DOKEZO Serikali tusaidieni wananchi, magari yanayouzwa kwenye yard za Wapakistan mitaa ya Morocco na Victoria ni mabovu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Tuambie mkuu Botswana hali ikoje?
 
Kuna gari nimeona ina km 189,000 Crown ya 2004, iko website ya Jan International.

Ikinunuliwa na dalali anapunguza hadi 50,000 afu anaongeza milioni juu
 
Sasa kama wewe ulikula rushwa ya milioni moja unapata wapi ujasiri wa kuja kulalamika hapa? Una tofauti gani na CHADEMA waliomlaumu mtu ni fisadi halafu wakamteua kuwa mgombea wao wa urais?
 
Hatukukupatia milion moja tulikupatieni elfu 10 tu ya mafuta, acha uongo. Halafu ile gari mliyokuja nayo mbayaaaaa!
 
Mchezo wa kurudisha nyuma km umeshamiri sana, kuna LC fulani inauzwa body, engine na gearbox vyote viko vizuri kabisa, wao wanasema chuma imekaza. Km kwa sasa inasoma 146K. Nilishangaa kuiona LC iwe na km chache kiasi hicho na imetumika bongo. Bahati nzuri owner ametunza vizuri logbook ya gari tangu ananunua mpaka sasa. Kwenye logbook ya gari tukaona file ya inspection iliyofanyika Japan 2005, odometer ilikuwa inasoma 197k (hii ndio mistake aliyofanya owner, ilibidi hili file alitoe ili awe smart) leo hii baada ya miaka 15 plus odometer inasoma 146K. Tulipochunguza sana tukaona hata dashboard yenyewe ina cracks zinazoashiria ilikuwa tempared. Lakini sikuona sababu kubwa ya kufanya utundu huo body ya gari na performance yake vyote viko vizuri kabisa
 
Hata huko japan unaweza kupigwa tukio,
 
Ukute huyu ndo Mpakistani mwenyewe, nimewaza tu
 
We mleta uzi ulipopewa hyo mln 1 ulitakiwa ukaushe,sasa hela uchukue na kuwachoma uwachome
Katika mambo ya kidunia utakuja poteza uhai kiboya

Ova
 
Nchi ina laana hii. Kwa nini wapakistani wanaruhusiwa kuja kuuza magari used? Ni watanzania au ni wageni?
 
Hao ni wawekezaji mkuu.
Mkuu wangu wawekezaji wa namna hii nitawapinga mpaka kesho. Magari used tuwaachia wabongo wafanye hiyo shughuli. Na uzuri ni kwamba unaweza kununua moja kwa moja kutuka Japan. Big NO!
 
Wapuuzi sana, hivi kwa nn Tz inachezewa sana??
 
Kuna gari nimeona ina km 189,000 Crown ya 2004, iko website ya Jan International.

Ikinunuliwa na dalali anapunguza hadi 50,000 afu anaongeza milioni juu
[emoji1787]bro tangu mwanzo anapita na upepo anapiga promo Jan motors.....(kuna site za auction ukiingia unaona hadi history ya gari kama iliwahi pata ajali...kuhusu magari usikurupuke bora uingie gharama zaidi ili upate kitu kizuri...
 
Nilishawahi kukaa na Mpakistan mmoja wa Yard akaniambia magari mengi yanayokuja Japan Odometer ni 120,000+ lakini kutokana na Wabongo wengi kupenda low millage...mtu anakuja kwenye yard yake anakuta gari ina millage 90,000 ya halali anaondoka anaenda kununua yenye Millage 200,000 ila imechezewa inasoma 43,000. Sasa kila mtu anataka kuuza kilichobaki saivi wote wanachezea , kama unataka gari yard kikubwa uende na mtu mzuri akakague mifumo yote ya gari na uzima wake pamoja na hali ya bodi..Japan kuagiza kunahitaji utulivu na kampuni sahihi kuna mtu alishawahi kulalamika huku aliagiza gari japan ikaja imeliwa kutu vibaya mno na mwingine aliagiza japan akakuta Chassis ilikatika na imechomewa, kwa sisi roho ndogo gari za kwanza tunataka tulipie apo tuondoke na gari apo apo tunahitaji umakini extra.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…