Tunajadiliana kuhusu maombolezo ya 29.10.2025
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema Serikali bado haijafanya uamuzi kuhusu pendekezo la kutenga siku maalumu ya kitaifa ya kuwakumbuka Watanzania waliofariki na kuathiriwa na vurugu zilizotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akieleza kuwa suala hilo linaendelea kufanyiwa majadiliano na tathmini.
Akizungumza na gazeti la Mwananchi, Msigwa amesema baadhi ya watu wanaona kuwa kuadhimisha siku hiyo kunaweza kufufua maumivu ya waathirika, huku wengine wakisisitiza umuhimu wa kuwaenzi waliopoteza maisha na kuwakumbuka waliojeruhiwa na kupata madhila mengine.
Amesema Serikali haijafikia uamuzi wa mwisho kwa kuwa si kila pendekezo la tume hutekelezwa mara moja bila tathmini ya kina.Pendekezo hilo lilitolewa na Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Ghasia na Uvunjifu wa Amani, iliyoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman, wakati akiwasilisha ripoti kwa Rais Samia Suluhu Hassan Aprili 23, 2026.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watu 518 walifariki dunia na wengine 2,390 kujeruhiwa katika ghasia zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.Wakati Serikali ikiendelea kutathmini pendekezo hilo, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limeelekeza parokia, vituo vya sala na taasisi za Kanisa Katoliki nchini kuadhimisha misa maalumu Alhamisi, Oktoba 29, 2026, kwa ajili ya kuwaombea waliouawa, waliopotea, waliojeruhiwa na wengine walioathiriwa na matukio hayo.
Maelekezo hayo yametolewa na Rais wa TEC, Askofu Wolfgang Pisa, kupitia waraka wa kichungaji wa Oktoba 23, 2026.Mbali na Kanisa Katoliki, Chama cha ACT Wazalendo kupitia Ngome ya Wanawake kilizindua mnara wa kumbukumbu na kuweka mashada ya maua Machi 3, 2026, kwa ajili ya kuwakumbuka waliopoteza maisha.
Hatua hiyo ni miongoni mwa jitihada zilizofanywa na taasisi za kisiasa na kijamii kuenzi waathirika wa matukio hayo, huku wito wa kutambua madhila yaliyowapata Watanzania ukiendelea kujadiliwa.
Katika waraka wake, Askofu Pisa amesema Kanisa linaona umuhimu wa kuendelea kuliombea Taifa na watu wanaoendelea kuishi na maumivu yaliyotokana na matukio hayo, akisisitiza haja ya kuombea umoja, upendo, ukweli, haki na mshikamano.