DOKEZO Serikali tusaidieni wananchi, magari yanayouzwa kwenye yard za Wapakistan mitaa ya Morocco na Victoria ni mabovu sana

DOKEZO Serikali tusaidieni wananchi, magari yanayouzwa kwenye yard za Wapakistan mitaa ya Morocco na Victoria ni mabovu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mtu anakula rushwa kuficha ushahidi, akishirikiana na matapeli.

Halafu anailalamikia serikali imsaidie.

Serikali itakusaidia vipi wakati ushakula rushwa kuharibu ushahidi?

Hao ndiyo wabongo wengi walivyo.

Contradictions.
Kwanza huyo ashaambiwa hizo gari ni used from Japan alitegemea nini zaidi

Hayo mambo ya kuchezea km,kupiga rangi na kunyoosha body ya zilizotoka nje haikuanza leo wala jana

Kama mfuko wake ni mzuri aende show room za toyota wamuagizie gari
0 km ...analetewa gari anachana maplastik ndani kwenye viti,usukani nk.....anakuta mpk menu ya kitabu kuhusu gari [emoji1]

Alafu huyo jamaa ashachkua mln 1 sasa anacholalamika nini kama rushwa ashapokea

Ova
 
Wivu unakusumbua. Fidia kwa harassment niliyopata
Maana yangu ni kwamba, usingelileta hilo jambo hadharani tena, kwa sababu ulishanyamazishwa kwa rushwa.

Rushwa ile ulipewa ili yaishe, lakini wewe ukapokea na ukayaendeleza!

Ndiyo nikakueleza katika comment yangu ile kuwa hauwezi kukaripia na kulilaani jambo unalolipenda kulifanya mwenyewe.

Uhujumu na rushwa hubebeshwa mbeleko moja, mashitaka yake husomwa kwa pamoja: "rushwa na uhujumu uchumi".

Kwako wewe na hao Wapakstani ni nani anayeweza kumtoa kibanzi mwenzake kwenye jicho?

Hii nchi raia wake tulishakuwa corrupted sana kupita kiwango cha ustahimilivu waalah!
 
Serikali itupie macho uhuni unaofanywa na hawa wafanyabiashara wa magari wenye asili ya Pakistan.

Jana mida ya saa sita mchana tulienda na rafiki yangu kwenye moja ya maduka (yard) ya kuuzia magari. Rafiki yangu alikuwa anataka Toyota Probox kwa ajili ya kubebea mizigo yake Kariakoo na kwenye godown yake.

Tukafika hiyo saa sita tukakuta magari ndiyo yanapangwa. Walivyomaliza tukaomba kukagua gari moja. Kijana akaitwa akaja mbio na funguo za gari zikiwa mkononi kwake.

Nikakaa kwenye usukani na rafiki yangu pembeni. Nilipoiweka gari switch on nikakuta odometer inasoma gari imetembea kilometa 219,551. Bei milioni 16

Tukashauriana tukasema hapana hili gari halifai. Tukaendelea duka jingine na jingine na jingine.

By saa tisa tukafudi tena kwenye ile Probox, tukakuta ishachezewa odometer, sasa inaonekana imetembea kilometa 46,755.

Nilikuwa nimeoiga picha chasis namba mlangoni na dashboard. Nikipowauliza mbona hii gari mmeichezea kilometa, nikawaonyesha na picha wakakasirika sana wakapora simu yangu. Nikawaambia kaeni nayo, leo mtalala polisi.

Nikawa naondoka kulekea kwenye gari tuliyokuja nayo hapo yard, ndipo mmoja ya wafanyabiashara wale akaja mbio huku akinibembeleza nifute zile picha watatupa million moja.

Hela tamu, tukakubali kufuta picha, tukabeba milioni yetu. Tukaondoka.

Lakini backyard ya hizo yard zote kuna mafundi wako busy wanayaweka sawa mamikweche hayo.

Kingine tulichogundua ni kwamba kwenye minada ya magari, magari ya nauzwa kwa classes. Hawa wanachagua class duni kabisa, yakifika hapa wanaongea vizuri na wakaguzi, wanatolewa bandarini.

Kwa somo hili tulilojifunza jana rafiki yangu amekata tamaa kabisa na magari haya. Sasa kaona bora aagize kutoka Japan 🗾 asubiri siku 45 abebe mwana wake wa uhakika
Hata huko Japan kuna watu wanacheza na Odomometer
 
Noma sana, hii ya kuchezea odometer inafanywa sana, wanajua wabongo wengi wanaangalia uchache wa mileage na sio service history. Kwa hiyo wanarudisha odo nyuma ili kutupa tunachokipenda.

Hongera kwa kupata milioni 1 na bado umefichua uovu. Sasa hapo polisi nao wanakwenda kujipatia hela huko.
[emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukienda kwenye yard kununa gari wewe nenda na fundi wako unayemuamini aangalie engine, gear box na body kama vipo vizuri . Ukienda na fundi janja janja mpenda pesa atakuchomesha atachukua pesa kwako na kwa hao wauza magari kwani kuna ishara atapewa arudi baadae kuja kuchukua mzigo wake. Hiyo habari ya km achana nayo kabisa utapotea. Unakuta gari ya mwaka 1995 imeletwa hapa kwetu 2022 halafu eti imetembea km 10,000 si maajabu hayo.
Wewe unaujua sana mrorongo wa figisu za kwenye maYard!

Mambo uliyoelezea, ndiyo sahihi ya kuangalia kabla ya kununua na siyo Odometer (km)!

Kwenda na fundi inaweza ikasaidia ama isikusaidie sana kama fundi huyo ni "macho pilu pilu" na kumcontrol yataka akili za ziada kwa kweli.
 
IMG_8838.jpg
 
Nakumbuka juzi TRA wakati wanatoa training ya UPGRADED E FILLING SYSTEM mkufunzi alisema "najua kuna watu wamekuja ili kuijua system na kuichezea kufanya uharibifu
Tafadhini acheni"
Sisi ndo wabongo bwana.

Hakuna kitu cha hovyo na chepesi cha kuchezea kama mfumo.
Sababu mfumo ni programing na KILA program Ina weakness yake,pale pale penye weakness ndipo mswahili anatengezea maisha.
Mifumo ni kwa ajili ya wenzetu Ulaya,kule mtu analipwa package ya kutosha hawezi kosa package kwa kupata kiduchu kwenye mfumo.
Mswahili yupo radhi akalipwe elf 5 masaa 12 KWA muhindi lkn ni lazima tu atamuibia.
 
Waombe file la Gari lilio tokanalo japan,Ukiona wanakupiga janjajanja sepa.

Option nyingine,chukua VIN(Vehicle Identification Number) ya Gari i-search mtandaoni possibility kubwa Ni kuikuta Gari hio na details zake zote(maana Gari hizo zinauzwa minadani hukk Japan) then linganisha Km za hii Gari hapo Yard vs Km ikiwa huko Mnadani.

Zamani Nilikua nalipia pesa kidogo ($10) kwny website flani,nawatumia VIN then wananitumia details zote za hio Gari,Ila hii sites iko shutdown siku hizi.
Kama hiyo site ishakua shut down basi ni biashara kubwa
 
Ukienda kwenye yard kununa gari wewe nenda na fundi wako unayemuamini aangalie engine, gear box na body kama vipo vizuri . Ukienda na fundi janja janja mpenda pesa atakuchomesha atachukua pesa kwako na kwa hao wauza magari kwani kuna ishara atapewa arudi baadae kuja kuchukua mzigo wake. Hiyo habari ya km achana nayo kabisa utapotea. Unakuta gari ya mwaka 1995 imeletwa hapa kwetu 2022 halafu eti imetembea km 10,000 si maajabu hayo.
Ya kwangu ni ya mwaka 2000, wakati naagiza Japan ilisoma km 17,000, mwaka wa sita sasa ndo ipo km 62,000.......kununua gari yenye zaidi ya km laki moja naona ni kama kujilipua.​
 
Serikali itupie macho uhuni unaofanywa na hawa wafanyabiashara wa magari wenye asili ya Pakistan.

Jana mida ya saa sita mchana tulienda na rafiki yangu kwenye moja ya maduka (yard) ya kuuzia magari. Rafiki yangu alikuwa anataka Toyota Probox kwa ajili ya kubebea mizigo yake Kariakoo na kwenye godown yake.

Tukafika hiyo saa sita tukakuta magari ndiyo yanapangwa. Walivyomaliza tukaomba kukagua gari moja. Kijana akaitwa akaja mbio na funguo za gari zikiwa mkononi kwake.

Nikakaa kwenye usukani na rafiki yangu pembeni. Nilipoiweka gari switch on nikakuta odometer inasoma gari imetembea kilometa 219,551. Bei milioni 16

Tukashauriana tukasema hapana hili gari halifai. Tukaendelea duka jingine na jingine na jingine.

By saa tisa tukafudi tena kwenye ile Probox, tukakuta ishachezewa odometer, sasa inaonekana imetembea kilometa 46,755.

Nilikuwa nimeoiga picha chasis namba mlangoni na dashboard. Nikipowauliza mbona hii gari mmeichezea kilometa, nikawaonyesha na picha wakakasirika sana wakapora simu yangu. Nikawaambia kaeni nayo, leo mtalala polisi.

Nikawa naondoka kulekea kwenye gari tuliyokuja nayo hapo yard, ndipo mmoja ya wafanyabiashara wale akaja mbio huku akinibembeleza nifute zile picha watatupa million moja.

Hela tamu, tukakubali kufuta picha, tukabeba milioni yetu. Tukaondoka.

Lakini backyard ya hizo yard zote kuna mafundi wako busy wanayaweka sawa mamikweche hayo.

Kingine tulichogundua ni kwamba kwenye minada ya magari, magari ya nauzwa kwa classes. Hawa wanachagua class duni kabisa, yakifika hapa wanaongea vizuri na wakaguzi, wanatolewa bandarini.

Kwa somo hili tulilojifunza jana rafiki yangu amekata tamaa kabisa na magari haya. Sasa kaona bora aagize kutoka Japan 🗾 asubiri siku 45 abebe mwana wake wa uhakika
Nazani pia ni hapo morocco unaozungumzia

Nilishakuta wanamafundi wengi na wanatest magari kila mda mabovu

Nikashangaa wanatengeneza gari kitu very important na ngumu kuharibika kwa gari mpya lakini mafundi wanatengeneza ili wamtumie mteja

Gari zao mbovu kabisa

Sasa sijui ni batch au gari zao zote mbovu
 
Na idara ya Usalama wa Taifa haiko mbali na madudu haya
 
Back
Top Bottom