Serikali: Walimu 52,551 kuneemeka na upandishaji madaraja kwa njia ya mserereko

Serikali: Walimu 52,551 kuneemeka na upandishaji madaraja kwa njia ya mserereko

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Nchi, Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete wakati anajibu maswali yaliyoulizwa na Mbunge wa Ngara Ndg. George Ruhuro Bungeni Dodoma.

Akieleza Naibu Waziri Kikwete amesema kuwa baada ya uhakiki wa taarifa za walimu ilibainika kuwa Walimu wapatao 52,551 wamefuzu vigezo vya kupandishwa madaraja ikiwemo Walimu 148 wa Halmashauri ya Ngara na wengine 54442 ambao walikuwa hawajapangwa katika madaraja ya kimshahara wakiwemo Walimu 540 watapangwa katika madaraja husika kwa njia ya Mserereko.

Walimu walioajiliwa mwaka 2014 Mpaka sasa wanadaraja Moja tu walilopanda na viongozi wanaliona hilo. Shida siasa zimetawala kwenye maisha ya watu
Kwani kuna kada iliyoajiriwa 2014 ina daraja zaidi ya moja?!
 
Walimu walioajiliwa mwaka 2014 Mpaka sasa wanadaraja Moja tu walilopanda na viongozi wanaliona hilo. Shida siasa zimetawala kwenye maisha ya watu
Nimeshangaa sana naibu waziri kuongelea walimu wa 2013 wakati hawa walipanda 2019 na pia mwaka 2023 wamepanda,wakati walimu wa 2014 na 2015 toka wameajiliwa hadi leo hii wana daraja moja tu wakati walitakiwa kuwa wanalotafuta daraja la tatu.
 
View attachment 2953361
kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Nchi, Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete wakati anajibu maswali yaliyoulizwa na Mbunge wa Ngara Ndg. George Ruhuro Bungeni Dodoma.

Akieleza Naibu Waziri Kikwete amesema kuwa baada ya uhakiki wa taarifa za walimu ilibainika kuwa Walimu wapatao 52,551 wamefuzu vigezo vya kupandishwa madaraja ikiwemo Walimu 148 wa Halmashauri ya Ngara na wengine 54442 ambao walikuwa hawajapangwa katika madaraja ya kimshahara wakiwemo Walimu 540 watapangwa katika madaraja husika kwa njia ya Mserereko.
Walimu ndiyo kada pekee inayo dharaulika, kupunjwa, kuminywa haki za msingi, kutumikishwa kwa malipo duni, isiyo heshimika na serikali.

Ndiyo kada pekee yenye kutukanwa, kuagizwa na kufokewa na kila kiongozi hata kiongozi wa mtaaa.

Mshahara alio anza nao 2014 anaambulia nyongeza ya 130,000/=
Hatimaye anaishi kinyonge, mchafu kunuka, nyumba duni, nauri kukopa, mavazi duni, kutomidu bili ya umeme, maji, madeni lukuki.

Anaamua kuwa MLEVI Maana ndoto zimezima.

Huku wanasiasa na viongozi wa serikalini wakifurahia maisha na kulaumu walimu walivyo wavivu kwa kutojituma kufundosha muda wa nje ya kazi na weekend.
 
WALIMU 52551 KUNEEMEKA NA UPANDISHAJI MADARAJA KWA NJIA YA MSEREREKO -KIKWETE

kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Nchi, Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete wakati anajibu maswali yaliyoulizwa na Mbunge wa Ngara Ndg. George Ruhuro Bungeni Dodoma.

Akieleza Naibu Waziri Kikwete amesema kuwa baada ya uhakiki wa taarifa za walimu ilibainika kuwa Walimu wapatao 52,551 wamefuzu vigezo vya kupandishwa madaraja ikiwemo Walimu 148 wa Halmashauri ya Ngara Na wengine 54442 ambao walikuwa hawajapangwa katika madaraja ya kimshahara wakiwemo Walimu 540 watapangwa katika madaraja husika kwa njia ya Mserereko.

#NeemaZaAwamu6 #KaziInaendelea
 
Attachments

  • WhatsApp Video 2024-04-03 at 10.30.43 PM.mp4
    15.8 MB
  • WhatsApp Image 2024-04-03 at 10.31.00 PM.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-03 at 10.31.00 PM.jpeg
    125.8 KB · Views: 24
  • IMG_5196kjuyt.jpg
    IMG_5196kjuyt.jpg
    445 KB · Views: 25
Back
Top Bottom