DOKEZO Serikali tusaidieni wananchi, magari yanayouzwa kwenye yard za Wapakistan mitaa ya Morocco na Victoria ni mabovu sana

DOKEZO Serikali tusaidieni wananchi, magari yanayouzwa kwenye yard za Wapakistan mitaa ya Morocco na Victoria ni mabovu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wamefuta 1 au 2 yaani ilikuwa na km217,000 au km117,000. Gari wanajua ni nzuri pamoja na km hizo ila wanajua ukiona hizo km hutanunua kwahio wanafuta tu hio 1 au 2 kukuridhisha. Gari ya 2002 itakuwaje na km12,000?
Niliagiza kutoka japan baada ya kuangalia details zote kwenye mtandao, unaweza kuta ilikuwa haitumiki mara kwa mara au mwenye gari hana safari au mizunguko mingi, au alikuwa na gari nyingine pia. Japan siyo kama bongo ambapo wengi wanakuwa na gari moja na wanazurura huku na huko bila mpangilio, wajapan wengi wana discipline ya hali ya juu ya maisha...​
 
Gari yoyote used kutoka nje haikosi hitilafu mkuu
Labda mtu akanunue showroom toyota au dt dobie mapugu Road huko

Ova

Sio kweli nina gari nimenunua mwaka wa tatu huu naitumia na nimesha badilisha tairi mara mbili kwa jinsi ninavyo safiri nayo sana mikoani hata Battery iliyokuja nayo tu sijawahi hata kuifungua hapo ilipo sembuse kuibadilisha ni tairi na normal service tu ilikuja na km. 63,000 hivi na sasa hivi ina km 100,000 +.
 
Wamefuta 1 au 2 yaani ilikuwa na km217,000 au km117,000. Gari wanajua ni nzuri pamoja na km hizo ila wanajua ukiona hizo km hutanunua kwahio wanafuta tu hio 1 au 2 kukuridhisha. Gari ya 2002 itakuwaje na km12,000?
Hivi mkuu, unapobadilisha ile odometre, kumbukumbu za kilometa zinazosoma kwenye odometre mpya zinakua za gari toka iliponunuliwa au za toka odometer ilipobadilishwa??

Msingi wa swali ni kuwa baadhi ya web za japan huwa unaona wameandika kabisa Changed odometer kama detail kwenye gari wauzalo
 
Zitasoma za odometer mpya. Hii nayo ni njia rahisi ya kucheza na km za gari kwa wauzaji.
 
Niliagiza kutoka japan baada ya kuangalia details zote kwenye mtandao, unaweza kuta ilikuwa haitumiki mara kwa mara au mwenye gari hana safari au mizunguko mingi, au alikuwa na gari nyingine pia. Japan siyo kama bongo ambapo wengi wanakuwa na gari moja na wanazurura huku na huko bila mpangilio, wajapan wengi wana discipline ya hali ya juu ya maisha...​
Jp au Ulaya mtu hawezi kununua gari kama hana matumizi nayo. Anyway it's all good.
 
Serikali itupie macho uhuni unaofanywa na hawa wafanyabiashara wa magari wenye asili ya Pakistan.

Jana mida ya saa sita mchana tulienda na rafiki yangu kwenye moja ya maduka (yard) ya kuuzia magari. Rafiki yangu alikuwa anataka Toyota Probox kwa ajili ya kubebea mizigo yake Kariakoo na kwenye godown yake.

Tukafika hiyo saa sita tukakuta magari ndiyo yanapangwa. Walivyomaliza tukaomba kukagua gari moja. Kijana akaitwa akaja mbio na funguo za gari zikiwa mkononi kwake.

Nikakaa kwenye usukani na rafiki yangu pembeni. Nilipoiweka gari switch on nikakuta odometer inasoma gari imetembea kilometa 219,551. Bei milioni 16

Tukashauriana tukasema hapana hili gari halifai. Tukaendelea duka jingine na jingine na jingine.

By saa tisa tukafudi tena kwenye ile Probox, tukakuta ishachezewa odometer, sasa inaonekana imetembea kilometa 46,755.

Nilikuwa nimeoiga picha chasis namba mlangoni na dashboard. Nikipowauliza mbona hii gari mmeichezea kilometa, nikawaonyesha na picha wakakasirika sana wakapora simu yangu. Nikawaambia kaeni nayo, leo mtalala polisi.

Nikawa naondoka kulekea kwenye gari tuliyokuja nayo hapo yard, ndipo mmoja ya wafanyabiashara wale akaja mbio huku akinibembeleza nifute zile picha watatupa million moja.

Hela tamu, tukakubali kufuta picha, tukabeba milioni yetu. Tukaondoka.

Lakini backyard ya hizo yard zote kuna mafundi wako busy wanayaweka sawa mamikweche hayo.

Kingine tulichogundua ni kwamba kwenye minada ya magari, magari ya nauzwa kwa classes. Hawa wanachagua class duni kabisa, yakifika hapa wanaongea vizuri na wakaguzi, wanatolewa bandarini.

Kwa somo hili tulilojifunza jana rafiki yangu amekata tamaa kabisa na magari haya. Sasa kaona bora aagize kutoka Japan 🗾 asubiri siku 45 abebe mwana wake wa uhakika
Umenkumbusha jaba. Hamhitaji serikali kuwasaidia. Jisaidieni wenyewe. Nenda choma moto kila kitu kwisha mchezo
 
Gari yeyoye chini ya 100,000 imechezewa, na gari nzuri sio hizo odo ni kuipeleka fundi akague tu
Jamaa yangu alinunua jan international ina 159,000 km hadi leo ina miaka zaidi ya 5 na bado inadunda na haijamsumbua
Janmotors wanauza gari kama ilivokuja...na kama kuna issues wanakuambia, na wanakumbia wakufixie au wakupunguzie bei ukafix kwa fundi wako yet unanunua price ya chini..na wanakupa auction details zote
 
Hata uniue yard sipaamini
Au kununua tu kwa mtu.usiyemjua
 
Back
Top Bottom