao kuwa kwenye hayo.mashule wenye kufundisha dini je awatalazimisha mambo yao ya kidini kuanzia uvaaji itikadi na utabaka mfano mwanafunzi wa kiislama akifanyiwa kitu awezi kwenda kwa mwalimu wa dini yake kuki lalamikia kidini na kuleta tatizo ...mwisho wa siku mambo kama ya zanzibar yataingia mashuleni kuwalazimisha watu wengine wasionekane wanakula chakula kisa mfungo wa ramadhani
Wewe ni mpumbavu sana. Hakuna mwalimu wa dini anayelipwa na Serikali. Walimu wa dini wanaofundisha kwenye shule za msingi na sekondari wanalipwa na madhehebu yao husika na wala siyo waajiriwa wa Serikali. Ama kama inakuuma kuona kwamba Serikali italazimika kuajiri walimu wa kufundisha lugha ya Kiarabu mashuleni tambua kuwa Kiarabu si dini na lugha tu iliyokuwepo kabla hata ya Uislam. Kuna Wakristo kibao ni wajuzi wa lugha ya Kiarabu na wanaweza kuajiriwa pia kufundisha somo hilo. Mbona huhoji walimu wanaofundisha Kiingereza na Kifaransa mashuleni?
 
Kwenye shule za umma kulitakiwa kuwe na Religious studies, wanafunzi wajifunze kuhusu dini zote, sio kusoma kidini kama kanisani au msikitini.
Huo utaratibu viongozi wa dini zote waliukataa. Muislam wa kweli na Mkristo wa kweli hawawezi kukubali watoto wao wafundishwe dini tofauti na zao. Kingine masomo ya dini ni hiyari nyie povu linawatoka la nini?
 
Nimeona wameongeza combi nyingi sana kwenye kwenye elimu ya advance jambo zuri ila lina ubaya wake pia

Niende kwenye mada nchi yetu sio ya kidini yaani haifungamani na dini yeyote ile sasa serikali kwanini imeweke masomo ya dini ya kiislam na kikristo kwenye mtaahala ni kurudisha nyuma taifa letu na kuleta mkanganyiko hizo elimu zitolewee miskitini na makanisani full stop visiweke kwenye mifumo rasimi ya kiserikali

Naandika haya najua madhara ya serikali kuanza kuweka vitu vya kidini kwenye mifumo rasmi ya serikali

Sasa mfano wakristo wana madhebu mengi mno walokole waroman wapentecoste ...haya waislam kuna shia kuna suni ....mtaafundishaje maana haya madhehebu huwa yanatofautiana kwenye mambo mbali mbali kama sio kuleta fujo na mikanganyiko

Hao walimu watalipwa na nani yaani serikali ilipe walimu wa dini kama kweli ndo tumefikia huku tena katika elimu ya advance watoto narudia wasome hizo elimu huko makanisani au misikitini na madrassa ....

Naamini raisi ajae ataliangalia hili labda huyu wa sasa kaona sawa.....tunaomba rais atakae kuja atoe haya madude sijui divinity/ukristo sijui islamic knowledge hayana umuhimu wa taifa ambalo liko nyuma kisayansi na kiteknlogy mnazidi kulipoteza taifa kuleta mambo imani kwenye ulimwengu wa elimu serious zinahitaji fact sio imani .... fact ni muhimu kuliko imani ndo maana wazungu wanatupita maana wanaamini katika fact sio imani......sasa sisi imani ndo tunataka kabisa iwe elimu rasmi ni uzwazwa...

TANZANIA SIO NCHI YA KIDINI NA HAIRUSIWA HATA KUONESHA DALILI HIZO NI HATARI MNO KUWEKA MASWALA YA DINI SERIKALI

Eti necta nao wako busy watunge mitihani sijui yesu alifanya nini mara sijui mtume alifanya nini ...

Tuiheshimu tanzania hasa tanganyika mambo ya dini hatutaki toeni....kama upande wa pili znz watapenda muwakeeni ila tanganyika haiwezi jengwa kamwe na mifumo hii mnayoleta TANGANYIKA TUNATAKA WATOTO WAWE BUSY NA ELIMU DUNIA ZAIDI.....

SIJUI MAKAMBA SIJUI MAKONDA SIJUI RIDHIWAN AU YEYOTE ATAYEKUJA KUWA RAIS BAADa ya mama samia atoe haya madini kwenye elimu rasmi hayana tija kwa taifa ... taifa linahitaji sana kuendelea upande wa elimu dunia...... sio elimu ahera

Acha utoto na ujinga wewe.Hayo masomo yapo zamani na hayajawahi kuleta shida.
 
Kwenye shule za umma kulitakiwa kuwe na Religious studies, wanafunzi wajifunze kuhusu dini zote, sio kusoma kidini kama kanisani au msikitini.
Pia masomo hayo ni optional sio lazima ,waweke tu fresh anayetaka fresh ..

Sioni haja eti kupinga kwa sababu serikali sawa haina dini ila wananchi wake wana dini ..
 
Wewe ni mpumbavu sana. Hakuna mwalimu wa dini anayelipwa na Serikali. Walimu wa dini wanaofundisha kwenye shule za msingi na sekondari wanalipwa na madhehebu yao husika na wala siyo waajiriwa wa Serikali. Ama kama inakuuma kuona kwamba Serikali italazimika kuajiri walimu wa kufundisha lugha ya Kiarabu mashuleni tambua kuwa Kiarabu si dini na lugha tu iliyokuwepo kabla hata ya Uislam. Kuna Wakristo kibao ni wajuzi wa lugha ya Kiarabu na wanaweza kuajiriwa pia kufundisha somo hilo. Mbona huhoji walimu wanaofundisha Kiingereza na Kifaransa mashuleni?
Wapi nimeandika malipo au wanalipwa na serikali? Bora wangelipwa na serikali wafundishe dini sehemu stahiki ...ila ili la dini kwenye shule za serikali ni kosa kubwa sana
 
Wapi nimeandika malipo au wanalipwa na serikali? Bora wangelipwa na serikali wafundishe dini sehemu stahiki ...ila ili la dini kwenye shule za serikali ni kosa kubwa sana
Hebu ainisha hilo kosa kisheria lipo wapi?
 
Islamic..... islamic........ islamic........ arabic....... arabic ...........islamic.......divinity toeni ujinga huu kwenye mitaala, mambo ya udini hayata kaa kulikomboa taifa hili kwenye umaskini

bado dini zenyewe hazilipi kodi sasa si mnazalisha wachungaji na mashehe wengi baadae wakajifiche huko wasilipe kodi?? tuondoe udini kwenye mambo ya maana, China hawana upuuzi huu ndo mana lile taifa limeendelea tunaagiza mpaka stiki za meno kutoka kwao.
 
Ni option sio lazima ... Uhuru wa kuchagua anachopenda mtoto au mzazi
 
Na ulimwengu wa sasa wa kuhalalisha ushoga ..naipongeza serikali kwa hili
 
Back
Top Bottom