DOKEZO Serikali tusaidieni wananchi, magari yanayouzwa kwenye yard za Wapakistan mitaa ya Morocco na Victoria ni mabovu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwani ungepeleka hizo details police ndio wangekuja kuwafanya Nini hao jamaa?Kuwatishia/kuwafunga au?

Mpakistani hakupi 1mil kizembe namna hio.
Polisi wangeweza kutowafanya kitu, ila kumpora mtu simu yake akipata mwanasheria mzuri akiunganisha na vingine ulimpora, kutumua ofisi yako kama tegesheo la kupora watu vitu basi ingekuwa kesi kubwa au anehonga sana zaid ya hiyo 1m
 
Kurudisha Odometer sio zoezi la saa moja. Ni zoezi la muda kidogo.

Jan Motors wao hawa gari zao utaikuta kama ilivyo na bei zao ziko chini, hivyo watu huenda kwao wananunua afu wanaenda uza tena
 
Ninachojuwa Mimi gari used kitu muhimu sana ni engine na body, jitahidi kumlipa Fundi mkweli uende naye kununuwa gari kuna technical kadhaa za kuangalia.

Kuna kitu kinaitwa kuvunja, mfano una Rav4 unataka tako la nyani unampa mwenye yard Rav4 unamuongeza na pesa kisha anakupa tako la nyani.

Affricaries ni kampuni kubwa ya kuuza magari ya Fidahussein lakini wanarudia Rangi magari.

Kama kuna mtu anawaza kwenda Polisi asipoteze muda wake, Mimi ni ushahidi nimeshakamatwa na Interpol nikiwa na gari ya wizi iliibiwq Japan lakini tulinunuwa Kwa Fidahussein alichofanya alinipa gari ya kutumia Kwa muda then akaenda kutowa ile gari ya wizi nikarudishiwa.

Kuna kipindi Interpol huwa wana kuja Tanzania kuendesha oparesheni ya magari ya wizi, wale wenye magari ya kijanja ya bei mbaya huwa wanapewa taarifa wanayafungia.

Utajifanya unakwenda kutowa taarifa Polisi wakati huyo mkuu wa kituo kapewa gari bure atumie na haohao unaodhani eti unawalipuwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…